Songwe: Mwalimu auwawa akizuia mifugo isipite katikati ya Shule

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Galula wilayani Songwe, Nisetas Dimoso amefariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji, kufuatia jitihada zake za kuzuia mifugo kupita ndani ya eneo la shule.

Mwalimu Dimoso alifariki dunia Julai 28, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya majeraha aliyodaiwa kuyapata baada ya kushambuliwa usiku wa Julai 26, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo lilianza baada ya vijana wawili kujaribu kupitisha mifugo katikati ya eneo la Shule ya Sekondari Galula, jambo ambalo mwalimu huyo alilizuia na kusababisha mabishano yaliyopelekea ugomvi. Inadaiwa mmoja wa vijana hao aliwaita watu wengine wanaodaiwa kuwa wamiliki wa mifugo waliokuwa jirani, ambao walifika eneo hilo na kumshambulia mwalimu huyo kwa kipigo kabla ya kutoweka.

Baada ya kushambuliwa, walimu na wananchi walimuwahisha Mwalimu Dimoso katika Kituo cha Afya Mbuyuni kwa huduma ya kwanza, kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa matibabu zaidi ambako baadaye alifariki dunia.

Diwani wa Kata ya Galula, Mikozi Mwavilundo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema linawahusisha watu wanaodaiwa kutoka katika familia ya mtu ambaye jina lake limehifadhiwa. Amesema taarifa zilitolewa mapema katika Kituo Kidogo cha Polisi Galula, lakini hadi sasa hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa licha ya baadhi yao kudaiwa kufahamika.

Ameongeza kuwa hilo ni tukio la pili la kushambuliwa kwa mtumishi katika eneo hilo, baada ya mtendaji wa kitongoji katika kijiji hicho kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji mwezi Machi mwaka huu na kupoteza maisha.
 
Apumzike kwa Amani Mwl. Dimoso
 
Back
Top Bottom