Songwe: TARURA yakamilisha kivuko, chagharimu Tsh. Milioni 207 huko Momba

Songwe: TARURA yakamilisha kivuko, chagharimu Tsh. Milioni 207 huko Momba

Serikali tafuteni pesa mjenge Daraja la Kudumu kubwa sio hivi vivuko vya boda boda japo Kwa kuanzia sio mbaya sana.

View: https://www.instagram.com/reel/Cyk0lp6MfNV/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
203354568.jpg
1403118784.jpg
-1425067752.jpg
 
Kivuko hicho muhimu kinaunganisha maeneo na Mjini na Vijijini.

Hiki hapa;


====

Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe wameunganishwa baada ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kukamilisha ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu katika mto Nyamba chenye urefu wa mita 115 na kuunganisha Kata za Ivuna na Mkomba kuelekea Wilaya ya Songwe.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Momba, Mhandisi Yusuph Shaban amesema kuwa kivuko hicho cha waenda kwa miguu ambacho kimegharimu kiasi cha Shilingi milioni 207 kimeweza kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwani sasa wananchi wataweza kuvuka katika kipindi chote cha mwaka na ameeleza kuwa mpango wa TARURA katika Wilaya hiyo ni kuhakikisha linajengwa daraja la kudumu litakalokuwa na uwezo wa kupitisha mizigo.

“Eneo hili lilikua ni changamoto kwa wananchi maana kuvuka upande wa pili ilikuwa vigumu hasa kipindi cha masika lakini sasa kivuko hiki kimekuwa mkombozi na tuna mpango wa kujenga daraja la kudumu litakalopitisha mizigo ili wananchi wa meneo haya waweze kusafirisha mazao yao, kuna mazao kama alizeti, ufuta, mtama na mazao mengine yanayotakiwa kutolewa mashambani na kupelekwa sokoni’’, amesema Mhandisi Yusuph.

Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Ivuna, Mhe. Erick Mkamba amesema kuwa daraja hilo limekuwa muhimu kwani wananchi sasa wanaweza kuvuka na kuzifikia huduma za kijamii kiurahisi na ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea daraja hilo.

“Tunapongeza jitihada za Serikali kupitia TARURA kwa ujenzi wa kivuko hiki ambapo wananchi wanavuka upande wa pili kwa urahisi, ombi langu kwa Serikali ni kujenga daraja la kudumu la moja kwa moja kwani maeneo haya kuna mazao mengi yanayotakiwa kufikishwa sokoni’’, amesema Mhe. Erick.

Naye Bi. Honorata Emily, Mkazi wa Kijiji cha Ivuna ameishukuru Serikali kwa kuwajengea kivuko hiko kwani hapo awali wananchi walikuwa wanapata shida kuvuka kutokana na maji mengi kujaa hasa kipindi cha mvua na kusababisha akina mama wengi kujifungulia njiani na pia hata wanafunzi walishindwa kuvuka kwenda shuleni.

Tanzania Web
Najua unabeza ila hapo Tarura wapo gezwe ,mita 115 kwa.hiyo pesa ni kidogo Sana.

Serikali tafuteni pesa za kujenga Daraja la Kudumu.
 
Wewe Kwa akili Yako hizo nguzo unajua ni sh.ngapi? Acha upuuzi wewe ,unajua mita 115 wewe?
Sasa bro mbona unanitukana aisee, kwani kuna popote nimeuliza kwa kutukana? Kama kujibu bila matusi ni shida then usijibu. Pia elewesha nguzo moja imetumia nondo mia za labda MM 16, cement mifuko 1000 na chuma kile kiasi kadhaa, pia pale pana mbao labda 500 za mninga za sh 50,000 kila moja. Kwa vile tarura ni wajenzi naamini wamejenga wenyewe. Hawajaoutsorce nguvu kazi maana ina wafanya kazi au?
 
Back
Top Bottom