Songwe: TARURA yakamilisha kivuko, chagharimu Tsh. Milioni 207 huko Momba

Songwe: TARURA yakamilisha kivuko, chagharimu Tsh. Milioni 207 huko Momba

Daraja za hivi tumezoea kuona kwenye movie za vita kama ile ya Rambo
Huyu hapa

Screenshot_2023-10-14-09-34-45-1.png
 
Najua unabeza ila hapo Tarura wapo gezwe ,mita 115 kwa.hiyo pesa ni kidogo Sana.

Serikali tafuteni pesa za kujenga Daraja la Kudumu.
Sometimes ukiwa neutral uwa na mawazo positive sana but hilo hicho kiasi kingelikuwa ni kipindi cha Magu ungelipiga kelele sana.
Kwenye hilo daraja gharama kubwa itakuwa Kwenye piles (nguzo za kwenda chini ya ardhi hadi kukutana na tabaka gumu).
Hapa naungana nawewe kuwapongeza TARURA
 
Sometimes ukiwa neutral uwa na mawazo positive sana but hilo hicho kiasi kingelikuwa ni kipindi cha Magu ungelipiga kelele sana.
Kwenye hilo daraja gharama kubwa itakuwa Kwenye piles (nguzo za kwenda chini ya ardhi hadi kukutana na tabaka gumu).
Hapa naungana nawewe kuwapongeza TARURA
Hakuna gharama kubwa,nipige kelele kisa ni Magufuli au? Kwanza yule alikuwa anaharibu miradi Kwa kulazimisha gharama za chini amabzo kiuhalisia hazipo.

Matokeo yake expansion joint,pamoja na kudanganya gharama ziliongezeka lakini mradi ulijengwa chini ya kiwango.
 
Hakuna gharama kubwa,nipige kelele kisa ni Magufuli au? Kwanza yule alikuwa anaharibu miradi Kwa kulazimisha gharama za chini amabzo kiuhalisia hazipo.

Matokeo yake expansion joint,pamoja na kudanganya gharama ziliongezeka lakini mradi ulijengwa chini ya kiwango.
Hilo la gharama za chini ni tatizo kubwa sana na ndilo likaleta mdudu was force account. Jamii ilihaminushwa ujenzi ni cheap tu, watendaji wa serikali na mashirika ya uma waliogopa kufanya ujenzi kwa hofu ya kutumia gharama (halisi) kubwa na kupelekea kusumbuliwa na takakuru.
Mama inabidi halitoe hili zimwi la force account
 
Kivuko hicho muhimu kinaunganisha maeneo na Mjini na Vijijini.

Hiki hapa;


====

Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe wameunganishwa baada ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kukamilisha ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu katika mto Nyamba chenye urefu wa mita 115 na kuunganisha Kata za Ivuna na Mkomba kuelekea Wilaya ya Songwe.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Momba, Mhandisi Yusuph Shaban amesema kuwa kivuko hicho cha waenda kwa miguu ambacho kimegharimu kiasi cha Shilingi milioni 207 kimeweza kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwani sasa wananchi wataweza kuvuka katika kipindi chote cha mwaka na ameeleza kuwa mpango wa TARURA katika Wilaya hiyo ni kuhakikisha linajengwa daraja la kudumu litakalokuwa na uwezo wa kupitisha mizigo.

“Eneo hili lilikua ni changamoto kwa wananchi maana kuvuka upande wa pili ilikuwa vigumu hasa kipindi cha masika lakini sasa kivuko hiki kimekuwa mkombozi na tuna mpango wa kujenga daraja la kudumu litakalopitisha mizigo ili wananchi wa meneo haya waweze kusafirisha mazao yao, kuna mazao kama alizeti, ufuta, mtama na mazao mengine yanayotakiwa kutolewa mashambani na kupelekwa sokoni’’, amesema Mhandisi Yusuph.

Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Ivuna, Mhe. Erick Mkamba amesema kuwa daraja hilo limekuwa muhimu kwani wananchi sasa wanaweza kuvuka na kuzifikia huduma za kijamii kiurahisi na ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea daraja hilo.

“Tunapongeza jitihada za Serikali kupitia TARURA kwa ujenzi wa kivuko hiki ambapo wananchi wanavuka upande wa pili kwa urahisi, ombi langu kwa Serikali ni kujenga daraja la kudumu la moja kwa moja kwani maeneo haya kuna mazao mengi yanayotakiwa kufikishwa sokoni’’, amesema Mhe. Erick.

Naye Bi. Honorata Emily, Mkazi wa Kijiji cha Ivuna ameishukuru Serikali kwa kuwajengea kivuko hiko kwani hapo awali wananchi walikuwa wanapata shida kuvuka kutokana na maji mengi kujaa hasa kipindi cha mvua na kusababisha akina mama wengi kujifungulia njiani na pia hata wanafunzi walishindwa kuvuka kwenda shuleni.

Tanzania Web
Ma QS wa JF tupeni rough cost estimates hapo.
 
Back
Top Bottom