Songwe: Vifusi vilivyokuwa kero Barabara ya Sogea-Machinjioni (Tunduma) vyasambazwa

 Songwe: Vifusi vilivyokuwa kero Barabara ya Sogea-Machinjioni (Tunduma) vyasambazwa

SAUTIYANGU

New Member
Joined
Oct 23, 2024
Posts
4
Reaction score
2
Vifusi vilivyowekwa barabarani kwa muda mrefu katika Barabara ya Sogea - Machinjioni katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma na kusababisha kero kwa Wananchi vimesambazwa na kutatua kero hiyo kwa kuanza utengenezaji wa Barabara inayotarajiwa kutengenezwa kwa kiwango cha lami.

Ni siku nne baada ya kero hiyo kuwasilishwa hapa kwenye jukwaa letu la JamiiForums, awali malalamiko yetu ilikuwa vifusi hivyo vilivyodaiwa kukaa kwa zaidi ya Miezi 3.

Vifusi hivyo vilisababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo hasa wafanyabiashara wa nyama wanaolazimika kusafirisha nyama kutoka machinjioni hadi Buchani.

Pia, soma: - KERO - Vifusi barabara ya Sogea Machinjioni (Songwe) vinaleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo
20241106_135146.jpg

20241106_135152.jpg

20241106_135314.jpg
 
Back
Top Bottom