Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Waungwana hivi zile pesa tunazolipa wakati wa kuingia kwenye vyoo hasa maeneo ya Stand zinafanya kazi gani?
Maana vyoo vingi vya Umma vina changamoto ya usafi na ukosefu wa maji bila kusahau ubovu wa miundombinu, nimeona mara kadhaa hapa JF watu wamekuwa wakiripoti kero hiyo kisha kisha wenye Mamlaka wanajitokeza kufanya usafi, kwanini iwe hivyo kila mara?
Nikiwa katika safari zangu nikapita Stendi ya Mabasi ya Tunduma pale maeneo ya Mpemba, nikaingia Chooni mimi na abiria wenzangu, tulichokikuta huko kwa kweli hali ni Mbaya kutokana na mazingira mabovu.
Vyoo havina majina, milango ni mibovu, vyumba vingine ndani ya choo havina milango kabisa, mapima yanayotumika kuhifadhi maji ni machafu kama ilivyo kwa ndoo zilizomo humo ndani lakini ajabu zoezi la kukusanya pesa linaendelea kama kawaida.
Nililipa Shilingi 200 kuingia lakini nilichokiona ni kama nililipa hela ili niingie kupata magonjwa ya kuambukiza ndani ya vyoo hivyo.
Halmashauri ya Mji wa Tunduma tunawaomba basi jitahidini kuweka miundombinu ya maji kwenye hizo Toilet, lasivyo mnakaribisha magonjwa ambukizi.