Songwe: Watu 24 wakamatwa wakizingira kituo cha polisi

Songwe: Watu 24 wakamatwa wakizingira kituo cha polisi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Polisi mkoani Songwe wanawashikilia watu 24 wa Kijiji cha Chang'ombe wilayani Songwe kwa tuhuma za kuzingira kituo cha polisi Galula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amesema watu hao walivamia kituo wakishinikiza kurejeshewa mikoba ya waganga wa jadi (lambalamba) iliyokamatwa na askari wa kituo hicho.

Amesema watu hao walikizingira kituo hicho Novemba 22, 2021 alfajiri baada ya askari kuzuia kazi za lambalamba wanaowadhalilisha watu wakiwatuhumu ni wachawi.

Amesema kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji na watu wengine 23 wanashikiriwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba akiwa Mji Mdogo wa Mlowo aliwataka wakazi wa mkoa huo kuachana na wapiga ramli chonganishi wakiwamo lambalamba.

MWANANCHI
 
Cha kujifunza: "Wangechukua mikoba ndani na kuondoka badala ya kusubiria nje."
 
Wanyakyusa jaman [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama wako salama itakua walienda kuzingira kwenye ktuo kisicho na silaha. Laa sivyo ungeskia watu wasiojulikana waliojaribu kuvamia kituo Cha polisi wawili wameuwawa na wengine kujeruhiwa
 
Hao polisi wazembe wangeua hata watatu wangekuwa na nidhamu hao watu
 
Halafu tunataka maendeleo huku tukiwa tunaendekeza imani za kishirikina!! Tukiambiwa sisi ni "shit hole society" na Wazungu tusiwalaumu.
 
Polisi mkoani Songwe wanawashikilia watu 24 wa Kijiji cha Chang'ombe wilayani Songwe kwa tuhuma za kuzingira kituo cha polisi Galula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amesema watu hao walivamia kituo wakishinikiza kurejeshewa mikoba ya waganga wa jadi
Hizo ndizo imani zetu za kale tuwape uhuru wa kuabudu
 
Wanyakyusa jaman [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sio kila ukisikia Songwe akili inakutuma ni Wanyakyusa.! Makabira makubwa mkoa wa Songwe ni Wanyiha na Wanyamwanga. Mbeya ni Wasafwa, Wanyakyusa na Wandali.
Be a knoledge seeker!
 
Back
Top Bottom