Pre GE2025 Songwe yabubujikwa na machozi ya furaha na kumshukuru Rais Samia baada ya kupewa Majiko ya Gesi ya Ruzuku

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpuuzi mkubwa wewe , unampa mtu cylinder pesa ya kufanya refill hana unatarajia nini?

Kwanini serikali na huyo mama yenu wasingeteneze mazingira rafiki kusambaza hiyo gesi majumbani kupitia pipes watu walipie kwa mwezi kuliko hizo drama wanazofanya.

Hao watu kama hawakuwa na uwezo wa kununua hizo cylinder mwanzo hadi wakapikia kuni maana yake waliona hawamudu kupata pesa ya kununua cylinder ya kufanya refill tumia akili wewe kunguni wa mama Abduli.
Kama umeumia jinyonge tu UFE
 
Wananchi wanahitaji ajira, huduma mzuri na nafuu za afya, elimu, umeme, maji na pasipe na mfumuko wa juu wa vyakula.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa Hakika Rais Samia ni Chaguo La Mungu,Kwa hakika Mama Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe,Kwa hakika Mama alikuja kulipa Furaha Taifa hili ,kwa hakika Mama alikuja Kwa Makusudi Maalumu Hapa Duniani,Kwa hakika Mama Samia Ana Sehemu yake Katika Mioyo ya watanzania Ambayo huwezi kukaa na Kumuondoa wewe Mtu mwingine.

Haijapata Kutokea Watu wanaimba jina la Rais mitaani kote Utafikiri wimbo wa Taifa,haijapata kutokea RAIS anapendwa na watanzania Utafikiri ni Mama Mzazi wa Kuwazaa Watanzania wote. Rais Hakauki midomoni mwa Watu utafikiri chemchemi ya maji inatiririka midomoni mwa watanzania.

Songwe Imejikuta ikibubujikwa na machozi ya Furaha na kumshukuru Rais Samia Baada ya kupewa Majiko ya Gas yaliyojaa hadi juu kwa Bei ya Ruzuku sawa na Bure kabisa. Zoezi hilo la kugawa majiko hayo ya Gas limefanywa na REA mkoani Songwe na kuwaacha mamia kwa mamia ya wananchi wakishangilia mitaani kote na katika barabara zote huku wakiwa wamebeba majiko yao kichwani Utafikiri bendera ya uhuru iliyowekwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kupepea muda wote.

Watu wengine wamefikia hatua ya kubeba mabango ya Rais Samia na kutembea nayo Mitaani na kutamka waziwazi bila hofu kuwa Mama Samia ndiye Rais wa Mioyo ya watanzania,Ndiye kipenzi chao na ndiye chaguo lao. Wakati hayo yakifanyika watu mbalimbali wamekuwa wakishangilia kwa kelele za shangwe na Nderemo kuishangilia picha ya Rais Samia na kuiinua juu juu na kuimba RAIS Rais RAIS Rais MaMa Mama Mama Mama .

Kwa hakika usishindane na aliyepewa kibali na Mungu na wala huwezi kumshinda wala kumshusha aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu.View attachment 3234447

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mitungi ya gesi isiyokwisha gesi na ikiisha gesi mtafuteni tena mama
 
Hivi kweli Lucas huwa unajielewa!? Ni kujitoa ufahamu, uvivu wa kufikiri, ama vyote kwa pamoja!?

Hivi raia kupewa bure jiko la gesi ndiyo habari kubwa ya kusifia!? Je! Hao wanaCCM waliohongwa hayo majiko, ni wangapi wanaweza kumudu gharama za kuzidi kuyatumia!?
 
Kwahyo wanaacha kupunguza bei ya Gesi, Wanagawa Mitungi ya Gesi.

Hapa ndo tumefikiri mpaka mwisho?
 
Hivi kweli Lucas huwa unajielewa!? Ni kujitoa ufahamu, uvivu wa kufikiri, ama vyote kwa pamoja!?

Hivi raia kupewa bure jiko la gesi ndiyo habari kubwa ya kusifia!? Je! Hao wanaCCM waliohongwa hayo majiko, ni wangapi wanaweza kumudu gharama za kuzidi kuyatumia!?
Acha wivu wako wewe. Umewahi wasaidia wangapi kupata majiko ya Gas?
 
Back
Top Bottom