Sonko arrested in Voi ‘while escaping arrest’

Kuna tofauti kubwa sana kwenye mienendo ya hao watu wawili...
 
Hiyo kweli, kuna mmoja kaghushi vyeti na kutumia hadi jina la mtu mwengine mpaka leo.

Hawa wote kwangu mimi ni Plus or Minus,
Kinachomgharimu bashite ni uwezo wake mdogo wa Kufikiri,
Ila mike sonko hapana, Imagine mtu ni Kiongozi anafanya matanuzi na show off za maana huku amezungukwa na wananchi maskini, this is too much, toeni hii Takataka
 
Jamaa aliishi maisha expensive kama drug lord!
 
Sonko amenichekesha..kapiga yowe original
 

Attachments

  • 254725242353_status_43f9383095944366b1b48bd0d628f515.mp4
    2.9 MB
LOL walikua wanamkagua kama tayari huko gerezani manunda wameshafanya yao
 

Inawezekana, hivyo ukaribu wao na Mkuu wa Nchi wasijidanganye. Itafika siku watatoswa na mkubwa kabisa anayewakingia kifua. Hivyo waishi kwa machale na akili nyingi kuwa siku ya siku inaweza kutokea hasahasa ktk masuala haya ya siasa na uongozi.
 
Gavana wa Nairobi apandishwa kizimbani, akana mashtaka yanayomkabili

Gavana wa jiji la Nairobi nchini Kenya Mike Mbuvi Sonko, amekana mashtaka yanayomkabili, ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi unaohusisha mamilioni ya dola, wakati alipofikishwa mahakamani mapema leo.

Sonko alitiwa nguvuni siku ya Ijumaa akituhumiwa pamoja na mambo mengine, kula njama ya kufanya ufisadi, kushindwa kufuata sheria zinazohusu taratibu za manunuzi na kumiliki mali ya umma kinyume cha sheria.

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka wa Kenya, DPP Noordin Haji amemtuhumu Mike Sonko na wasaidizi wake kuwa wamehusika na matumizi mabaya ya shilingi milioni 357 za Kenya, ambazo ni sawa na dola milioni 3.52 za Marekani.

Meya huyo wa jiji la Nairobi ambaye ni mwanachama wa chama tawala cha Jubilee, alisema katika taarifa aliyotoa hapo jana kuwa, kukamatwa kwake kumetokana na sababu za kisiasa na kwamba yeye ni raia anayetii sheria.

Kupitia taarifa yake hiyo iliyoandikwa kwa lugha mbili za Kiingereza na Kiswahili, Sonko amewahimiza wafuasi wake wajiepushe na vitendo ambavyo amesema "vinaweza kuhatarisha amani".

Aidha amesema, anawaomba wafuasi wake na hata maadui zake pia wamuombee dua.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa na hakimu mkazi mkuu Douglas Ogoti, gavana huyo wa jiji la Nairobi amewakilisha na jopo zito la mawakili wa Kenya, akiwemo kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti, Kipchumba Murkomen.

Sonko ni maarufu kwa mitindo yake maalumu ya mavazi, aina kwa aina za vito vya dhahabu anavyovaa na mikato yake maalumu ya nywele.

Polisi waliweka vizuizi na ulinzi mkali katika eneo linalozunguka mahakama ili kuzuia kutokea fujo baada ya wafuasi wa gavana huyo kutoa mwito wa kufanya maandamano.../

 
December 9, 2019
Nairobi, Kenya

Mahakamani Live : Gavana Mike Sonko kusalia rumande

Gavana wa Nairobi, Mike Mbuvi Sonko atasalia rumande hadi siku ya jumatano ambapo Mahakama ya Milimani jijini Nairobi itatoa uamuzi kuhusu ombi la kuachiliwa kwa dhamana. Mawakili wa Sonko wameishutumu Afisi ya Kiongozi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kwa kutumia mamlaka yake vibaya..
Source : Kenya CitizenTV
 
Huyu jamaa si nilisikia alishawahi kukamatwa yeye na mwenzie waititu kwa tuhuma za uvutaji bangi kwenye vyoo vya bunge
 
Huyu ukimfuatilia!
Hana kiwanda
Hana biashara yoyote inayonekana inayomuingizia fedha
Cha kujiuliza pesa anatoa wapi kufanya vurugu zake?????
Ndomana anangangania watu wa Hali ya chini awatumie kama mtaji

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…