Bantugbro
JF-Expert Member
- Feb 22, 2009
- 4,473
- 4,252
Kuna tofauti kubwa sana kwenye mienendo ya hao watu wawili...
Hapa nawaza hivi inawezekana siku moja Bashite mfalme wa Dar naye akatiwa pingu, au yule ni dogo wa mkulu, maana huboronga kupita maelezo na anapeta tu bila kuelekezwa kidole na mtu.
Sonko kwa kweli naye alipitiliza kwenye majigambo, ila kiaina nilikua nimeanza kumkubali pale alipokua anapambana na cartels za Nairobi, inawezekana hao ndio wamesuka haya yote ili azikwe hai, tatizo naye ana figisufigisu nyingi kiasi kwamba kumtolea nje nje ni kazi rahisi sana kwa cartels.