Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

wangshu

Member
Joined
May 26, 2021
Posts
72
Reaction score
83
Nawasalimu wote.

Kama mada inavyojieleza.

Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.

Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.

Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.

Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.

Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.

Natanguliza shukrani!
 
Acha ubinafsi wewe ,akija si ndo utabond naye, wasiwasi wako ni hivo vihela vya jamaa ambavyo mama wa huyo dogo kachangia kwa asilimia nyingi,huijui kesho,so mpokee mtoto,mlee Kama mwanao , mengine yatajiset, kausha huyo ndo lango la hela la baba yake,yangu ni hayo tu,btw hawez kula kila ya mchele kwa siku Mamie🤣🤣
 
Wanawake wengi we luck emotional intelligence.Huyo ni mtoto wa Mume wako na ameamua kumleta ndani .Card zote umeshikilia mkononi unataka kuwa mama wq kambo au no ?,unaitaka ndoa au no,unampenda Mume wako au no, unataka mumewe awe happy or no .Kama majibu yote no Vunja ndoa kama yes kaa kwenye ndoa .Na kwa wewe kuwa happy kwenye ndoa lazima Mume wako awe happy pia .Marriage ni institution kama Darasa Unaweza ingia au kutoka .
 
nina mtoto wa kambo, wife hataki nimlete. hiyo imeniletea shida sana kwasababu inabidi mara nyingi niwe nawasiliana na mama wa mtoto huyo na kujikuta tumesharudisha majeshi hadi kuogopa kupata mtoto mwingine wa pili. ila angekubali kuishi nami hiyo chain angeshaikata. wanawake kuweni na akili, kuna vitu vingine sio lazima uende shule cha pili, nakushauri usije kumtesa, utafungwa, pia usimbague kwasababu hata ufanyeje watoto wako wanajua hiyo ni damu yao wakiwa wazima utajikuta umelaumiwa, pia watoto wote wa kambo wanaoishi kwa kuteswa na mama wa kambo huwa wanafanikiwa kimaisha kuliko watoto wa ndani ya ndoa. amini usiamini.
 
Haya maisha hayana formula,binafis sina roho mbaya nahisi ninaweza mlea mtoto wa kambo bila chuki.ila iwapo huyo mtoto sikufichwa taarifa zake.

Wewe uliolewa umeshajulishwa huyo mtoto,mpokee umlee kama wako.kama ni wa kike usitegemee akupende na kukuheshimu. Hii ni nadra.

Kama ni wa kiume atakupenda na kukuheshimu.na hutojuta kumpokea mtoto huyo.
Mtoto wa kike wa kambo ni mzuri akiletwa akiwa mdogo.kama ni binti mkubwa lazima ukutane na vitibwi.

All in all wewe mpokee tu.cha kwanza muoneshe upendo.

Kama mmeo anakupenda na kukujali huna shida yeyote.mpokee dia. pole kwa hiyo sintofahamu.
 
Mkeo anakosea sana; ila wewe usitafute justification ya kulala na mzazi mwenzio kisa mawasiliano ya mtoto. Kama bado mnatakana, hata huyo mtoto akija kuishi na mkeo bado mtaendelea kupasha kiporo na huyo baby momma wako. Na kwa nini mliachana kama bado mnatakana? Kwa nini mkeo anamkataa mtoto, subiri agundue mnapasha kiporo, utaenjoy show

nina mtoto wa kambo, wife hataki nimlete. hiyo imeniletea shida sana kwasababu inabidi mara nyingi niwe nawasiliana na mama wa mtoto huyo na kujikuta tumesharudisha majeshi hadi kuogopa kupata mtoto mwingine wa pili. ila angekubali kuishi nami hiyo chain angeshaikata. wanawake kuweni na akili, kuna vitu vingine sio lazima uende shule. cha pili, nakushauri usije kumtesa, utafungwa, pia usimbague kwasababu hata ufanyeje watoto wako wanajua hiyo ni damu yao wakiwa wazima utajikuta umelaumiwa, pia watoto wote wa kambo wanaoishi kwa kuteswa na mama wa kambo huwa wanafanikiwa kimaisha kuliko watoto wa ndani ya ndoa. amini usiamini.
 
Bond, upendo utajengeka tu automatically kutegemea na ninyi wenyewe. Ila cha msingi ni mpokee na mtreat kama ambavyo unawatret watoto wako. Kila mzazi ana parenting style, so mlee kama unavyowalea watoto wako wengine. Kwa kuwa alikuwa analelewa na mama yake, inawezekana yakawa ni malezi ya aina tofauti na ya kwako; so kama kuna vya kubadilisha vibadilishe taratibu na kwa upendo na yeye anaweza akaadapt taratibu kadri anavyokaa na wadogo zake: kuna mengine hutoweza kuyabadili na as long as hayana tatizo basi unayaacha tu. Isijeonekana kana kwamba unajifamya wewe malezi yako ndiyo perfect kuliko ya mama yake; mkaanza matimbwili.

Yes kuanza kumlea mtoto ambaye tayari ana ufahamu wake sio rahisi sana tofauti na ukianza kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kuna watoto ni wema tu naturally, labda na mama yake ndiyo wale wenye hekima kashamwambia aje aishi na wewe vizuri so mtajikuta tu taratibu mambo yanakaa sawa.

Au anaweza akaja ashaambiwa kuwa mama wa kambo ni watesaji, au kashajazwa sumu kuwa huyu ndiyo kasababisha baba yako na mama yako wasiwe pamoja, so anakuja ameshajipanga. Don't fight with the kid, prove him/her wrong kwa moyo wako mweupe kwake. Ifike hatua mtoto mwenyewe aanze kujiuliza mbona niliyokuwa naambiwa sio nayoyaona. Akizidi kukuletea majaribu, mkabidhi baba yake.

Kama umeolewa kwenye familia yenye mawifi wanaojitambua basi kheri. Ila kama ndiyo umeolewa kwenye hizi familia zenye mawifi wasiostaarabika, jiandae kisaikolojia kuziba masikio na kujifanya bubu. Maana mawifi wanawatumiaga sana watoto wa kambo kujiingiza kwenye ndoa za kaka zao na kuleta mitafaruku, unless ukute mtoto ana akili akagoma kutumika au baba ni mkali akawanyamazisha dada zake. But all in all, mtreat vizuri huyo mtoto, akija kukushukuru baadaye sawa, asipokushukuru sawa pia; ila as long as ulimtendea mema wakati unatimiza wajibu wako, basi utakuwa na amani. Hata watoto wetu wa kuwazaa wengine hawana shukrani pia

Tatu usiwe defensive na epuka maneno yoyote ya kumkumbusha huyo mtoto kuwa si mtoto wako. Akikosea muadhibu kama mtoto aliyekosea sio ndiyo unaanza "aah umetumwa na mama ako eeh, ntakukomesha", sijui umenishinda tabia nenda tu kwa mama ako; mtoto wako akikushinda unampelekea nani? Kama ambavyo watoto wako wa kuwazaa wanaweza kuwa na tabia za ajabu, hata mtoto wa kambo anaweza kuwa na tabia za ajabu vilevile; so deal naye kama ambavyo ungedeal na mwanao wa kumzaa

Usiache kujiombea na kumuombea kama unavyowaombea watoto wako, akiwa mtoto mwema ni faida kwenu wote, na akiwa jaribu basi amini ni mzigo wenu nyote pia. Panda mbegu njema kwa huyo mtoto, regardlessly. Ombea amani ya nyumba yako na watoto wako wote.

Hayo mambo ya baba yake kusema sijui atapima DNA sijui hawajafanana, muachie baba mtoto. As long as kamleta nyumbani kwenu na kukwambia huyo ni mtoto wake, basi mpokee na kumlea vizuri.
 
Jambo zuri ni kwamba ulishaambiwa kabla hata hujaolewa na umeshiriki hata kwenye kumnunulia vitu huyu dogo. Ishi nae kama mwanao wa kumzaa wewe utakuja kuona faida yake huko mbeleni.

Kuna Rafiki yangu yeye alilelewa na Mama wa kambo kiroho safi. Sasa hivi huyu jamaa amemjengea nyumba huyu mama yake wa kambo kama shukrani maana walikuwa wanaishi kwenye nyumba ya kupanga, wazazi wa huyu jamaa wote walifariki akawa anaendelea kukaa vizuri na mama wa kambo hadi amekuja kupata kazi.
 
Dalili mbaya nilizoona kwenye maandishi yako

1.Ukijiona unaanza kujisemesha "ninge" "ange" "tunge"
2.Hapo ulipoandika ulifahamishwa kwamba kuna kakid ka nje dakika chache kabla ya ndoa
3.Kuongelea suala la DNA wakati hujui alipopita/anapopita huyo mume wako...hiyo ni mbinu tu kaitumia mume wako kukuchota akili ,huyo ni mwanae 100%
4.Bond,bond na mtu huwa inatengenezwa haijalishi mmekutana akiwa na umri upi

Kimsingi kama mwanaume kaamua kumleta mwanae hiyo ni dalili nzuri kwako,kakuamini...usivunje uaminifu na upendo uliopo kati yako na mume sababu ya mtoto

Kama una roho mbaya jitahidi upunguze ama kama utaweza uiache

Comment ya chapwa24 pia imenifunza jambo huko mbeleni nikukutana na jambo kama lako
 
Mkeo anakosea sana; ila wewe usitafute justification ya kulala na mzazi mwenzio kisa mawasiliano ya mtoto. Kama bado mnatakana, hata huyo mtoto akija kuishi na mkeo bado mtaendelea kupasha kiporo na huyo baby momma wako. Na kwa nini mliachana kama bado mnatakana? Kwa nini mkeo anamkataa mtoto, subiri agundue mnapasha kiporo, utaenjoy show
Imagine kupiga simu kila wakati kuulizia mtoto anaendeleaje, mara mpe simu mwanangu niongee naye, mara utume pesa unakuwa kama unahudumia familia mbili, kwa watu ambao mlishawahi kukutanisha vikojoleo mkipigiana simu mara moja mbili au ukienda kumtembelea mtoto kwa mamake, ni mara chache sana utakosa kukumbushia kama binadamu mwenye madhaifu.

Kukata mzizi wa fitna ni kuweka mazingira ya kutokuwa na sababu ya kuwasiliana. hata hivyo , kama yeye anaona hiyo ni issue mwache, kuna siku atakuta mtoto wa pili kwa mchepuko. na hilo litakuwa fundisho kwake, manake kama yeye ana watoto na yule ana watoto hapo kipimo kitakuwa nani bora kwasababu kote kuna watoto wa kutosha. nitaawaacha wapambane mbabe niendelee naye.ndivyo akili za wanaume zilivyo.

Unasema nisubiri agundue tunapasha kiporo...simwogopi hata nusu, na wala siwezi kukataa akiuliza, yeye mwenyewe nafikiri kama mtu mzima anajua kinachoendelea kama watu mnawasiliana mara kwa mara namna ya kulea mtoto wenu, kuna mengi mnaweza kujadili na kujadili na kukumbushana story n.k
 
Dalili mbaya nilizoona kwenye maandishi yako

1.Ukijiona unaanza kujisemesha "ninge" "ange" "tunge"
2.Hapo ulipoandika ulifahamishwa kwamba kuna kakid ka nje dakika chache kabla ya ndoa
3.Kuongelea suala la DNA wakati hujui alipopita/anapopita huyo mume wako...hiyo ni mbinu tu kaitumia mume wako kukuchota akili ,huyo ni mwanae 100%
4.Bond,bond na mtu huwa inatengenezwa haijalishi mmekutana akiwa na umri upi

Kimsingi kama mwanaume kaamua kumleta mwanae hiyo ni dalili nzuri kwako,kakuamini...usivunje uaminifu na upendo uliopo kati yako na mume sababu ya mtoto

Kama una roho mbaya jitahidi upunguze ama kama utaweza uiache

Comment ya chapwa24 pia imenifunza jambo huko mbeleni nikukutana na jambo kama lako
Tena sisi wanaume tulivyo. Tukija kusikia Mtoto ananyanyaswa na Mama wa kambo ule upendo na uaminifu huwa unakufa na ni rahisi sana mke mtesi kuja kuachwa.
 
Back
Top Bottom