Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Ndugu yangu kuna wanawake walihisi waume zao wakichukua watoto wao wa nje itawafanya watulie na ndoa zao, walikuja kushangaza baby momma ana watoto wengine na mume wake. Kuna watu waliamua kuachana seriously na wanawasiliana kwa ajili ya mtoto tu, mengine kila mtu anapambana na maisha yake. Mimi mume wangu hawezi piga simu kwa baby momma kila saa in the name of kumjulia hali mtoto; siruhusu huo upumbavu. Mawasiliano yawepo ila kuwe na mipaka, sio mtoto kakohoa simu, kapiga chafya simu. Hata mkimchukua mtoto, itakuwa zamu ya mama yake na yeye kupiga simu kwako kila wakati kumjulia hali kwa sababu umeshamzoesha hivyo. Huna justification my brother.

Na ukute mkeo kagundua kuwa mnapashana viporo ndiyo maana kagoma kumchukua na mtoto. Apambane yeye kulea afu nyie mkutane kufanyana kwa amani? Na kama unahisi anafahamu mnavyochepuka, unahisi ni mjinga sana karuhusu hilo au ndiyo kamuachia Mungu? Na kwa style hiyo jiandae kwa vita kati ya watoto wako, utafurahi kwa kweli. Wewe kuzaa njw humkomeshi mkeo bali watoto wako.

Huyo baby momma anaku-entertain kwa sababu bado anakutaka na yupo single; unafikiri angekuwa na mahusiano yake serious au ameolewa angekuruhusu upigepige simu kila wakati mbele ya mume wake? Baby momma kakuzidi akili na wewe unacheza tu beat lake, unavunja ndoa yako taratibu. Mwanaume mpumbavu hujisababishia kifo chake mwenyewe. Jikute sasa unamkomesha mkeo, mwisho wa siku utaona nani atakomesheka

C.c @espy
imagine kupiga simu kila wakati kuulizia mtoto anaendeleaje, mara mpe simu mwanangu niongee naye, mara utume pesa unakuwa kama unahudumia familia mbili, kwa watu ambao mlishawahi kukutanisha vikojoleo mkipigiana simu mara moja mbili au ukienda kumtembelea mtoto kwa mamake, ni mara chache sana utakosa kukumbushia kama binadamu mwenye madhaifu. kukata mzizi wa fitna ni kuweka mazingira ya kutokuwa na sababu ya kuwasiliana. hata hivyo , kama yeye anaona hiyo ni issue mwache, kuna siku atakuta mtoto wa pili kwa mchepuko. na hilo litakuwa fundisho kwake, manake kama yeye ana watoto na yule ana watoto hapo kipimo kitakuwa nani bora kwasababu kote kuna watoto wa kutosha. nitaawaacha wapambane mbabe niendelee naye.ndivyo akili za wanaume zilivyo.

unasema nisubiri agundue tunapasha kiporo...simwogopi hata nusu, na wala siwezi kukataa akiuliza, yeye mwenyewe nafikiri kama mtu mzima anajua kinachoendelea kama watu mnawasiliana mara kwa mara namna ya kulea mtoto wenu, kuna mengi mnaweza kujadili na kujadili na kukumbushana story n.k
 
Nampenda sana mama yangu japo si wa kunizaa.
Baba angu aliniiba kwa mama yangu mzazi nikiwa na miezi mi 3 tu duniani akanileta kulelewa kwa huyu mama ambae ndio mkewe wa ndoa.nikawa mtoto wake wa 5.Namkubali sana lich ya mapungufu yake ambayo wengine huwa wanalazimisha niyaone ila hata siyaonagi
 
Bado sijaona shida iko wapi,ila inaonekana unakauchoyo fulani na roho mbaya tofauti na hapo sijaona kutu cha kudoubt
 
Nampenda sana mama yangu japo si wa kunizaa.
Baba angu aliniiba kwa mama yangu mzazi nikiwa na miezi mi 3 tu duniani akanileta kulelewa kwa huyu mama ambae ndio mkewe wa ndoa.nikawa mtoto wake wa 5.Namkubali sana lich ya mapungufu yake ambayo wengine huwa wanalazimisha niyaone ila hata siyaonagi
Mi pia namfeel sana shangazi yangu kuliko hata mama yangu yaani alinichukua nikiwa mdogo lakini alinilea kama binti yake yaani mpaka kuna vitu nkikumbuka nabaki kujiuliza ntamlipa nini shangazi yangu alafu pia nilijifunza kwamba anaroho nzuri ya kuzaliwa nayo maana kuna watoto wa marehemu shemeji yake tulikuwa tukiishi nao lakini nao walikuwa kama watoto wake
 
Wanawake wengi we luck emotional intelligence.Huyo ni mtoto wa Mume wako na ameamua kumleta ndani .Card zote umeshikilia mkononi unataka kuwa mama wq kambo au no ?,unaitaka ndoa au no,unampenda Mume wako au no ,unataka mumewe awe happy or no .Kama majibu yote no Vunja ndoa kama yes kaa kwenye ndoa .Na kwa wewe kuwa happy kwenye ndoa lazima Mume wako awe happy pia .Marriage ni institution kama Darasa Unaweza ingia au kutoka .
Ndoa gani hio ndugu yangu unaweza kuingia nakutoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nampenda sana mama yangu japo si wa kunizaa.
Baba angu aliniiba kwa mama yangu mzazi nikiwa na miezi mi 3 tu duniani akanileta kulelewa kwa huyu mama ambae ndio mkewe wa ndoa.nikawa mtoto wake wa 5.Namkubali sana lich ya mapungufu yake ambayo wengine huwa wanalazimisha niyaone ila hata siyaonagi
Ulibahatika Sana mkuu,
Bila shaka Atakua Ni Mnene.

Kuna mdau mmoja aliwai sema,
"Wanawake wanene wanaupendo Sana na watoto hata ambao hawajawazaa"
 
Bond, upendo utajengeka tu automatically kutegemea na ninyi wenyewe. Ila cha msingi ni mpokee na mtreat kama ambavyo unawatret watoto wako. Kila mzazi ana parenting style, so mlee kama unavyowalea watoto wako wengine. Kwa kuwa alikuwa analelewa na mama yake, inawezekana yakawa ni malezi ya aina tofauti na ya kwako; so kama kuna vya kubadilisha vibadilishe taratibu na kwa upendo na yeye anaweza akaadapt taratibu kadri anavyokaa na wadogo zake: kuna mengine hutoweza kuyabadili na as long as hayana tatizo basi unayaacha tu. Isijeonekana kana kwamba unajifamya wewe malezi yako ndiyo perfect kuliko ya mama yake; mkaanza mtimbwili.

Yes kuanza kumlea mtoto ambaye tayari ana ufahamu wake sio rahisi sana tofauti na ukianza kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kuna watoto ni wema tu naturally, labda na mama yake ndiyo wale wenye hekima kashamwambia aje aishi na wewe vizuri so mtajikuta tu taratibu mambo yanakaa sawa.

Au anaweza akaja ashaambiwa kuwa mama wa kambo ni watesaji, au kashajazwa sumu kuwa huyu ndiyo kasababisha baba yako na mama yako wasiwe pamoja, so anakuja ameshajipanga. Don't fight with the kid, prove him/her wrong kwa moyo wako mweupe kwake. Ifike hatua mtoto mwenyewe aanze kujiuliza mbona niliyokuwa naambiwa sio nayoyaona. Akizidi kukuletea majaribu, mkabidhi baba yake.

Kama umeolewa kwenye familia yenye mawifi wanaojirambua basi kheri. Ila kama ndiyo umeolewa kwenye hizi familia zenye mawifi wasiostaarabika, jiandae kisaikolojia kuziba masikio na kujifanya bubu. Maana mawifi wanawatumiaga sana watoto wa kambo kujiingiza kwenye ndoa za kaka zao na kuleta mitafaruku, unless ukute mtoto ana akili akagoma kutumika au baba ni mkali akawanyamazisha dada zake. But all in all, mtreat vizuri huyo mtoto, akija kukushukuru baadaye sawa, asipokushukuru sawa pia; ila as long as ulimtendea mema wakati unatimiza wajibu wako, basi utakuwa na amani. Hata watoto wetu wa kuwazaa wengine hawana shukrani pia

Tatu usiwe defensive na epuka maneno yoyote ya kumkumbusha huyo mtoto kuwa si mtoto wako. Akikosea muadhibu kama mtoto aliyekosea sio ndiyo unaanza "aah umetumwa na mama ako eeh, ntakukomesha", sijui umenishinda tabia nenda tu kwa mama ako; mtoto wako akikushinda unampelekea nani? Kama ambavyo watoto wako wa kuwazaa wanaweza kuwa na tabia za ajabu, hata mtoto wa kambo anaweza kuwa na tabia za ajabu vilevile; so deal naye kama ambavyo ungedeal na mwanao wa kumzaa

Usiache kujiombea na kumuombea kama unavyowaombea watoto wako, akiwa mtoto mwema ni faida kwenu wote, na akiwa jaribu basi amini ni mzigo wenu nyote pia. Panda mbegu njema kwa huyo mtoto, regardlessly. Ombea amani ya nyumba yako na watoto wako wote.

Hayo mambo ya baba yake kusema sijui atapima DNA sijui hawajafanana, muachie baba mtoto. As long as kamleta nyumbani kwenu na kukwambia huyo ni mtoto wake, basi mpokee na kumlea vizuri.
Najaribu kufikiria wewe ni mwanamke wa namna gani vile ulivyojaa hekima naamini kabisa familia yako ni moja ya familia Bora na zenye furaha.

Mleta mada pamoja na ushauri mzuri wenzetu wanaoutoa hapa lakini ushauri wako huu naomba auchukue Kama jibu rasmi la mada yake hii.
 
Ndugu yangu kuna wanawake walihisi waume zao wakichukua watoto wao wa nje itawafanya watulie na ndoa zao, walikuja kushangaza baby momma ana watoto wengine na mume wake. Kuna watu waliamua kuachana seriously na wanawasiliana kwa ajili ya mtoto tu, mengine kila mtu anapambana na maisha yake. Mimi mume wangu hawezi piga simu kwa baby momma kila saa in the name of kumjulia hali mtoto; siruhusu huo upumbavu. Mawasiliano yawepo ila kuwe na mipaka, sio mtoto kakohoa simu, kapiga chafya simu. Hata mkimchukua mtoto, itakuwa zamu ya mama yake na yeye kupiga simu kwako kila wakati kumjulia hali kwa sababu umeshamzoesha hivyo. Huna justification my brother.

Huyo baby momma anaku-entertain kwa sababu bado anakutaka na yupo single; unafikiri angekuwa na mahusuano yake serious au ameolewa angekuruhusu upigepige simu kila wakati mbele ya mume wake? Baby momma kakuzidi akili na wewe unacheza tu beat lake, unavunja ndoa yako tarstibu. Mwanaume mpumbavu hujisababishia kifo chake mwenyewe. Jikute sasa unamkomesha mkeo, mwisho wa siku utaona nani atakomesheka

C.c @espy
Olewa na single father ikiwa umeshuhudia kaburi la baby moma. Lasivyo jiandae tu kwa yajayo yasiyofurahisha.
 
Nawasalimu wote.

Kama mada inavyojieleza.

Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.

Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.

Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.

Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.

Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.

Natanguliza shukrani!
Kwakweli ata mi nina mtoto wa nje na mke niliye nae sasa hajui siku nimwambie itakuwa kasheshe? Yani basi ujana maji ya mtoto,
 
Mkeo anakosea sana; ila wewe usitafute justification ya kulala na mzazi mwenzio kisa mawasiliano ya mtoto. Kama bado mnatakana, hata huyo mtoto akija kuishi na mkeo bado mtaendelea kupasha kiporo na huyo baby momma wako. Na kwa nini mliachana kama bado mnatakana? Kwa nini mkeo anamkataa mtoto, subiri agundue mnapasha kiporo, utaenjoy show
Walaa huyo mke hakosei, kulea mtoto yeyote asie wako ni kipaji. Kama amejigundua hana hicho kipaji its better alivyokataa kuliko akubali kumpokea kishingo upqnde halafu aje asimangwe kwa kumnyanyasa mtoto.
 
Back
Top Bottom