kitulike
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 286
- 648
Bond, upendo utajengeka tu automatically kutegemea na ninyi wenyewe. Ila cha msingi ni mpokee na mtreat kama ambavyo unawatret watoto wako. Kila mzazi ana parenting style, so mlee kama unavyowalea watoto wako wengine. Kwa kuwa alikuwa analelewa na mama yake, inawezekana yakawa ni malezi ya aina tofauti na ya kwako; so kama kuna vya kubadilisha vibadilishe taratibu na kwa upendo na yeye anaweza akaadapt taratibu kadri anavyokaa na wadogo zake: kuna mengine hutoweza kuyabadili na as long as hayana tatizo basi unayaacha tu. Isijeonekana kana kwamba unajifamya wewe malezi yako ndiyo perfect kuliko ya mama yake; mkaanza mtimbwili.
Yes kuanza kumlea mtoto ambaye tayari ana ufahamu wake sio rahisi sana tofauti na ukianza kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kuna watoto ni wema tu naturally, labda na mama yake ndiyo wale wenye hekima kashamwambia aje aishi na wewe vizuri so mtajikuta tu taratibu mambo yanakaa sawa.
Au anaweza akaja ashaambiwa kuwa mama wa kambo ni watesaji, au kashajazwa sumu kuwa huyu ndiyo kasababisha baba yako na mama yako wasiwe pamoja, so anakuja ameshajipanga. Don't fight with the kid, prove him/her wrong kwa moyo wako mweupe kwake. Ifike hatua mtoto mwenyewe aanze kujiuliza mbona niliyokuwa naambiwa sio nayoyaona. Akizidi kukuletea majaribu, mkabidhi baba yake.
Kama umeolewa kwenye familia yenye mawifi wanaojirambua basi kheri. Ila kama ndiyo umeolewa kwenye hizi familia zenye mawifi wasiostaarabika, jiandae kisaikolojia kuziba masikio na kujifanya bubu. Maana mawifi wanawatumiaga sana watoto wa kambo kujiingiza kwenye ndoa za kaka zao na kuleta mitafaruku, unless ukute mtoto ana akili akagoma kutumika au baba ni mkali akawanyamazisha dada zake. But all in all, mtreat vizuri huyo mtoto, akija kukushukuru baadaye sawa, asipokushukuru sawa pia; ila as long as ulimtendea mema wakati unatimiza wajibu wako, basi utakuwa na amani. Hata watoto wetu wa kuwazaa wengine hawana shukrani pia
Tatu usiwe defensive na epuka maneno yoyote ya kumkumbusha huyo mtoto kuwa si mtoto wako. Akikosea muadhibu kama mtoto aliyekosea sio ndiyo unaanza "aah umetumwa na mama ako eeh, ntakukomesha", sijui umenishinda tabia nenda tu kwa mama ako; mtoto wako akikushinda unampelekea nani? Kama ambavyo watoto wako wa kuwazaa wanaweza kuwa na tabia za ajabu, hata mtoto wa kambo anaweza kuwa na tabia za ajabu vilevile; so deal naye kama ambavyo ungedeal na mwanao wa kumzaa
Usiache kujiombea na kumuombea kama unavyowaombea watoto wako, akiwa mtoto mwema ni faida kwenu wote, na akiwa jaribu basi amini ni mzigo wenu nyote pia. Panda mbegu njema kwa huyo mtoto, regardlessly. Ombea amani ya nyumba yako na watoto wako wote.
Hayo mambo ya baba yake kusema sijui atapima DNA sijui hawajafanana, muachie baba mtoto. As long as kamleta nyumbani kwenu na kukwambia huyo ni mtoto wake, basi mpokee na kumlea vizuri.
Wewe dada nimekupenda bure, ni km ulikua unaandika nnachowaza.... asipouona ushaur huu bas hakuna ushauri mwingine utaomfaa