Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Haya maisha hayana formula,binafis sina roho mbaya nahisi ninaweza mlea mtoto wa kambo bila chuki.ila iwapo huyo mtoto sikufichwa taarifa zake.

Wewe uliolewa umeshajulishwa huyo mtoto,mpokee umlee kama wako.kama ni wa kike usitegemee akupende na kukuheshimu. Hii ni nadra.

Kama ni wa kiume atakupenda na kukuheshimu.na hutojuta kumpokea mtoto huyo.
Mtoto wa kike wa kambo ni mzuri akiletwa akiwa mdogo.kama ni binti mkubwa lazima ukutane na vitibwi.

All in all wewe mpokee tu.cha kwanza muoneshe upendo.

Kama mmeo anakupenda na kukujali huna shida yeyote.mpokee dia. pole kwa hiyo sintofahamu.
Ohoo! ni wa kike! kwahiyo ndio kusema hatanipenda! hahahhaa. Ukweli mume wangu ananipenda na anijali. Mtoto nampokea kwa roho nyeupe tu haina shida. Nilitaka kujifunza zaidi ili itakapofika muda niwe nimeshajifunza kama yapo ya kujifunza na ya kufanyia kazi
 
Kama unaroho mbaya basi utakuwa na wasiwasi kwani si anakuja kukaa kama wengine wanavokaa mbona unaanalyse vitu ambavyo havina umuhimu,nadhani utakuwa mbaguzi tuu
Sio mbaguzi ila maandalizi lazima yawepo. Unaweza kuchukulia kitu easy kumbe sio unavyofikiria. Ndio maana nikashea wajameni.
 
Bond, upendo utajengeka tu automatically kutegemea na ninyi wenyewe. Ila cha msingi ni mpokee na mtreat kama ambavyo unawatret watoto wako. Kila mzazi ana parenting style, so mlee kama unavyowalea watoto wako wengine. Kwa kuwa alikuwa analelewa na mama yake, inawezekana yakawa ni malezi ya aina tofauti na ya kwako; so kama kuna vya kubadilisha vibadilishe taratibu na kwa upendo na yeye anaweza akaadapt taratibu kadri anavyokaa na wadogo zake: kuna mengine hutoweza kuyabadili na as long as hayana tatizo basi unayaacha tu. Isijeonekana kana kwamba unajifamya wewe malezi yako ndiyo perfect kuliko ya mama yake; mkaanza mtimbwili.

Yes kuanza kumlea mtoto ambaye tayari ana ufahamu wake sio rahisi sana tofauti na ukianza kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kuna watoto ni wema tu naturally, labda na mama yake ndiyo wale wenye hekima kashamwambia aje aishi na wewe vizuri so mtajikuta tu taratibu mambo yanakaa sawa.

Au anaweza akaja ashaambiwa kuwa mama wa kambo ni watesaji, au kashajazwa sumu kuwa huyu ndiyo kasababisha baba yako na mama yako wasiwe pamoja, so anakuja ameshajipanga. Don't fight with the kid, prove him/her wrong kwa moyo wako mweupe kwake. Ifike hatua mtoto mwenyewe aanze kujiuliza mbona niliyokuwa naambiwa sio nayoyaona. Akizidi kukuletea majaribu, mkabidhi baba yake.

Kama umeolewa kwenye familia yenye mawifi wanaojirambua basi kheri. Ila kama ndiyo umeolewa kwenye hizi familia zenye mawifi wasiostaarabika, jiandae kisaikolojia kuziba masikio na kujifanya bubu. Maana mawifi wanawatumiaga sana watoto wa kambo kujiingiza kwenye ndoa za kaka zao na kuleta mitafaruku, unless ukute mtoto ana akili akagoma kutumika au baba ni mkali akawanyamazisha dada zake. But all in all, mtreat vizuri huyo mtoto, akija kukushukuru baadaye sawa, asipokushukuru sawa pia; ila as long as ulimtendea mema wakati unatimiza wajibu wako, basi utakuwa na amani. Hata watoto wetu wa kuwazaa wengine hawana shukrani pia

Tatu usiwe defensive na epuka maneno yoyote ya kumkumbusha huyo mtoto kuwa si mtoto wako. Akikosea muadhibu kama mtoto aliyekosea sio ndiyo unaanza "aah umetumwa na mama ako eeh, ntakukomesha", sijui umenishinda tabia nenda tu kwa mama ako; mtoto wako akikushinda unampelekea nani? Kama ambavyo watoto wako wa kuwazaa wanaweza kuwa na tabia za ajabu, hata mtoto wa kambo anaweza kuwa na tabia za ajabu vilevile; so deal naye kama ambavyo ungedeal na mwanao wa kumzaa

Usiache kujiombea na kumuombea kama unavyowaombea watoto wako, akiwa mtoto mwema ni faida kwenu wote, na akiwa jaribu basi amini ni mzigo wenu nyote pia. Panda mbegu njema kwa huyo mtoto, regardlessly. Ombea amani ya nyumba yako na watoto wako wote.

Hayo mambo ya baba yake kusema sijui atapima DNA sijui hawajafanana, muachie baba mtoto. As long as kamleta nyumbani kwenu na kukwambia huyo ni mtoto wake, basi mpokee na kumlea vizuri.
Asante sana kwa ushauri. Nimekuelewa vilivyo
 
Najaribu kufikiria wewe ni mwanamke wa namna gani vile ulivyojaa hekima naamini kabisa familia yako ni moja ya familia Bora na zenye furaha.


Mleta pamoja na ushauri mzuri wenzetu wanaoutoa hapa lakini ushauri wako huu naomba auchukue Kama jibu rasmi la mada yake hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri nimechukua. Amejibu kwa ufasaha na kistarabu sana. Kuna wengine wanakazana mimi sijui mchoyo, mbinafsi, sijui ndezi jamani Khaaa!
 
Bond watu wanatemgeneza tu, huwa hakuna wakati ambao mtu hudhamiria kufanya hivyo...

Mbona sisi tusiojuana hata kwa sura let say mi na Joanah , tumekutana tu kijiwe cha JF na unapata tume bond vizuri wakati hata sijui ako anafanana aje...

Wanadamu huwa tuna sifa moja, tumeumbwa/undwa kukutana na vitu vipya na kuvi own...

Ukiona li mtu lina mihasira hasira ujue kachagua kuwa hivyo, ukiona mtu mwenye roho nzuri naye halikadhalika kachagua kuwa hivyo...
 
Bibie kwani mumeo ulizaliwa nae hadi mkatengeneza bond? Kama mlikutana ukubwani na mkatengeneza bond basi amini kuwa bond inatengenezwa wakati wowote ule.

It seems hauko tayari kuwa mama wa huyu mtoto, ndio maana unajiuliza sana. Hata kuanzisha uzi pia ni dalili ya hilo.

Ulifahamu uwepo wake hata kabla ya ndoa yenu, je hamkujadiliana mstakabali wake? Kumfanyia shoping haimaanishi unamkubali, maana kama baba katoa pesa mwanae afanyiwe shoping nawe ndoa waitaka unadhani utafanya nini? Ungemuhitaji ungesisitiza aje angalau kipindi cha likizo ili mtengeneze hiyo bond ulokazana nayo.

Kama ndani ya nafsi yako unahisi kusita, unahisi hautokuwa mama bora kwa huyo mtoto its better ukamuacha kwa mama yake ila mkahakikisha mahitaji yake anayapata ipasavyo.
Mtoto ni wake yet mimi tena nimsisitizie aje likizo! naamini ilikuwa ni jukumu lake na hakuwahi kufanya hivyo. Yaan yeye alitakiwa awe mstari wa mbele. Mtoto sio wangu halafu ningeanzaje kusisitiza? Alitakiwa ajiongeze kwahiyo sidhani kama ilikuwa kosa langu. Mwanzoni kabisa baada ya kuniambia kuna mtoto niliimwambia amlete but akasema hataishi na sisi. Sikuona sababu ya kumlazimisha. Sasa baada ya miaka 10+ ndio anataka amlete na mimi sina shida na hilo. Nilitaka tu kupata mawili matatu kutoka hapa jamvini. Si unajua penye wengi pana mengi. Maisha ni funzo na kujifunza ni kitu endelevu
 
Ondoa hio negativity ya u mama wakambo kwanza! Pia utajaribu kuwa nae karibu kumjali kama mwanao wakumzaa japo kuna watoto wengine humezeshwa sumu na mamazao hata uwapende vipi! Mungu akusaidie mpatane
 
Ni kwa "NEEMA" tu [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Najaribu kufikiria wewe ni mwanamke wa namna gani vile ulivyojaa hekima naamini kabisa familia yako ni moja ya familia Bora na zenye furaha.


Mleta pamoja na ushauri mzuri wenzetu wanaoutoa hapa lakini ushauri wako huu naomba auchukue Kama jibu rasmi la mada yake hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema wanawake saa zngne mnaakili ndogo sana mm nililelewa Na mama wa kambo wawili tofauti huyo wa kwanza alinilea kama mwanae baadae akaachana na mzee akaja huyu funga kazi roho mbaya chuki na alipandikiza sumu hadi mshua akawa hanipendi kabsa kabsa lakini sikuhizi japokua sina maisha mazuri kvle naona anajifanya kunipenda kumbe unafki tu shenz kabsa.
 
Nawasalimu wote.

Kama mada inavyojieleza.

Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.

Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.

Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.

Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.

Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.

Natanguliza shukrani!
Unataka amtupe? Je angekuwa wako ungetaka amuweke wapi? Ni suala la busara na kutokuwa mbinafsi na mjinga kumkataa mtoto wa mwenzio.
 
Sema wanawake saa zngne mnaakili ndogo sana mm nililelewa Na mama wa kambo wawili tofauti huyo wa kwanza alinilea kama mwanae baadae akaachana na mzee akaja huyu funga kazi roho mbaya chuki na alipandikiza sumu hadi mshua akawa hanipendi kabsa kabsa lakini sikuhizi japokua sina maisha mazuri kvle naona anajifanya kunipenda kumbe unafki tu shenz kabsa.
Pole sana! maana kulelewa na mama wa kambo wawili hiyo nayo kali. Well mimi akili yangu sio ndogo lakini hahaha! Ila mimi naamini kukaa na mtoto akiwa mdogo inakuwa rahisi. Wengine wakishakuwa wakubwa nao wanaweza kuwa na perception zao kwamba mama wa kambo labda ni hivi na hivi anajikoki kabisa maana jamii nayo haichukulii mama wa kambo kama mtu poa. Wameshaweka ni wabaya tu wengi wanavyofikiria. Mimi niko poa tu sina shida. Inategemea sasa na mtoto mwenyewe atakavyonichukulia
 
Unataka amtupe? Je angekuwa wako ungetaka amuweke wapi? Ni suala la busara na kutokuwa mbinafsi na mjinga kumkataa mtoto wa mwenzio.
Hamna sehemu nimesema nimekataa mtoto wala kusema amtupe. Soma vizuri jamani.
 
Maneno yamekua meeeng...inshort ni hiv..maisha yako wont be the same no more...hvyo yan.....man rule the world remember
Sijaelewa vizuri mkuu. Sasa hapo man rule the world na nini inakujaje tena wakati mambo ni maelewano. Manake ni suala la mahusiano hapa na sio siasa or anything
 
Walikuwa wanapima tabia yako wamejiridhisha hawana shaka nayo thus walichelewa.Mpokee mwa moyo mweupe show love usimbague hakuna ajuae kesho yake nani atakulea
 
Mtendee wema kesho yako uijui hata watoto wako wanaweza kuja lelewa na mama wa kambo ya kesho atuyyajui kama ambavyo Sabaya na bashite awakutegemea kuwa raia wa kawaida leo.
 
Mtoto hakuletwa mapema kutokana na reaction yako siku umeambiwa mmeo ana mtoto. Mmeo alifanya hivyo kuinisuru ndoa yenu.
Sasa amejua una uwezo wa kuishi nae ndiyo maana anamleta.
Wewe cha kufanya acha kujipa umama wa kambo ule wa kiibilisi bali jipe umama. Hujui ya baadae kwani hata watoto wako wanaweza kuja lelewa na mama wa kambo.
Hivyo mtendee huyo mtoto vile ambavyo ungependa mama wa kambo wa wanao aje watendea watoto wako.[emoji120]
 
Kama unaishi na mtu na humpendi si itakuwa unafiki jamani! mimi sijawahi mchukia coz hamna mtu ana apply azaliwe. Nimeshea tu kupata ushari na iwapo kuna maandalizi yoyote ambayo natakiwa niwe nayo haswa ya kisaikolojia basi nisaidiwe kuyajua. Lakini suala sijui la chakula, mavazi, malazi, elimu hakuna shida. Anapata na ataendelea kupata
Sasa upendo haulazimishwi, hiyo inategemeana na roho yako ilivyoumbwa. Huwezi chagua umpende nani na nani usimpende. Ila kumpa mtu haki yake hilo ni suala la uchaguzi na usipochagua kutoa haki ni kinyume cha maadili na sheria.
 
Back
Top Bottom