Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Wangshu:

Hii dunia hakuna ulichokuja nacho na wala hakuna utakachoondoka nacho tambua sisi sote ni wageni hapa.


Changamoto yetu kubwa hapa duniani ni UPENDO haijalishi una Imani kubwa kiasi gani yakuhamisha mito milima na mabonde kama una Imani ni bure.


Cha kwanza unapaswa kujua dhumuni la wewe kuwa hapa duniani ni nini au ni huyo mtoto wa kambo? Kuna watu walipishana pasipokujua alikuja ndani ya nyumba zao. Pengine huyo ndiyo baraka za nyumba yako au ni mkombozi wa watoto wako siku za usoni.

Let 💚 , Lead !!
 
Hii ndio perception ya watu kwa baadhi ya step mothers. Roho mbaya hiyo vipi! roho mbaya labda unayo wewe na mawazo yako negative towards wengine. Mimi nimeshaandika toka mwanzo roho mbaya sina. Na ningekuwa nayo wala asingesema anamleta mtoto.
Samahan mama wa kambo mtarajiwa lakn wachangiaji wote hatuwez kuwa na mtazamo mmoja "nilikua nachomekea tu " in magufuli voice
 
Mwisho wa siku kulea mtoto asie wako ni shughuli, ni kazi huo ndio ukweli tena ukweli usiotakiwa make ukiusema lazima uambiwe una roho mbaya....

Unaambiwa mlee kama mwanao sawa, mwanao akikosea utamkanya, kama ni kuchapa utamchapa, huyo wa mme mguse uone!!! Unamchapa kwa sababu sio wako....okay ukiamua uache tu napo utaambiwa haumrekebishi kwakua sio wako.

Mke wa bro hampendi kabisa mtoto wa bro, nami namuelewa na nasisitiza bro asilazimishe mke amlee huyo mwanae

Mwenyekiti; natamani unisimulie kidogo hapo kwa bro na mkewe na mtoto; kascenario kao kidogo tu.
 
Hongera kwa kukubali si jambo rahisi kulea mtoto mkubwa.

Nimeishi na watoto wa kuletwa ( si wa baba)
- wanahisi wewe si mhusika wa maisha yao. Wanachopewa mara nyingi huhisi wangestahili zaidi.

- Wewe si wa muhimu sana kwao. Kwenye kuwaadabisha wanachagua kukusikiliza au kutokusikiliza.

- Fadhila kwako hata baada ya kujitolea ni option, si wajibu.

-Do not force to be loved or respected.
- Mjalie huduma stahiki, usijikombe ukajuta baadaye.

- Jifunze tabia zake ujue namna ya kumuadabisha. Ukimuacha tu atakugharimu.

- Usiondoe family standard zako kumfanya yeye tu awe comfortable.

Mengine with time, mambo yanaenda.
Thank you a million times. Kweli umenielewa concern yangu na umenipa ushauri mzuri. Nondo kama hizi ni muhimu. Kuna wachangiaji wengine wamekazana ooh una roho mbaya blah blah mi siko huko.
 
Nawasalimu wote.

Kama mada inavyojieleza.

Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.

Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.

Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.

Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.

Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.

Natanguliza shukrani!
Huyo ni mali ya mumeo kua mpole,mtoto akija kuishi na ndgu zake ni jambo zuri
 
Mwisho wa siku kulea mtoto asie wako ni shughuli, ni kazi huo ndio ukweli tena ukweli usiotakiwa make ukiusema lazima uambiwe una roho mbaya....

Unaambiwa mlee kama mwanao sawa, mwanao akikosea utamkanya, kama ni kuchapa utamchapa, huyo wa mme mguse uone!!! Unamchapa kwa sababu sio wako....okay ukiamua uache tu napo utaambiwa haumrekebishi kwakua sio wako.

Mke wa bro hampendi kabisa mtoto wa bro, nami namuelewa na nasisitiza bro asilazimishe mke amlee huyo mwanae
Nashukuru! umenielewa na mimi nimekuelewa sana tu.
 
Imagine kupiga simu kila wakati kuulizia mtoto anaendeleaje, mara mpe simu mwanangu niongee naye, mara utume pesa unakuwa kama unahudumia familia mbili, kwa watu ambao mlishawahi kukutanisha vikojoleo mkipigiana simu mara moja mbili au ukienda kumtembelea mtoto kwa mamake, ni mara chache sana utakosa kukumbushia kama binadamu mwenye madhaifu.

Kukata mzizi wa fitna ni kuweka mazingira ya kutokuwa na sababu ya kuwasiliana. hata hivyo , kama yeye anaona hiyo ni issue mwache, kuna siku atakuta mtoto wa pili kwa mchepuko. na hilo litakuwa fundisho kwake, manake kama yeye ana watoto na yule ana watoto hapo kipimo kitakuwa nani bora kwasababu kote kuna watoto wa kutosha. nitaawaacha wapambane mbabe niendelee naye.ndivyo akili za wanaume zilivyo.

Unasema nisubiri agundue tunapasha kiporo...simwogopi hata nusu, na wala siwezi kukataa akiuliza, yeye mwenyewe nafikiri kama mtu mzima anajua kinachoendelea kama watu mnawasiliana mara kwa mara namna ya kulea mtoto wenu, kuna mengi mnaweza kujadili na kujadili na kukumbushana story n.k
Kunywa bia bucket mbili kwa bili yng,mke ambae hapendi mwanao ndio dawa yke kuendeleza game kwa mzazi mwenzio...mimi na case kma yko namvutia kasi nimpe mtoto wa 2
 
Yaani mtu ulipewa taarifa kabla hata hujaolewa afu et leo unakuwa na wasiwasi miaka yote hiyo kama siyo roho mbaya ni nini,kwani mtoto anapunguza nini kwenye familia?
Sijasema anapunguza kitu. Nilitaka kujifunza mambo tofauti tofauti hapa juu ya hilo jambo langu. Roho mbaya labda unayo wewe. Mimi sina hiyo
 
Wangshu:

Hii dunia hakuna ulichokuja nacho na wala hakuna utakachoondoka nacho tambua sisi sote ni wageni hapa.


Changamoto yetu kubwa hapa duniani ni UPENDO haijalishi una Imani kubwa kiasi gani yakuhamisha mito milima na mabonde kama una Imani ni bure.


Cha kwanza unapaswa kujua dhumuni la wewe kuwa hapa duniani ni nini au ni huyo mtoto wa kambo? Kuna watu walipishana pasipokujua alikuja ndani ya nyumba zao. Pengine huyo ndiyo baraka za nyumba yako au ni mkombozi wa watoto wako siku za usoni.

Let 💚 , Lead !!
Nimekupata! asante
 
Huhitaji kujiandaa kisaikoloji,ni kumpokea na kumkubali kama mtoto wako.Changamoto ni kama mama yake wa kumzaa yupo,sina hakika kama utaweza kumlea vizuri.Ukimkaripia au kumuonya ni rahisi kumkumbuka mama yake na kutamani kurudi.
 
Na uzuri alipewa taatifa kabla ya ndoa sa nashangaa anachoogopa ni nini?
Mimi siogopi wajameni. Taarifa nilipewa ndio na hata taarifa yenyewe mimi nilihoji kama ana watoto au mtoto? Sio yeye alianza kusema. Huenda nisingeuliza labda nisingeambiwa ! i dont know. Basi akasema yupo but sijawahi mfuatilia. Mimi hapa nikasema kama yupo basi kamtafute umlete maana staki uje uniletee mtoto mkubwa sijui amelelewaje, amepata elimu gani etc. Kama atakuwa part ya maisha yako kamtafute. Akatafutwa lakini sasa hakuletwa nyumbani. So nashangaa wanaosema roho mbaya blah blah. Am not that kind of a person. Kwa sababu zake anazojua mwenyewe hakumleta wakati huo na kwa sababu zake anamleta wakati huu. Mimi niko peace tu.Maisha yanaendelea. Nachofanya ni maandalizi ambayo yanaambatana na kujifunza basi.
 
Mwenyekiti; natamani unisimulie kidogo hapo kwa bro na mkewe na mtoto; kascenario kao kidogo tu.
Bro ni single father 😂
Sasa kaja kuoa, ila huyu mtoto na mama wa kambo haziivi, mtoto kishalishwa sumu na mamake huko hamuheshimu kabisa step mom sometimes huwa anasema"baba angu ana wake wawili, huyu na mama angu"

Wifi angu huwa anasema kabisa mi simpendi huyu mtoto, wala familia hatumuoni ana roho mbaya wote tunamuelewa
 
Sijasema anapunguza kitu. Nilitaka kujifunza mambo tofauti tofauti hapa juu ya hilo jambo langu. Roho mbaya labda unayo wewe. Mimi sina hiyo
Basi kama ni hivo huna cha kuhofia yaani kiufupi aishi kama wenzie na ukiwatreat sawa wote hamna atayekupangia malezi reward na punishment ziwe kwa wote
 
He/ She is just a little child. Achana na suala la bond. Litakuja tu.

Love wins over everything, even the hardest of hearts.

Let the child be a child,know that he is a different human being with different upbringing but also know that his addition into your family can make yours a happier one. The more the merrier they say.

Acceptance is key, take him in as you would have another woman take in your kids and slowly mould him into a responsible, moral and upright young man.

About discipline, be fair and just.

Let God lead and all the best.
 
Back
Top Bottom