- Thread starter
- #141
Makubwa!Ngoja nitafute mtoto wa nje nione vile inakua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Makubwa!Ngoja nitafute mtoto wa nje nione vile inakua
HahahahKumbe umeolewa na singo faza.
Asante sana. Nimekuelewa na ushauri wako nimepokea na nitaufanyia kazi. Nahitaji nondo kama hizi. Barikiwa sanaMleta mada, kwanza nikupongeze kwa kuaminiwa na mumeo kulea mtoto ambae sio wa kumzaa. Naweza kushauri mawili matatu kutokana na uzoefu - nami pia ninaishi na mtoto wa kambo na alimleta nyumbani mwaka mmoja baada ya kuwa tumefunga ndoa, akiwa na miaka 6.
1. Mchukulie sawa na watoto wako wengine, pasiwe na tofauti namna unavyoishi nao. Mfano, asome shule moja na wenzake au kama ni tofauti basi ziwe na hadhi inayofanana. Hata unapomtambulisha kwa ndugu/jamaa/marafiki/majirani mtambulishe kama ni mwanao. Epuka kabisa kumtambulisha kama "mtoto wa mume". Hii itasaidia kujenga bond kati yako na mtoto na pia kati yake na ndugu zake.
2. Anapokosea jambo usiwe mwepesi wa kumwadhibu, mshirikishe kwanza baba yake, usije ukaonekana kama unamwonea.
3. Mfundishe/mwelekeze utaratibu wa maisha yenu hapo nyumbani (do's and donts), kila inapobidi bila kuwa mkali. Mfano, wa kwangu alipokuja alikuwa na tabia za kupiga wenzake nikawa namwelekeza mara kwa mara kuwa humu ndani hairuhusiwi kupigana, akikuchokoza mwenzako shitaki kwa mama au baba. Au kabla ya kulala ni lazima kusali kwa pamoja n.k n.k
4. Uwe na mawasiliano na mama yake mzazi. Sababu as long as mtoto hayupo kwa mama, ni lazima atakuwa na uhitaji wa kujua maendeleo ya mtoto wake-kiafya, kimasomo n.k. Usimpe sababu baba mtu kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mama wa mtoto. Wewe ndio uwe kiunganishi.
5. Muhimu zaidi, omba sana Mungu mtoto huyo awe ni chambo ya maelewano mazuri kati yako na mumeo.
All the best!
Wengine hadi leo vinaendelea ila wakikwama hao wamekuja....Wengine tulifanyiwa vitimbi na mama zetu wa kambo vya kila aina lakn Leo hii ndio tunawalea na wanatutegemea kwa kila kitu
Hakuna anaye ijua kesho yake
PoleWengine hadi leo vinaendelea ila wakikwama hao wamekuja....
Sitarajii penye utu na upendo na kutamalaki kwa Mungu iwe katika nafsi, familia, ndoa na etc pawepo na uthubutu wa fikra kama hizi. Mfanye Mungu aishi ndani yako. Upupu haumjui mjomba wala etc...Nawasalimu wote.
Kama mada inavyojieleza.
Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.
Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.
Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.
Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.
Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.
Natanguliza shukrani!
OkSitarajii penye utu na upendo na kutamalaki kwa Mungu iwe katika nafsi, familia, ndoa na etc pawepo na uthubutu wa fikra kama hizi. Mfanye Mungu aishi ndani yako. Upupu haumjui mjomba wala
Asante kwa ushauriMpende kama mwanao lakini usiwe na expectations zozote kwamba kuna kiasi cha upendo na wewe unahitaji kutoka kwake. Kama na yeye ataamua kukupenda kama mama yake au la hilo ni juu yake.
Yaani mtu ulipewa taarifa kabla hata hujaolewa afu et leo unakuwa na wasiwasi miaka yote hiyo kama siyo roho mbaya ni nini,kwani mtoto anapunguza nini kwenye familia?Kikubwa uishi na mtoto wa mwenzio kama wako
Na uzuri alipewa taatifa kabla ya ndoa sa nashangaa anachoogopa ni nini?Huo Ni mtego amekuletea
Na ni kipimo sahii kabisa cha Ubora wa uanamke Wako (wife material) ktk familia na Ndoa yako kiujumla.
Ukijichanganya hapo,
Iyo Ndoa inaota mbawa
Mama ake si yupo? Kwani lazima amlee yeye?Na uzuri alipewa taatifa kabla ya ndoa sa nashangaa anachoogopa ni nini?
Mpaka ameamua kumleta basi sina budi kuhoji alipo,Mama ake si yupo? Kwani lazima amlee yeye?
Of course ni changamoto na uzuri umefafanua vyema ila cha msingi ni kumlea kama wengine very simpleHongera kwa kukubali si jambo rahisi kulea mtoto mkubwa.
Nimeishi na watoto wa kuletwa ( si wa baba)
- wanahisi wewe si mhusika wa maisha yao. Wanachopewa mara nyingi huhisi wangestahili zaidi.
- Wewe si wa muhimu sana kwao. Kwenye kuwaadabisha wanachagua kukusikiliza au kutokusikiliza.
- Fadhila kwako hata baada ya kujitolea ni option, si wajibu.
-Do not force to be loved or respected.
- Mjalie huduma stahiki, usijikombe ukajuta baadaye.
- Jifunze tabia zake ujue namna ya kumuadabisha. Ukimuacha tu atakugharimu.
- Usiondoe family standard zako kumfanya yeye tu awe comfortable.
Mengine with time, mambo yanaenda.
@wangshu jifunze kitu hapa.Wengine tulifanyiwa vitimbi na mama zetu wa kambo vya kila aina lakn Leo hii ndio tunawalea na wanatutegemea kwa kila kitu
Hakuna anaye ijua kesho yake