Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Ohoo! ni wa kike! kwahiyo ndio kusema hatanipenda! hahahhaa. Ukweli mume wangu ananipenda na anijali. Mtoto nampokea kwa roho nyeupe tu haina shida. Nilitaka kujifunza zaidi ili itakapofika muda niwe nimeshajifunza kama yapo ya kujifunza na ya kufanyia kazi
Nafkr keeping an open mind
Asilazimishwe kukuita mama
Anaweza ita mamkubwa au mamdogo tu
 
nina mtoto wa kambo, wife hataki nimlete. hiyo imeniletea shida sana kwasababu inabidi mara nyingi niwe nawasiliana na mama wa mtoto huyo na kujikuta tumesharudisha majeshi hadi kuogopa kupata mtoto mwingine wa pili. ila angekubali kuishi nami hiyo chain angeshaikata. wanawake kuweni na akili, kuna vitu vingine sio lazima uende shule cha pili, nakushauri usije kumtesa, utafungwa, pia usimbague kwasababu hata ufanyeje watoto wako wanajua hiyo ni damu yao wakiwa wazima utajikuta umelaumiwa, pia watoto wote wa kambo wanaoishi kwa kuteswa na mama wa kambo huwa wanafanikiwa kimaisha kuliko watoto wa ndani ya ndoa. amini usiamini.

Wanawake hawajui tu hio karata angeicheza vizuri mkeo ni Bonge la point
Mimi mwanangu wa kwanza nilimkuta lakini ndio tunabond vizuri sana na niliweka juhudi hapo maana ndio roho ya mume ilipo...inampa amani sana baba yake,anapata kila kitu anachotaka zaidi,nampenda tu bure sio kwasababu baba yake yupo hata asipo kuwepo atapata same treatment
 
Yaani mtu ulipewa taarifa kabla hata hujaolewa afu et leo unakuwa na wasiwasi miaka yote hiyo kama siyo roho mbaya ni nini,kwani mtoto anapunguza nini kwenye familia?
Roho mbaya tuuuu
 
Uchoyo plus ubinafsi wa mali atazo gawiwa huyo kijana ndio zinazo kutesa kuna ka asset unaona wanao watapunjika akiongezeka huyo. Ila kumbuka huyo anafuata matunzo tu atimize ndoto zake ,About tommorow ajuae ni mungu.Hakuna cha bond wala james bond.
 
Bond, upendo utajengeka tu automatically kutegemea na ninyi wenyewe. Ila cha msingi ni mpokee na mtreat kama ambavyo unawatret watoto wako. Kila mzazi ana parenting style, so mlee kama unavyowalea watoto wako wengine. Kwa kuwa alikuwa analelewa na mama yake, inawezekana yakawa ni malezi ya aina tofauti na ya kwako; so kama kuna vya kubadilisha vibadilishe taratibu na kwa upendo na yeye anaweza akaadapt taratibu kadri anavyokaa na wadogo zake: kuna mengine hutoweza kuyabadili na as long as hayana tatizo basi unayaacha tu. Isijeonekana kana kwamba unajifamya wewe malezi yako ndiyo perfect kuliko ya mama yake; mkaanza mtimbwili.

Yes kuanza kumlea mtoto ambaye tayari ana ufahamu wake sio rahisi sana tofauti na ukianza kumlea mtoto tangu akiwa mdogo. Kuna watoto ni wema tu naturally, labda na mama yake ndiyo wale wenye hekima kashamwambia aje aishi na wewe vizuri so mtajikuta tu taratibu mambo yanakaa sawa.

Au anaweza akaja ashaambiwa kuwa mama wa kambo ni watesaji, au kashajazwa sumu kuwa huyu ndiyo kasababisha baba yako na mama yako wasiwe pamoja, so anakuja ameshajipanga. Don't fight with the kid, prove him/her wrong kwa moyo wako mweupe kwake. Ifike hatua mtoto mwenyewe aanze kujiuliza mbona niliyokuwa naambiwa sio nayoyaona. Akizidi kukuletea majaribu, mkabidhi baba yake.

Kama umeolewa kwenye familia yenye mawifi wanaojirambua basi kheri. Ila kama ndiyo umeolewa kwenye hizi familia zenye mawifi wasiostaarabika, jiandae kisaikolojia kuziba masikio na kujifanya bubu. Maana mawifi wanawatumiaga sana watoto wa kambo kujiingiza kwenye ndoa za kaka zao na kuleta mitafaruku, unless ukute mtoto ana akili akagoma kutumika au baba ni mkali akawanyamazisha dada zake. But all in all, mtreat vizuri huyo mtoto, akija kukushukuru baadaye sawa, asipokushukuru sawa pia; ila as long as ulimtendea mema wakati unatimiza wajibu wako, basi utakuwa na amani. Hata watoto wetu wa kuwazaa wengine hawana shukrani pia

Tatu usiwe defensive na epuka maneno yoyote ya kumkumbusha huyo mtoto kuwa si mtoto wako. Akikosea muadhibu kama mtoto aliyekosea sio ndiyo unaanza "aah umetumwa na mama ako eeh, ntakukomesha", sijui umenishinda tabia nenda tu kwa mama ako; mtoto wako akikushinda unampelekea nani? Kama ambavyo watoto wako wa kuwazaa wanaweza kuwa na tabia za ajabu, hata mtoto wa kambo anaweza kuwa na tabia za ajabu vilevile; so deal naye kama ambavyo ungedeal na mwanao wa kumzaa

Usiache kujiombea na kumuombea kama unavyowaombea watoto wako, akiwa mtoto mwema ni faida kwenu wote, na akiwa jaribu basi amini ni mzigo wenu nyote pia. Panda mbegu njema kwa huyo mtoto, regardlessly. Ombea amani ya nyumba yako na watoto wako wote.

Hayo mambo ya baba yake kusema sijui atapima DNA sijui hawajafanana, muachie baba mtoto. As long as kamleta nyumbani kwenu na kukwambia huyo ni mtoto wake, basi mpokee na kumlea vizuri.
Ameeeen, mama mlezi. Hujawahu kushindwa ktk mambo haya.
 
Imagine kupiga simu kila wakati kuulizia mtoto anaendeleaje, mara mpe simu mwanangu niongee naye, mara utume pesa unakuwa kama unahudumia familia mbili, kwa watu ambao mlishawahi kukutanisha vikojoleo mkipigiana simu mara moja mbili au ukienda kumtembelea mtoto kwa mamake, ni mara chache sana utakosa kukumbushia kama binadamu mwenye madhaifu.

Kukata mzizi wa fitna ni kuweka mazingira ya kutokuwa na sababu ya kuwasiliana. hata hivyo , kama yeye anaona hiyo ni issue mwache, kuna siku atakuta mtoto wa pili kwa mchepuko. na hilo litakuwa fundisho kwake, manake kama yeye ana watoto na yule ana watoto hapo kipimo kitakuwa nani bora kwasababu kote kuna watoto wa kutosha. nitaawaacha wapambane mbabe niendelee naye.ndivyo akili za wanaume zilivyo.

Unasema nisubiri agundue tunapasha kiporo...simwogopi hata nusu, na wala siwezi kukataa akiuliza, yeye mwenyewe nafikiri kama mtu mzima anajua kinachoendelea kama watu mnawasiliana mara kwa mara namna ya kulea mtoto wenu, kuna mengi mnaweza kujadili na kujadili na kukumbushana story n.k
Bond kati ya mzazi.na mtoto huwa haiondoki kirahisi. Mama atataka kumchukua mwanae likizo. Haya mambo ni magumu na yanahitaji sana hekima na busara katika kutafanyia maamuzi
 
Nawasalimu wote.

Kama mada inavyojieleza.

Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.

Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.

Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.

Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.

Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.

Natanguliza shukrani!
@yangshu we ni mchina kwa ubatizo?
Hili jina sio la kibantu.
Anyways. ..jipange kuchonganishwa na mumeo kama mtoto ni mkubwa kidogo (anaweza kuchongea kwa baba). Ukimkemea hata kama kosa analo...vumilia yajayo
 
@yangshu we ni mchina kwa ubatizo?
Hili jina sio la kibantu.
Anyways. ..jipange kuchonganishwa na mumeo kama mtoto ni mkubwa kidogo (anaweza kuchongea kwa baba). Ukimkemea hata kama kosa analo...vumilia yajayo
Mimi sio Mchina ni jina tu. Kuhusu kuchonganishwa possibly inaweza ikatokea. Maana hata huko aliko anachongea. Naonaga anavyompigia simu na kumueleza mambo. Kama huko anafanya hivyo akija anaweza fanya the same au asifanye..i dont know! Ndiyo hivyooo najiandaa kuvumilia yajayo.
 
Uchoyo plus ubinafsi wa mali atazo gawiwa huyo kijana ndio zinazo kutesa kuna ka asset unaona wanao watapunjika akiongezeka huyo. Ila kumbuka huyo anafuata matunzo tu atimize ndoto zake ,About tommorow ajuae ni mungu.Hakuna cha bond wala james bond.
Nyie ndio wale mnafeligi mtihani. Soma uelewe ndugu sio kuanza ku attack. Mali kitu gani wewe. Mimi sina shida ya mali ninazo za kutosha aisee.
 
Km ni wa kiume mfanye kibenteni ndani kwa ndani..... Bond itakua imetiki kirahisi kabisaa
 
Back
Top Bottom