Soon Simba SC wataaminishwa Mo kamkataa Niyonzima

Soon Simba SC wataaminishwa Mo kamkataa Niyonzima

Vipi kuhusu Ngoma ? Offer yenu ya 180ml imeishia wapi? Mmedanganywa mkadanganyika subiri uone Aisha Manula na Niyonzima kama utawaona msimbazi
Manula alitoa sharti waondoke Dida na Bartez atue Jangwani ...Loading.....
 
Niyonzima ni mchezaji wa Yanga fc.
Mbona wana Simba sc, hatuna habari kuwa atasaini Simba sc.
Yanga fc. Mnamambo ya ajabu hasa,
Ninani kawaambia eti Mo atamkataa Niyonzima.
Alimkubali lini?
Au mnasoma kwenye magazeti yenu.
Yaani mchezaji wenu mnaisingizia Simba sc bila hata kusaini mkataba
na timu.
Kwataarifa yenu Niyonzima hayupo kwenye mipango ya kocha wa Simba sc.
Na wala hatumuhitaji labda mchezaji mwenyewe kama ataomba kujiunga na Simba sc, tunaweza kumfikiria kwasababu bado anaonekana ni mzuri uwanjani.
Niyonzima ni mchezaji wenu acheni kuweweseka.
Ungekuwa sahihi kama Uongozi wenu ungekanusha rasmi huo unaouita uzushi wa magazeti yetu kuhusu Niyonzima na Ngoma.
 
Ungekuwa sahihi kama Uongozi wenu ungekanusha rasmi huo unaouita uzushi wa magazeti yetu kuhusu Niyonzima na Ngoma.
Ingia kwenye Simba app kama utaona neno Official ; Ngoma na Niyonzima wajiunga na Simba Sc, Tatizo ni mitandao tu. Issue yeyote inayoenda kiofficial official Basi lazma utaona neno official. Mambo mengine ni mbwembwe tu.
 
Hivi ndivyo watakavyojifariji Kama walivyojifariji kwa yaliyotokea kwa Ndombo Ngoma Jana.. ...stay tuned
Bila kusahau hata ninyi mlikua mkisema Ngoma haende tu mchezaji msumbufu. Niyonzima ndo nani. Mara yanga kapata mbadala was Niyonzima. Leo mnawataka ama kweli SIZITAKI MBICHI HIZI.[emoji12]
Ingia kwenye Simba app kama utaona neno Official ; Ngoma na Niyonzima wajiunga na Simba Sc, Tatizo ni mitandao tu. Issue yeyote inayoenda kiofficial official Basi lazma utaona neno official. Mambo mengine ni mbwembwe tu.
 
Ungekuwa sahihi kama Uongozi wenu ungekanusha rasmi huo unaouita uzushi wa magazeti yetu kuhusu Niyonzima na Ngoma.
Kukaa kimya siyo kithibitisho cha kukubali uzushi.
Kiongozi anamajukumu yake muhimu ya kuyatekeleza kila siku.
Sio lazima kukanusha au kukubali, minon'gono yoote inayonong'onwa mitaani.
 
Bila kusahau hata ninyi mlikua mkisema Ngoma haende tu mchezaji msumbufu. Niyonzima ndo nani. Mara yanga kapata mbadala was Niyonzima. Leo mnawataka ama kweli SIZITAKI MBICHI HIZI.[emoji12]
Mpenzi wa Yanga alipochoma jezi ya Niyonzima Uongozi wa Yanga ukalaani, maana yake ni kutokubaliana na kitendo hicho baada ya nyinyi na magazeti yote kusema kwamba Yanga imechoma jezi ya Niyonzima. Ndio ishara ya uongozi unaojitambua. Kama kweli Uongozi unaojitambua wa Simba haukuhusika na kauli za wawili hao kusajiliwa nao ila ulikaa kimya kwa sababu haukuona haja ya kukanusha, nini tafsiri ya viongozi wenu wa usajili kuongezea kauli kwamba Yanga vocha imekata na ndio adha ya kumtegemea mtu mmoja? Nini tafsiri ya yinyi kudai jukwaani humu kwamba Niyo hawezi kuweka picha ya kusainishwa Simba mpaka mkataba wake na Yanga kumalizika? Nini tafsiri ya Dalali kusema Ngoma na Niyonzima ni wachezaji anaowakubali tangu zamani na amefurahi kuwa wamesajili Simba? Basi Uongozi unaojitambua wa Simba usingejaribu angalau kumnon'goneza mzee wa watu huyo kwamba hali haiko hivyo? Si kwa sababu Uongozi wenyewe ndiyo chanzo cha habari hizo? Na kama hamkuwa kweli na imani ya dhati kwamba wawili hao wanakuja kwenu, kwa nini mnatoa povu hivi sasa kwamba eti Yanga ni vigeugeu? Kwani kusema kwamba wameshindwana na Niyonzima maana yake kwamba Niyonzima hangeruhusiwa tena kusajiliwa hata kama atarejesha majeshi nyuma? Kwani kusema Ngoma ni msumbufu ndiyo kusema hatakubaliwa tena klabuni hapo? Kwani hamjapata kusema Okwi ni msumbufu? Mbona Yanga hawajatoa povu kulaani mlipomsajili tena kama mnalotoa nyinyi dhidi ya kusajiliwa Ngoma?
 
Kukaa kimya siyo kithibitisho cha kukubali uzushi.
Kiongozi anamajukumu yake muhimu ya kuyatekeleza kila siku.
Sio lazima kukanusha au kukubali, minon'gono yoote inayonong'onwa mitaani.
Waambie basi viongozi wako kwamba miongoni mwa majukumu muhimu ya viongozi ni kuhakikisha kwamba wanaowaongoza wanapata habari sahihi na kwa wakati. Kwa hivyo ni juu ya viongozi kuhakikisha kwamba wawache kuamini habari potofu zinazoonekana kuwa sahihi (fake news). Kukaa kimya dhidi ya habari kama hizo ni sawa na kuzikubali. Waambie kwambaWalatini walisema Qui tacet consentire videtur au kwa Kiingereza chepesi ni he who is silent seems to consent.
 
Hujanielewa mkuu,
nimesema sio kazi ya kiongozi wa Clabu ya Simba kujibu MINONG'ONO YOTE.
Angalia maana ya neno
YOTE.
Kuna baadhi ya habari Uongozi unawajibika kujibu lakini sio KILA HABARI.

Kama unafahamu kiswahili vema nadhani umenielewa.
 
Nisielewe Kiswahili kwa sababu tu ya nukuu ya Kilatini? Nimekuelewa fika. Kwamba si juu ya Kiongozi kujibu kila habari inayovuma. Wewe ndiye hujanielewa. Kwamba hii ya Niyo na Ngoma kujiunga na Simba kama mkakati wa timu kujiimarisha na kufanya vyema kwenye mashindano ya kimataifa kutokana na fedha ya Mo Dewji si kama hizo habari nyengine. Ni miongoni mwa hizo habari muhimu zinazohitaji ufafanuzi - au ukanushi - ili kutowachanganya wachezaji waliopo na wapenzi/washabiki wasichanganyikiwe kisaikolojia pale tamaa yao itapokuja kutamauka, kama ilivyotamauka kwa swala la Ngoma. Kama unafahamu Kiswahili vyema nadhani umenielewa.
 
Wanachama na wapenzi wa timu ya Simba Sports Club.
Wakitaka habari za usahihi huwa wanazipata toka katika uongozi wa Simba sc.
Au
Kutoka kwenye vyanzo vya habari vya timu.
Uongozi wa Simba sc, haujawahi kutoa habari za kuwasajiri wachezaji unaowaongelea.
Wala kocha hajawahi kuwahitaji.
Wala vyombo vya habari vinavyotambuliwa na wanasimba kama Simba Blog, Msemaji wa timu nk. havijawahi
kuzungumzia usajiri wa hao wachezaji unaowasema.
Sasa
wewe ndugu unachukua habari unakokujua halafu unawa lazimisha viongozi wa Simba sc wazijibu. Ni jambo la kustaajabia.
Ivi wewe hizo habari umezipata wapi ? Na nani alizipeleka huko.
Mnaandika habari huko mnakokujua bila kushirikisha viongozi wa Simba, halafu mnawalazimisha wazijibu.
Ivi mliwashirikisha kuziandika ?
Kwanini msizijibu wenyewe mliozitunga ?
Naomba hizo habari uzijibu wewe maana naona unazijua kwa undani,
Sisi huku Msimbazi hatuzijui hizo habari na wala hatujasema popote kuhusu huo usajiri.
Unaelewa kiswahili au mwenzetu ni
Mlatino.
 
Mkuu naona tunarejeshana huo kwa humo kama santuri yenye pengo! Nimesema kwa Kiswahili ambacho wengi wamekielewa kuwa si kila habari ni za kunyamaziwa na uongozi. Hii ya kuwatia tamaa wafuasi na kuwachanganya wachezaji waliopo inahitaji kukanushwa iwapo siyo ya kweli. Unaniuliza ninakozitoa habari hizo. Si sahihi kudhani kwamba ni vyombo rasmi ulivyovitaja tu ndani ya Simba ndiyo vinavyotoa habari sahihi za Simba. Vyombo vyengine vinaweza kutoa habari sahihi, ingawa zinaweza zisiwe rasmi. Katika mazingira hayo, ni juu ya Simba yenyewe kuvikanusha moja kwa moja au kukanusha habari teule zitazoonekana kuikwaza kama hizi za usajili. Kwani, mathalan, gazeti la Ngurumo za Simba linachapishwa Jangwani? Utamshawishije Mwanasimba na tusio wana-Simba kwamba taarifa za gazeti hilo si za Simba?Kwani Mkuu ni nani Dalali zaidi baina yako na Hassan Dalali? Mbona unamkanushia habari ambazo yeye mwenyewe hajazikanusha? Ni nani Hans Poppe zaidi baina yako na Zacharia Hans Poppe? Mbona unamkanushia kwamba hajasema Yanga salio limekata ilhali mwemyewe hajakanusha? Ni nani Simba zaidi baina yako na Manara, Aveva na Kaburu (Mungu awape malazi salama huko waliko)? Mbona unawakanushia kauli ambazo wao wenyewe hawajazikanusha? Kwenye habari kama hizo, za magazeti kama hayo, ndani ya kipindi kama hichi, na mazingira kama haya, ukimya wa uongozi dhidi ya habari hizo ni sawa na kuziwafiki. Ningekuwa Mwanasimba, ningekubali kistaarabu kwamba uongozi umerejea kutudanganya. Nisingejidhalilisha kwa kuwatetea hadharani huku nikiugulia machungu ya kusutwa na nafsi yangu ilhali wao wanatucheka kimoyomoyo kwa jinsi walivyotugeuza 'hewalla bwana'. Huko ni kujiafutia maradhi ya moyo kwa makusudi ilhali wao wanatononoka kila uchao.
 
Vipi kuhusu Ngoma ? Offer yenu ya 180ml imeishia wapi? Mmedanganywa mkadanganyika subiri uone Aisha Manula na Niyonzima kama utawaona msimbazi
Sijui waliotaka kumsajili Ngoma na huyo Niyonzima ila Manula sawa na uhakika atatua simba,.Kaa na uchapati wako utaona
 
Sijui waliotaka kumsajili Ngoma na huyo Niyonzima ila Manula sawa na uhakika atatua simba,.Kaa na uchapati wako utaona
Usije ukaja kuyakataa maneno yako mwenyewe! Wenzio nguvu kubwa imehamia segerea kuwapelekea chakula Aveva na mwenzio habri ya usajili wameweka pose
 
Back
Top Bottom