Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Dikteta uchwara katika ubora wake hataki kupingwa! Lakini wakati huo huo bado kawakumbatia wahuni, majangili, wezi, wapokea na watoa rushwa, wafitini na mafisadi ndani ya chama. Kama ilivyomshinda nchi chama pia kimemshinda kukiendesha huyu mkurupukaji.
Spot on chief...halafu mtu aitwaye MTAZAMO ati anaona CCM inajitengeneza!!
 
Mkuu huyu jamaa ni mtu wa visasi na ana roho mbaya sana pia hajui kusamehe! Kaja kulipa kisasi baada ya karibu miaka miwili! Ogopa sana watu wenye visasi kama huyu malaika Mkuu.
Tabia za kitusi hizi.
 
Coz upinzani nao kama hujatoka Kaskazini, utakuwa unatwanga maji...... Mbowe kwenye uenyekiti humwambii kitu kabisa ukionekana unaanza harakati za kugombea zengwe linaundwa...... Upinzani bado siyo bongo Africa nzima.
 
..safi kabisa...acha wafu wazikane....hizi fitna zao watakaofaidi ni wapinzani... Ndani ya muda mfupi ccm wameondokewa na wema, mama yake na sasa Sofia...wote hawa wana wafuasi nyuma yao...ccm ni jahazi linalozama....serikali yake dhalimu wamekosa hoja...bajeti inawashinda...wanachoweza ni kufukuzana...kama namna ya kutafta kiki kwa wananchi....hatudanganyikiiiii...

Kile chama cha kuzoa mizoga wabebe huo mzoga wanaitwa kunguru au fisi
mnaanza kuitana mizoga?ama kweli.....kuwa mzoga ndani ya ccm ni kuwa na mawazo mbadala na pia kutokuwa na vyeti vya wengine!
 
Tukisema wote mlioko huko kijani ni FAFAFA ni akina Bashite mnaona mnaonewa.haya kama mnalazimisha mpaka watu kumpenda mtu.
Kuanzia vyetyi vya form four feki hadi phd feki alafu tunategemea nchi ya viwanda wkt hawajui hata principle moja ya uchumi.....Wanachukia matajiri
 
Mama Salma kuchukua nafasi yake soon,CCM wana fitna sana.

Nchi inaongozwa kimabavu na chama pia.

Kwani ni kosa mwanachama kupinga maamuzi ya ndani ya chama?

Unyama unyamani.
Nifah kipenzi tulia chama kitoe wanafiki ndo waliokuwa wanaleta makundi chamani hao
 
Mbona Waziri mkuu MKM alikuwa miongoni mwa watu waliosimama ukumbini na kuimba wimbo wa "Tuna imani na Lowassa"na hajafutiwa uanachama?

Ndiyo maana Taifa linakumbwa na misukosuko kila siku,kumbe hata sisi tusiomchagua tunaweza kuundiwa zengwe na kupoteza utanzania wetu,hii hatari sana.





Mods tafadhari pandisheni hiyo video ili jf iwasaidie hao viongozi kutendeana haki,wawafukeze wote walioonesha mapenzi/imani kwa mh.Lowassa.

Siyo hilo tu. Huyu Majaliwa alikuwa mmoja wa wale walioitwa mawaziri mizigo na kina Kinana na Nape!
 
CCM ipi inayojitengeneza? Wewe toka Slaa kaweka mpira kwapani, akili zako zimekuwa clotted...umekuwa lightweight sana chief...

Kumfukuza Sophia ndiyo kujitengeneza? Ipi misingi yao ya kujitengeneza? Yaani kutotaka upinzani ndani ya chama ndiyo kujitengeneza? Chama kuwa na wanachama wa ndiyo mzee ndiko unakokuzungumzia?

Kujitengeneza gani huko ilhali bado CCM imekumbatia mafisadi? Tena mafisadi wao wengine ndiyo wenyeviti wa Bunge la Jamhuri, huku wengine wakiwa ndiyo wenyeviti wa chama! Kujitengeneza gani wakati bado inaogopa kufukua makaburi? Bado inakutumbatia mikataba iliyoitwa ni ya kisanii? Bado inakumbatia watu walituuzia ARV feki?

Yaani CCM ni wepesi mno. Washukuru tu watanzania ni watu wafu, wasiojielewa kama wanadamu. Kama wangekuwa wanajielewa, no matter how weak the opposition is, CCM haipaswi kushinda hata uongozi kwenye kijiji. Kwani CCM wamesha-prove failure. Hawana jipya! No matter what games they play, CCM kitabaki kuwa chama cha kisanii tu. AND THIS IS PROVEN.
.....
.....Poti huyoo jamaa hajitambuwi
 
Tukisema wote mlioko huko kijani ni FAFAFA ni akina Bashite mnaona mnaonewa.haya kama mnalazimisha mpaka watu kumpenda mtu.
Tumemsaidia Sofia Simba awe huru kumfuata Lowasa huko aliko, maana alisema hadharani na kila mtu alisikia

Kwanini abaki ccm wakati moyo wake upo kwa mamvi?

Huu ubireshaji wa chama sio habari nzuri kwa chadomo/chawema
 
Mgonjwa anapokaribia hupata nafuu au huanza kupaparika Na CCM muda wao wa kuondoka umefika hii tunasema wanapaparika.

Mabadiliko yoyote katika CCM hayana tija kwa mwananchi wa chini. 2015 walitumia gia ya kuwa udhaifu wa Kikwete ktk kufanya maamuzi magumu Ndio Sababu ya matatizo Yao.

Sasa maamuzi magumu ya Magufuli yamemsaidia nini mwananchi mpaka sasa? Jibu no

CCM Na viongozi wake +wanachama+wafuasi ni watu wasiojua maendeleo ktk ulimwengu wa sasa hayaletwi Na maamuzi magumu tu peke yake. Yanahitaji kiongozi mwenye VISION Na ktk CCM Hakuna Na Wala hatokuwepo. Na Kama maamuzi magumu ya Magufuli Ndio maendeleo basi KOREA KASKAZINI ingekuwa taifa tajiri duniani.

Kuwatia uoga watu anavyofanya Magufuli hakutoleta maendeleo Bali kutadumaza akili za watu.
 
Back
Top Bottom