Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

O
Mabadiliko ndani ya CCM ni lazima yatokee khasa baada ya miaka 40 tangu kuundwa kwake.

Nafasi katika halmashauri kuu zimepunguzwa kutoka 388 hadi 158, wakati nafasi katika kamati kuu zimepunguzwa kutoka 34 hadi 24.

Mabadiliko kama haya au kwa kiingereza "reforms " ni muhimu khasa ukiwa na kiongozi anaejali kupunguza matumizi hata katika chama chake.

Pia mabadiliko kama haya kutakiwezesha chama cha CCM kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kuondokana na wanachama wasohitajika lakini wanaolipwa fedha za mishahara bure.

Ila kumvua uanachama Sophia Simba ni uamuzi sahihi na balozi Nchimbi kukaa nje akiwa balozi ni adhabu tosha.

Kwa umri alokuwa nao mama Sophia Simba alipaswa kuchunga kauli zake na ile kauli yake aloitoa kwenye harakati za kuchuja wagombea uraisi mwaka 2015 ya kwamba, yeye ni mjumbe wa kamati kuu na hatakubali kuona mgombea mwenye sifa kama Edward Lowasa akikatwa jina kwasababu za kijinga na kwamba wote wanaomchafua Edward Lowasa ni wajinga na wapumbavu.

Hii ni sawa na mtu kutapika kabisa halafu baadae anakuja kula matapishi yake mwenyewe.
Amfuate huko huko, CCM ni ya Wanachama si mtu kama ilivyo kwa baadhi ya Vyama.
 
Yaani kumuunga mkono mgombea mwingine ni kosa la kufutiwa uanachama? Kwenye uchaguzi lazima kuwe na makundi ya wagombea, siyo usaliti huo
 



Ok, nimewapata maana nakumbuka safari ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana Iringa mwaka 2013 huyo mama alitajwa kama Joyce.

Ni hayahaya ya waandishi wetu kuandika habari zisizo sahihi, kama ni hivyo.
 
CCM inakua chama cha mwenyekiti, sizonje anajipanga vyema 2020 apite bila kupingwa
 
Hapo hamna haki kabisa.. Hahahahaha..
Kosa la Mama simba na hao waliopewa onyo linatofauti gani??
Mwisho wa siku mtajuana wenyewe..
Mtukufu mwenyekiti amejiskia vibaya kumtimua mteule wake bwana Nchimbi.
 
Walipoambiwa toroka uje hawakuelewa sasa wanasomeswa namba.
 
Back
Top Bottom