Huyo wa Iringa anaitwa Joyce Msavatavangu na siyo Jesca Msambatavangu.
Mkuu
Richard ngoja ngoja nikudadavulie kwa ufupi sana kuhusu huyo mama.
1.Kwanza anaitwa Jesca Msambatavangu. Alikuwa diwani wa ccm kata ya miyomboni mkoani Iringa. Ila huyo Joyce uliyemtaja labda ni wa huko "call me jey" na sio huyu wa miyomboni.
2. Pili anakaaa Iringa mjini pale mitaaa ya uhindini (Karibu na duka maarufu la miyomboni pharmacy mujini Iringa). Vijana wa kitanzini wanajua vema, mshindo , makorongoni mpaka pale ofisi yake ilipo mitaa ya saba saba. Opposite na makaz ya salim asas wa asas milk.
3. Amesoma elimu ya kiutu uzima Q.T pale Iringa , akasoma shahada /degree ya kwanza chuo kikuu cha Tumaini -Iringa. Pia masters yake kachukua pale pale , nitafatilia zaid kwenye vyanzo vyangu kama alifanikiwa Kuhitimu PhD pale Tumaini maana kuna kipindi alikuwa anachukua shahada ya uzamivu (PhD). Kumbuka darasani yuko njema sana (smart minded & academic talented, she is a real an avid learner). Ana element za kina john kisomo linapokuja sala la elimu , na lugha ya malkia inapanda sana.
4. Aliwahi kuingia mgogoro na mama Monica mbega (former MP -Iringa constituency) ,pia mkuu mwakalebela atakuwa naye anamkumbuka kwa namna alivyomletea zengwe kwenye kupitishwa kugombea ubunge , Mzee asas wa Asas dailies anajua vema.
5.Aliwahi kufundisha kule kitwiru kwenye kibamda mbuzi na kuuza vitumbua na maandazi (akimsaidia mama yake) mpaka pale alipokutwa na mzungu akiwafundisha watoto wa hali ya chini lugha ya malkia licha ya yeye kuishia la7 tu tena kwenye kibanda cha nyasi (mbavunza mbwa) ,ndipo alipopata wafadhiri wa kumjengea shule niliyoitaja pale juu.
6. Ni mama mjasiriamali mzuri sana na mpambanaji wa uhakika. Muulize jah pipo wa makambako (sanga deo), lukuvi,pindi chana wa karibu na NMC Iringa, Mzee Abeid kiponza , Kija wake ally (mlugulu wa Moro aliwahi kuuza soko kuu Iringa, alikuwa mlinzi wake -ana black belt aliopata toka kwa sensei Yahhya pale shule ya mwingi gamhilonga alikuwa na dojo.lake pamoja na kitanzini na kituo cha mgongo watoto yatima,
Pia alikuwa akipewa nafasi flani flani nyeti ya umoja wa vijana mkoa mmoja kusini huko) , ukitaka kumjua vema Kijana ally msaidiz wa Jesca msambatavangu muulize jamaa ammoja white hivi anaitwa ibrahimu ngwada (babu yake aliwahi kuwa kiongozi Mkubwa wa dini).
Ukizengua ntashusha utirio zaid kuhusu huyu mama msambatavangu...wewe dhani kila mtu humu JF ni mwenzio kumbuka falsafa ya mwl kila walipo 3basi kuna....wangu.
7.Ni mmiliki wa shule ya kimataifa maarufu sana Iringa ijulikanayo kama star international ipo ipogolo maeneo ya kitwiru..na kwa kweli kwa ile shule ni nzuri kitaaluma na ni bora kwa wale wazee wa shule za hi...madam, gd morning dad, etc. Hii itawafaa.
NB: siyo kila unayemuona hapa ukadhani ni mtu wa sport sport kutoka ufipa ,
Ukibisha zaidi ntamwaga uturio wake mpaka namna alivyozenguana na Mme wake bwana mmoja wa songea.
Au tukudadavulie na madabida na mgeja pia. ????
Usije omba pooooo lakini.