Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Huyo wa Iringa anaitwa Joyce Msavatavangu na siyo Jesca Msambatavangu.
Mkuu Richard ngoja ngoja nikudadavulie kwa ufupi sana kuhusu huyo mama.

1.Kwanza anaitwa Jesca Msambatavangu. Alikuwa diwani wa ccm kata ya miyomboni mkoani Iringa. Ila huyo Joyce uliyemtaja labda ni wa huko "call me jey" na sio huyu wa miyomboni.

2. Pili anakaaa Iringa mjini pale mitaaa ya uhindini (Karibu na duka maarufu la miyomboni pharmacy mujini Iringa). Vijana wa kitanzini wanajua vema, mshindo , makorongoni mpaka pale ofisi yake ilipo mitaa ya saba saba. Opposite na makaz ya salim asas wa asas milk.

3. Amesoma elimu ya kiutu uzima Q.T pale Iringa , akasoma shahada /degree ya kwanza chuo kikuu cha Tumaini -Iringa. Pia masters yake kachukua pale pale , nitafatilia zaid kwenye vyanzo vyangu kama alifanikiwa Kuhitimu PhD pale Tumaini maana kuna kipindi alikuwa anachukua shahada ya uzamivu (PhD). Kumbuka darasani yuko njema sana (smart minded & academic talented, she is a real an avid learner). Ana element za kina john kisomo linapokuja sala la elimu , na lugha ya malkia inapanda sana.

4. Aliwahi kuingia mgogoro na mama Monica mbega (former MP -Iringa constituency) ,pia mkuu mwakalebela atakuwa naye anamkumbuka kwa namna alivyomletea zengwe kwenye kupitishwa kugombea ubunge , Mzee asas wa Asas dailies anajua vema.

5.Aliwahi kufundisha kule kitwiru kwenye kibamda mbuzi na kuuza vitumbua na maandazi (akimsaidia mama yake) mpaka pale alipokutwa na mzungu akiwafundisha watoto wa hali ya chini lugha ya malkia licha ya yeye kuishia la7 tu tena kwenye kibanda cha nyasi (mbavunza mbwa) ,ndipo alipopata wafadhiri wa kumjengea shule niliyoitaja pale juu.

6. Ni mama mjasiriamali mzuri sana na mpambanaji wa uhakika. Muulize jah pipo wa makambako (sanga deo), lukuvi,pindi chana wa karibu na NMC Iringa, Mzee Abeid kiponza , Kija wake ally (mlugulu wa Moro aliwahi kuuza soko kuu Iringa, alikuwa mlinzi wake -ana black belt aliopata toka kwa sensei Yahhya pale shule ya mwingi gamhilonga alikuwa na dojo.lake pamoja na kitanzini na kituo cha mgongo watoto yatima,

Pia alikuwa akipewa nafasi flani flani nyeti ya umoja wa vijana mkoa mmoja kusini huko) , ukitaka kumjua vema Kijana ally msaidiz wa Jesca msambatavangu muulize jamaa ammoja white hivi anaitwa ibrahimu ngwada (babu yake aliwahi kuwa kiongozi Mkubwa wa dini).

Ukizengua ntashusha utirio zaid kuhusu huyu mama msambatavangu...wewe dhani kila mtu humu JF ni mwenzio kumbuka falsafa ya mwl kila walipo 3basi kuna....wangu.



7.Ni mmiliki wa shule ya kimataifa maarufu sana Iringa ijulikanayo kama star international ipo ipogolo maeneo ya kitwiru..na kwa kweli kwa ile shule ni nzuri kitaaluma na ni bora kwa wale wazee wa shule za hi...madam, gd morning dad, etc. Hii itawafaa.

NB: siyo kila unayemuona hapa ukadhani ni mtu wa sport sport kutoka ufipa ,

Ukibisha zaidi ntamwaga uturio wake mpaka namna alivyozenguana na Mme wake bwana mmoja wa songea.

Au tukudadavulie na madabida na mgeja pia. ????
Usije omba pooooo lakini.
 
Hiyo barabara waliotoa fedha ni AfDB chini ya uongozi wa JK... Tofauti iliyopo kati ya kanda pendwa na kanda isiyopendwa ni teuzi tu. Wa kanda pendwa hata awe na makandokando ya aina gani kama ilivyo kwa Daudi haguswi ila atoke wa kanda isiyopendwa aambiwe ameiba kijiko tu uone atakavyofurumushwa...

Amefukuzwa mmoja pale Umeme kwa sababu za kijiweni tu na kawekwa mpya kutoka kanda pendwa. Maskini sasahivi tuna ka mgao cha kimya kimya na tunakaa kimya tu..
Kitwanga alikuwa ni wa kanda pendwa lakini mbona alifurumushwa...?! Sema kwenye teuzi wa kanda pendwa ni wengi hata hapa Arusha nawaona, Wa kanda isiyo pendwa wengi walimtosa sana ila kuna wale waliokuwa nae mbona wanakula mema ya nchi, nadhani hata ungekuwa ni wewe ungeweka watu wako mliosimama pamoja...

Huku mlimgaragaza mno, ila na wewe mpo nae pamoja utakula mema ya nchi kama kina Mwanri na Lyatonga...
 
Hatuogopi kufukuzwa , nifukuzeni hata Mimi, poa tuu.

IPO siku tutawavua uanachama hata watu walimakaburini, kupoza machungu waliotufanyia.
 
Tatizo kubwa ni kumsapoti mtu kwa kutaja jina. Hilo huwa kosa kubwa katika siasa hasa ikitokea uliyemsapoti akashindwa.
Kinachomwokoa msukuma kwenye kundi hili ni kitendo chake cha kugeuka mara moja pale uenguaji ulipofanyika. Sentensi yake ya "mimi mpya, mkoa mpya, na mgombea mpya" na ile ya "anajinyea". Imemwokoa.
Ni vema viongozi wakawa makini kutolalia upande wowote wakati wa michakato ya uchaguzi. Kwao chama kiwe kwanza.
Mbona Majaliwa anaonekana hadi kwenye video akimuunga mkono Lowasa ila ameachwa?
 
ccm tumekua kama mazuzu, ndio mzee, na hapa ndio sisonje anapo furahia. atapunguza kamati ya uteuzi hadi watu 2 , yeye na mkewe
 
Umeona kale ka kikilipu ka video hapo juu? Mfukuzeni na Majaliwa, kwani alikuwa na imani na Lowasa! Vipi, yeye siyo msaliti?
Kwani Majaliwa ndiyo kaibeba CCM? Angekutwa na hatia angefukuzwa pia, uwaziri mkuu angeteuliwa mtu mwingine.

Siyo wote waliosimama na kuimba "tunaimani na Lowassa" wamefukuzwa uanachama. Kuna sababu za msingi zilizofanya tuwafukuze tuliowafukuza.

Ikitokea Majaliwa anakiuka maadili ya chama, basi hata yeye hatakuwa na kinga ya kufukuzwa. Lakini, kwa sasa hivi, Majaliwa hana hatia yoyote ile.
 
Kitwanga alikuwa ni wa kanda pendwa lakini mbona alifurumushwa...?! Sema kwenye teuzi wa kanda pendwa ni wengi hata hapa Arusha nawaona, Wa kanda isiyo pendwa wengi walimtosa sana ila kuna wale waliokuwa nae mbona wanakula mema ya nchi, nadhani hata ungekuwa ni wewe ungeweka watu wako mliosimama pamoja...

Huku mlimgaragaza mno, ila na wewe mpo nae pamoja utakula mema ya nchi kama kina Mwanri na Lyatonga...
Mwanri si yeye bali Majaliwa ndiye aliforce awepo tu. Mwanri na Majaliwa wote walikuwa manaibu ofisi ya Waziri Mkuu na walikuwa marafiki wazuri tu..

OK, endeleeni kula mema ya nchi.. 2025 pia alete zengwe ahakikishe mrithi anatoka hukohuko kanda pendwa..
 
Bro madabida ni janga, huyu alitumia cheo chake kuuza ARV feki mnasifia hapa! hawa watu wengine kama mnawapenda mwende mkanywe nao chai.
Kamanda...kuna kosa lilifanyika, lkn tusifanye kosa kumbebesha mtu mzigo usio wake...yeye si mkemia...ni mfanyibiashara...kanuni ya mfumo wa kutengeneza ARV, imekosewa, na zimeingizwa kwenye matumizi...wataalamu, wameshtukia, wametoa taarifa, zimeondolewa kwenye matumizi....!
Ni kosa...kuna wanaostahiki wajibishwa...lkn yeye kwa nafasi yake....hata kama, tunataka kujiliwaza kwa kumuhukumu mtu, basi tusimuhukumu mtu kwa mihemko....tutafakari....
 
Back
Top Bottom