Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Hahahaaa kumekucha! Daudi je hajajadiliwa? Sophia kapumzike siasa sasa basi! Ulisumbua kidogo nawe ulipokuwa karibu na Mkuu wa utawala uleeeee!
Alooo!! Acha tu, babu cheka alitupenda sana bila kujali unamkubali or not
 
Mchakato wa CCM kumpata mgombea wa urais ulivurugwa na mwenyekiti na baadhi ya vigogo wa chama kwa hiyo kama kuna wanachama hawakuridhika chama kilitakiwa kufuta makovu ya uchaguzi badala ya kuwafukuza wanachama waliokataa garasa walizo wekewa!
 
Mama Salma kuchukua nafasi yake soon,CCM wana fitna sana.

Nchi inaongozwa kimabavu na chama pia.

Kwani ni kosa mwanachama kupinga maamuzi ya ndani ya chama?

Unyama unyamani.
Ahhhh kumbe mpango huu ndio hivi! Sofia alikuwa karibu sana na familia ya Msoga dah kazi kweli kweli.
 
Natabiri kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais atakayekiwakilisha chama watafukuzwa wengi.
 
Chadomo walivyo mazuzu, wanasikitika Sofia kufukuzwa uanachama kwa usaliti! Mbona Zitto mlimfukuza kwa kosa lile lile la usaliti! Mbona hamkumtetea!!!?
 
Back
Top Bottom