[emoji23] [emoji23] [emoji23]Wamfukuze na Mwenyekiti wao.. Mbona naye anawasaliti?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Wamfukuze na Mwenyekiti wao.. Mbona naye anawasaliti?
Tokea juzi nimejikaza sana kukuuliza maana mabadiliko niyaonayo kwako sio bure [emoji23] [emoji23] [emoji23]Hahahahahahaha we acha tu... Ila bado twasoma upepo labda huko mbele mambo yatakuwa shwari.
kututoa gizani pia ni afya, japo tunaamini yote yanayofanyika yanasukumwa na nia njema ya mabadiliko.Sio kila jambo linaanikwa mpk uamuzi huo umefikiwa jpm hajakosea amechambua taarifa za vyombo vingi vinavyomzunguka katika mamlaka yake
Huna lolote...kwendraaSikujibu kwakuwa inaonesha bado mchanga ktk haya mambo
Kuwa na mawazo tofauti sio kosa ila kukihujumu chama ni kosa.wangefukuzwa wote au wengine walitubu?
Pia kwa utawala bora, wanachama wajulishwe sababu za kina za makosa yao ili isionekana kuwa na mawazo tofauti na wengi ndani ya chama ni makosa
Hili ni mbinu ya kutisha watu ili waogope kutopitisha mabadiliko wanayoyataka.
Bashite hatumuachiiiiiii,hata upite mwaka mzima ila akirudi nchini arudi na vyeti.Naona wameamua kututoa ktk Mada ya Vyeti vya Bashite.
Kweli ww kada alafu elimu yako itakuwa na mashaka.Mabadiliko ndani ya CCM ni lazima yatokee khasa baada ya miaka 40 tangu kuundwa kwake.
Nafasi katika halmashauri kuu zimepunguzwa kutoka 388 hadi 158, wakati nafasi katika kamati kuu zimepunguzwa kutoka 34 hadi 24.
Mabadiliko kama haya au kwa kiingereza "reforms " ni muhimu khasa ukiwa na kiongozi anaejali kupunguza matumizi hata katika chama chake.
Pia mabadiliko kama haya kutakiwezesha chama cha CCM kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kuondokana na wanachama wasohitajika lakini wanaolipwa fedha za mishahara bure.
Ila kumvua uanachama Sophia Simba ni uamuzi sahihi na balozi Nchimbi kukaa nje akiwa balozi ni adhabu tosha.
Kwa umri alokuwa nao mama Sophia Simba alipaswa kuchunga kauli zake na ile kauli yake aloitoa kwenye harakati za kuchuja wagombea uraisi mwaka 2015 ya kwamba, yeye ni mjumbe wa kamati kuu na hatakubali kuona mgombea mwenye sifa kama Edward Lowasa akikatwa jina kwasababu za kijinga na kwamba wote wanaomchafua Edward Lowasa ni wajinga na wapumbavu.
Hii ni sawa na mtu kutapika kabisa halafu baadae anakuja kula matapishi yake mwenyewe.