Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Ebu pima hizi kauli zako, alafu ujue unafiki wako umeuficha wapi?
1. Huna ushabiki na vyama.
2. Utaelekea kujiunga CCM.
3. Iwapo CDM (sijui kwanini hujaifikiria ATC au CUF)itamchukua hata mmoja wao.
4. Utaichukia rasmi (sijui ni lini ulianza kuwa na mapenzi na CDM)

Hivi chadema ndio imependekeza muwafukuze?
1.YES sina ushabiki na chama chochote
2.YES nitaelekea wakijirekebisha matendo yao
3.CDM inaongoza wapokea wahamiaji wote Wakubwa (bisha!)
4.Niliipenda CDM ya Dr.Slaa kipindi cha M4C hadi zilipotokea gia za angani.
Kila chama kina wanafiki na wafata upepo, ulipo kama sio mnafiki unafata upepo!..
 
MKUU SIYO KWAMBA HAPENDI KUKOSOLEWA UNA KOSOA UNA KOSOA KWA LIPI EM KOSOA BASI TUONE.
Serikali Yake imekuwa Ya kufanya Vitu Kwa tension Ya Mkuu Wa Nchi.Viongozi wake wengi ni wanafiki/Waoga.
Kila msaidizi Katika Serikali Yake Anafanya Vitu Kwa kuongopa Kuanzia Waziri Mpaka mtendaji wa Mtaa.Uoni Hilo ni tatizo?
 
Wakati Bashite bado anajiita mkuu wa mkoa na ziro yake anatumbuliwa aliyepingana na maamuzi ya chama ambacho hakituhusu wananchi tulio wengi.

Inashangaza sana.
Sasa kama hayakuhusu unayafuatilia ya nini
 
Lowasa huko aliko analia kwa uchungu
Mtandao uko kwenye mioyo ya watu Kwa hiyo kumtosa Sophia ifahamike alikuwa na back up ; Yeye akitumika tu kumfunga paka kengele. Wako wapi walioimba tuna imani na Lowassa!? Mbona walikuwa wengi? Wawatoe wote Kama wana ubavu? Akina Membe et al. Walichofanya ni kupulizia tu air refresher lakini mzoga bado is there to stay na solution ni kuutoa na kuuzika na siyo kupulizia air refresher. I mean hardcore wasaliti bado wako ndani ya chama
 
Ccm ina haki kumwondoa au kumkubali mwanachama kupitia vikao n.k. lakini tuzingatie sana watanzania wote bila upinzani changamoto itakufa. Hata ktk biashara unahitaji upinzani ili uboreke uwe na nidhamu pia. Kwa nchi yetu kwa sasa upinzani upo dhaifu sana unachangiwa na mambo mengi. Illa ni muhimu na ni jambo zuri kwa Ccm kwa na Taifa kwa ujumla wake kuwepo na upinzani wenye nguvu ili Taifa lisonge mbele kwakutambua ufisadi ubadhirifu n.k. na pia ujue kipimo cha utawala wako. Lakini kwa upinzani huu sio jambo zuri kabisa kwa mustakbali wa nchi hii kisiasa na kiuchumi. Bado tu wachanga ktk demokrasia tunahitaji kupiga hatua. Hata kama Ccm inatawala uwepo upinzani wenye nguvu kiuchumi na katika sifa za viongozi wao pia sio kwa hali hii ya sasa ya upinzani wapo dhaifu. Ni maoni yangu tu.
wapinzani marufuku kufanya siasa, wakifurukuta tu ndani wanawekwa btena bila dhamana, wapinzani wote wanao criticise serekali wana kesi za kutosha.
 
Kwani Majaliwa ndiyo kaibeba CCM? Angekutwa na hatia angefukuzwa pia, uwaziri mkuu angeteuliwa mtu mwingine.

Siyo wote waliosimama na kuimba "tunaimani na Lowassa" wamefukuzwa uanachama. Kuna sababu za msingi zilizofanya tuwafukuze tuliowafukuza.

Ikitokea Majaliwa anakiuka maadili ya chama, basi hata yeye hatakuwa na kinga ya kufukuzwa. Lakini, kwa sasa hivi, Majaliwa hana hatia yoyote ile.
Kwa hiyo kosa la Sophia lina tofauti gani na ya Nchimbi na Kimbisa?!? Mind you, Nchimbi amepewa ubalozi na Mwenyekiti wa chama, kilichompa onyo la usaliti!!
 
Hivi waloimba tunaimani na Lowasa ndo wanatimuliwa????

Kuna mmoja kasahauliwa
 
Kosa kubwa la Sofia sio kuimba.. ' tunaimani na lowasa' bali alivujisha siri nyingi za chama kipindi cha uchaguzi . Na ndio maana JPM kipindi kile alisema kuna wenzetu mchana wapo ccm usiku wasaliti.
 
Nimependa hiyo sehemu kuwa "waliofukuzwa hawaruhusiwi kukata rufaa"
Udikteta uchwara kazini
 
Kosa kubwa la Sofia sio kuimba.. ' tunaimani na lowasa' bali alivujisha siri nyingi za chama kipindi cha uchaguzi . Na ndio maana JPM kipindi kile alisema kuna wenzetu mchana wapo ccm usiku wasaliti.
Watu wanafikiri haya maamuzi yamefanywa pasipo kuwa na sababu.

Nakumbuka hiyo kauli ya uncle Magu wakati wa kampeni
 
Mkuu issue ya Katiba mpya si issue ya Chama ....Chadema hawawezi kushinikiza na kushinda issue ya Katiba mpya bila kupata support kutoka CCM... ....
Kwa akili zako timamu unafikiri CCM wanaweza kukubali katiba ya wananchi? Katiba ambayo itaondoa status quo? Tena chini huyu sadist dikteta uchwara?

Tatizo la Tanzania, wala siyo vyama vya upinzani. Tatizo kubwa ni sisi wenyewe wananchi. Haswa watu wasiojielewa; watu wenye kupigania maslahi ya watu, na siyo ya nchi. Hawa watu ndiyo wanaifanya CCM iendelee kuibaka Tanzania mchana kweupe.

Vyama vya upinzani vimeshafanya kazi yake kwa mafanikio makubwa sana, ukizingatia hali isivyo fair kwa CCM kuwa chama dola.

Tatizo pia lipo kwa watu kama wewe, ambao wanaamini watu fulani tu ndiyo wanastahili kuwa viongozi. Watu kama nyiye ndiyo wenye kupigania maslahi ya watu, mkiamini katika kushikwa mkono kwenye nchi ya maziwa na asali. Nyiye ndiyo sababu ya CCM kuendelea kuibaka Tanzania mchana kweupe.

Mpaka pale watu wa hayo makundi mawili watakapoisha ndipo nchi hii itasonga mbele. Kinyume na hapo, tutapiga mark time mpaka magaga yaishe.
 
Back
Top Bottom