Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Mkuu issue ya Katiba mpya si issue ya Chama ....Chadema hawawezi kushinikiza na kushinda issue ya Katiba mpya bila kupata support kutoka CCM..... Ajenda ya katiba mpya ilibebwa na akina Warioba (wana CCM) na pia ilipingwa na watu ambao ndio wengine waliokuja kukimbilia Chadema na kupewa fursa ya kugombea Urais ....hivyo kwa Chadema ya sasa hiyo si ajenda tena (kama ilivyo ufisadi) ....Chadema inaishi kwa matukio na kwasasa haieleweki inasimamia nini (labda Bashite saga) ....na huwezi kusikia nyie manguli wa kuikosoa CCM mkitoa ushauri wa kisera huko Chadema hata wafanye makosa gani ....au chadema hawakosei? Au Chadema si muhimu kwavile hawana dola? ....

Siku zote huwa nayaheshimu maandiko.....maana ni ya mtu anayetumia vyema kilichomo kichwani mwake......

Bravo.....
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.
Profesa, uliyoyasema ni sawa, ila tatizo la Watanzania wengi ukiwemo wewe mnasubiri kufanyiwa. Hamtaki kushiriki mambo ya kijamii. Lakini mnarefusha midomo kwa Yale yanayofanywa na wenzenu bila kujua changamoto zinazowakabili. Huu ni unafiki Mkubwa Sana. Hivi ktk mazingira Haya tutafanikiwa kuunda baiskeli? Hakika tutaendelea kuwa mizigo kwa dunia.
1d6bb09df98228f1e8166e9fcc51ab57.jpg

Nimeiona kwny JF twitter:

=========
UPDATES:

Waliofukuzwa Uanachama wa CCM kuanzia leo:
1. Sophia Simba
2. Ramadhan Madabida
3. Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa
4. Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na
5. Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga

View attachment 479745
View attachment 479746
View attachment 479747
View attachment 479748
View attachment 479749

=====
KWA UFUPI:

Machi 11, 2017 - Dodoma

Habari kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba, baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.

Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.

Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavangu, Mjumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.

Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido, Leizer amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Mollel, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Awadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.

Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Cheif Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali.

View attachment 479785
View attachment 479786
View attachment 479783
View attachment 479784
 
Dhambi ya usaliti ni kutosha tu. Heri kuwa na wanachama waaminifu 10, kuliko wanachama wasaliti 100.
 
Frankly speaking,kama walikiuka miongozo na taratibu za chama chao ni haki yao kabisa kuadhibiwa,na si chama cha kwanza kufanya maamuzi kama haya,Chadema ilifanya hivyo kwa akina ZITTO,K.MKUMBO,MWIGAMBA,M.MWAMPAMBA,J.SHONZA,na wengine wengi,baada ya kufukuzwa Mtela Mwampamba,Juliana Shonza na wengineo,walikimbilia CCM,(IKUMBUKWE WALIFUKUZWA,HAWAKUHAMA).Siku wanajiunga na CCM baada ya kutimuliwa CHADEMA,walipokelewa na mwenyekiti wa CCM wakati huo,Mh.Rais mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete.na sasa wanatumikia nafasi mbali mbali ndani ya serikali yetu.

Maana yake ni kwamba,kufukuzwa uanachama haimfanyi mtu kuwa USELESS,anaweza kuendelea na siasa ila mahala pengine,au anaweza kuamua kujipumzisha tu,hayo ni maamuzi binafsi.

Tusiwahukumu watakapoamua kujiunga na vyama vingine,wanaweza kuhamia huko na wakawa wanachama waaminifu kama walivyo wakina Mtela Mwampamba na Juliana Shonza,wanafanya kazi zao vizuri kabisa na kwa weledi uliotukuka,(nazungumza kwa dhati kabisa,pasipo kuwa na ushabiki wowote).

Tuwatakie maisha mema na maamuzi yao yasiwe ya hasira,watulie na wafanye maamuzi sahihi kwao.
 
1d6bb09df98228f1e8166e9fcc51ab57.jpg

Nimeiona kwny JF twitter:

=========
UPDATES:

Waliofukuzwa Uanachama wa CCM kuanzia leo:
1. Sophia Simba
2. Ramadhan Madabida
3. Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa
4. Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na
5. Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga

View attachment 479745
View attachment 479746
View attachment 479747
View attachment 479748
View attachment 479749

=====
KWA UFUPI:

Machi 11, 2017 - Dodoma

Habari kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba, baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.

Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.

Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavangu, Mjumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.

Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido, Leizer amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Mollel, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Awadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.

Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Cheif Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali.

View attachment 479785
View attachment 479786
View attachment 479783
View attachment 479784
Kuna kitu hapa niliwahi kusema
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma
Paskali
 
Kwani Lowassa, Sumaye, kingunge walirudisha kadi? Mbona hawajathibisha kutowatambua?!
 
CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.

Mie huwa sielewi hizi kauli, wabunge wa chama tawala waliokataliwa majimboni ni sawa kabisa wakipewa madaraka na chama tawala tena hata baada ya kutumbuliwa kwenye hayo madaraka wanaweza kuonekana wanafaa tu kupewa hata ubunge. Ila wakienda Chadema ghafla wanageuka kuwa makombo na makapi.
 
wangepotezwa wote...ila kwani kum support Lowassa si ilikuwa imeshaisha? au walikuwa wana msupport chini kwa chini?
CCM siku zote huwa hawakurupuki kuchukua hatua. Na wakichukua maana yake wamejiridhisha! Hongera CCM kwa maamuzi mazuri. Bado Bashe!
 
Mkuu Richard ngoja ngoja nikudadavulie kwa ufupi sana kuhusu huyo mama.

1.Kwanza anaitwa Jesca Msambatavangu. Alikuwa diwani wa ccm kata ya miyomboni mkoani Iringa.

2. Pili anakaaa Iringa mjini pale mitaaa ya uhindini (Karibu na duka maarufu la miyomboni pharmacy mujini Iringa). Vijana wa kitanzini wanajua vema, mshindo , makorongoni mpaka pale ofisi yakel ilipo mitaa ya saba saba. Opposite na makaz salim asas wa asas milk.

3. Amesoma elimu ya kiutu uzima Q.T pale Iringa , akasoma shahada /degree ya kwanza chuo kikuu cha Tumaini -Iringa. Pia masters yake kachukua pale pale , nitafatilia zaid kwenye vyanzo vyangu kama alifanikiwa Kuhitimu PhD pale Tumaini maana kuna kipindi alikuwa anachukua shahada ya uzamivu (PhD).

4. Aliwahi kuingia mgogoro na mama Monica mbega (former MP -Iringa constituency) ,pia mkuu mwakalebela Utakuwa naye anamkumbuka kwa namna alivyomletea zengwe kwenye kupitishwa kugombea ubunge , Mzee asas wa Asas dailies anajua vema.

5.Aliwahi kufundisha kule kitwiru na kuuza vitumbua na maandazi (akimsaidia mama yake) mpaka pale alipokutwa na mzungu akiwafundisha watoto wa hali ya chini lugha ya malkia licha ya yeye kuishia la7 tu tena kwenye kibanda cha nyasi (mbavunza mbwa) ,ndipo alipopata wafadhiri wa kumjengea shule niliyoitaja pale juu.

6. Ni mama mjasiriamali mzuri sana na mpambanaji wa uhakika. Muulizs jah pipo wa makambako (sanga deo).,pindi chana wa karibunna NMC Iringa, Mzee Abeid kiponza, Kija wako ally (mlugulu wa Moro aliwahi kuuza solo kuu Iringa, alikuwa mlinzi wake -ana black belt aliopata toka kwa sensei Yahhya, alikuwa pewa nafasi flani ya umoja wa vijana kusini huko) , ukitaka kumjua vema Kija ally msaidiz wa Jesca msambatavangu muulize kijan ammoja white hivi anaitwa ibrahimu ngwada (babu yake aliwahi kuwa kiongozi Mkubwa wa dini).

Ukozengua ntashusha utirio zaid kuhusu huyu mama msambatavangu...wewe dhani kila mtu humu JF ni mwensio kumbuka falsafa ya mwl kila walipo 3basi kuna....wangu.

7.Ni mmiliki wa shule ya kimataifa maarufu sana Iringa ijulikanayo kama star international ipo ipogolo maeneo ya kitwiru..na kwa kweli kwa ile shule ni nzuri kitaaluma ni bora kwa wale wazee wa shule za hi...madam, gd morning dad, etc. Hii itawafaa.

NB: siyo kila unayemuona hapa ukadhani ni mtu wa sport sport kutoka ufipa ,
Ukibisha ntamwaga uturio wake mpaka namna alivyozenguana na Mme wake bwana mmoja wa songea.

Au tukudadavulie na madabida na mgeja pia. ????
Usije omba pooooo lakini.
Huyu anatufaa CDM. Karibu mama
 
Madabida sijui hata atakimbilia chama gani.. Hahahaha..

Hao waliofukuzwa hawabebeki!
 
Mie huwa sielewi hizi kauli, wabunge wa chama tawala waliokataliwa majimboni ni sawa kabisa wakipewa madaraka na chama tawala tena hata baada ya kutumbuliwa kwenye hayo madaraka wanaweza kuonekana wanafaa tu kupewa hata ubunge. Ila wakienda Chadema ghafla wanageuka kuwa makombo na makapi.
Sio kipindi hiki wale wenye interest binafsi ndani ya chama hawana raha kabisa na haya mabadiliko
 
Kweli ujinga na maradhi vitaendelea kumtawala na kumsumbua mtanzania yaani kupunguza wajumbe kushiriki katika maamuzi eti ndio mabadiriko na kukifanya chama kua cha wananchi wa chini....kweli wewe ulioturoga watanzania ulikufa zamani
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.
Bora adui wa nje kuliko adui wa ndani. Safi sana JPM
 
Chadomo walivyo mazuzu, wanasikitika Sofia kufukuzwa uanachama kwa usaliti! Mbona Zitto mlimfukuza kwa kosa lile lile la usaliti! Mbona hamkumtetea!!!?
Alitetewa na ccm. Kwani wewe ulimtetea?
 
Back
Top Bottom