South Korea inazalisha chuma kingi kuliko Afrika ya watu bilioni 1.5!!

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Hii ni sababu moja kubwa ya umasikini wa sisi Waafrika. South Korea ina kama watu milioni 52 lakini inazalisha tani milioni 62 za chuma kila mwaka. Afrika ina watu bilioni 1.6 lakini inazalisha tani milioni 22 tu kwa mwaka. Kati ya hizo, tani milioni kumi zinazalishwa na Misri na tani milioni tano na South Africa!

Southh Korea hawana madini chuma ya maana. Wana kama tani milioni 34 tu. Kila mwaka wanaagiza madini chuma tani milioni 65! Wanaagiza hayo madini chuma kutoka Australia, Brazil, South Afrika nk. Wanasafirisha kwa meli hadi kwao na kuzalisha steel.

Afrika nchi ya Zimbabwe pekee ina tani bilioni 30 za madini chuma. Nchi ya Guinea ina tani bilioni 20 za madini chuma ya kiwango cha juu sana. Tanzania tuna kama milioni 200. Uganda 500m na Kenya 200m.

Si South Korea tu. Hata Vietnam wanazalisha chuma kingi kuliko Afrika Yote. Wakizalisha tani milioni 24.

Wakati vita ya pili ya dunia imekolea Ujerumani ilikuwa inazalisha tani milioni 34 za chuma. Miaka zaidi ya 80 baadaye Afrika yote haijafikia kiwango hicho!
Umasikini wa Afrika umetokana hasa na kupuuza nafasi ya chuma kwenye uchumi.

Huwezi lima bila chuma.

Huwezi kuwa na uchumi wa bluu bila trawlers za chuma.


Huwezi kujenga bila chuma





Huwezi kuchimba madini bila chuma.



Huwezi kusafirisha abiria bila chuma. Hizo bajaji 5,000 za Mbeya zingetengenezwa hapa hapa zingeingiza pesa ngapi?


Unapiganaje vita bila chuma? Unakuwaje jeshi bora la sita๐Ÿ˜๐Ÿ˜ Wasouth walijitahidi kuunda zana zao.


Hata watoto kukaa chini ni sababu ya kupuuza umuhimu wa chuma.

Tuache uzembe.
 
Inaniuma saana nikifikiria huaga mi nalia inaniuma sana afrika imepima imekutwa na tani 22
 
Kafulila kabaki kupiga porojo na kuposti JF nakujijibu na id zake tofauti lukuki.

Matrix19
 
Afrika maji tu ilitakiwa iwe Bure,
 
Mwaka 58 wenzetu wanarusha Vanguard 1 sisi bado ata hatujapata uhuru.

Tuna safari ndefu sana,
 
Sijui wamepatwa na nini. Karibu nchi zote 54!!

Masikitiko makubwa mkuu hamna mwenye tofauti hata mmoja! Nilianza kusikia habari ya chuma cha Liganga na Mchuchuma tangu Adam Sapi ni spika hadi leo spika mtoto wa mjini ni stori tupu!

Wanawekeza mabilioni kwnye V8 tangu mjapani kaanza kuzalisha hadi leo, kila toleo wanaamka nalo, wakati wamezaliwa wanakunywa maji na wanyama pori huko kwao hadi walipofika chuo ndio wakaanza kutumia mess tins za aluminium!
 
What else is new about Africa?!
 
 
you have good message lakin kuna kitu hujakiwaza vema african poverty is techinical poverty not normal poverty hujaelewa
 
China yuko mbali sana. Mbaya zaidi kwetu waafrika makampuni ya kichina yanakuja kukaba uzalishaji wote wa chuma huku.
Chuma cha Guinea wameshika na kuanza uzalishaji. Huko Zimbabwe wameshaanza uzalishaji toka 2024, wanazalisha tani laki sita kwa mwaka.
Hapa Tanzania wataanza karibuni kuzalisha.
Je haya makampuni ya kichina yatazalisha chuma cha kuweza kuzifanya nchi za Afrika ziweze kuwa na viwanda vya kushindana na China sokoni? Au wameshaona mbali kuwa potential kwa sasa ipo Afrika hivyo wamekuja kutublock huku huku?
Uzalishaji Zimbabwe.
 
Ongezea kwamba, Korea Kusini ni mshirika wa Marekani. Tunaambiwa kwamba, ukishirikiana na mabeberu unaanguka kiuchumi. Swali, imekuwaje Korea Kusini kufanikiwa kiuchumi licha ya kushirikiana na beberu Marekani kwa miaka mingi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ