SPECIAL FEEDBACK: JF members niliowasajilia Business Names na Company Limited 2013-2014

SPECIAL FEEDBACK: JF members niliowasajilia Business Names na Company Limited 2013-2014

Singo

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
1,204
Reaction score
1,143
Ninayo furaha kuwafahamisha kwamba nimeweza fanya kazi na member kadhaa wa Jamiiforums na ambao sio jf members( ila ni kwa kupitia jukwaa hili walinifahamu),waishio mikoa tofauti tofauti na mmoja nje ya Tanzania(Canada) zinazohusu usajili wa Business Name na Company Limited .

Walifahamu kuhusu mimi na ujuzi wa maswala ya usajili baada ya kujibu thread za member kadhaa humu waliouliza maswala ya usajili , rejea thread : Msaada juu ya kusajili jina la biashara(rejea post na 6 na kuendelea) na Jinsi ya Kusajili Kampuni Tanzania (rejea post no 128 page ya 7)

Wafuatao niliwasajilia Business names

Ally Msangi (Mwanza)

CHASHA POULTRY FARM (Arusha)

Mc Hestone Jr (Arusha)

Qsm ( Arusha)

PACMA ADVENTURE AND SAFARI(Arusha )

ALF(DAR ES SALAAM) kazi ni FALON ENTERPRISES

Elie Chansa (Arusha) kazi inaitwa INHOUSE INFO

Kln Investment Group(Dar es salaam) hili ni jina la biashara ,wenyewe id zao hawakuniambia japo walinifahamu pitia jf

Velx school and Office Supplies(Dar es Salaam)

Wizmark Solution (DA ES SALAAM)

Open Academy-KLM(DAR ES SALAAM)

Bilesi General Supplies(Dar)

etc......


Kwa Upande wa Company Limited


  • Elie Chansa (Arusha)Nimeshamsajilia Company(ilichukua takribani wiki mbili mpaka kukamilika......(Certificate of Incorporation ya TUCK AND ROLL COMPANY LIMITED nimemkabidhi 3rd Appril alipokuja Dar


  • KAE CREDIT AND FINANCE LIMITED (DAR)


  • J&K QUALITY SERVICE LIMITED(DAR ES SALAAM)hii ni company nyingine mpya niliyomsajilia JF member, ( April 2014 )


  • KIWALANI MICROCREDIT AND INVESTMENT COMPANY LIMITED(DAR) May, 2014 .Awali niliwasajilia kama business name na ilikuwa ni KLN INVESTMENT GROUP miezi minne iliyopita


  • Pia nimefanya kazi na jf member wa id ya GreenHouse(Dar ) limited company yake inafanya kazi rejea thread yake jukwaa hili la ujasiliamali



  • JAE & BOMA LIMITED (Hai ) JUNE 2014, nimeanya kazi na jf member wa hii Id Simburya.



  • COMMUNITY SUPERMARKET & COMPANY LIMITED (Dar es salaam)30 JUNE 2014 nimekabidhi kazi

etc...............

Nawashukuru wote wanaondelea kuniamini kufanya kazi na mimi huku hawanijui zaidi ya hii JF ID,mnanijengea CV nzuri kwa kazi za mtandaoni hasa kuhusu usajili.

Nawakaribisha wengine niwasaidie aidha kwa ushauri ama kwa vitendo kuhusu usajili wa Business Names na Company Limited.

Niliowataja IDS zenu samahani kama itawaletea usumbufu,ila nimefanya hivi ili wengine ambao hawajafahamu kuhusu kazi ninazofanya ,basi wafahamu na wawe na imani kupitia ninyi

---------- Updates

kuhsiana na gharama za usajili kwa mujibu wa Brela kuanzia company ya mtaji mdogo kabisa hadi mkubwa zaidi soma post na 28 kwenye hii thread .(KUANZIA JULY 1 2015 GHARAMA ZA BRELA ZIMEPANDA NITAZIWEKA KAMA ZILIVYO KUANZIA JINA LA BIASHARA ,CHARITABLE COMPANIES,NA PRIVATE COMPANY LIMITED BRELA
 
Gharama za kisajili Business Name ni shilingi ngapi kwa Ujumla?
 
Gharama za kisajili Business Name ni shilingi ngapi kwa Ujumla?

Ukinipa 40,000 Tshs Certificate of Registration unapata ndani ya week mbili.

.....updates.....

(KUANZIA JULY 1 2015 BRELA WAMEPANDISHA GHARAMA)
 
Nikupe Elfu 40 za nini na wakati kusajili kampuni ni Elfu 18 tu ?

kusajili jina la biashara ni sh 6000 tu na si 18 elfu(labda uniambie ni nchi gani nami nikasjili company yangu huko), nafanya 40 kwa sababu huwa napanga foleni bank,kisha kwa Muhasibu Kisha natumia nauli kufuatilia maendeleo ya kazi, nadhani umenielewa mkuu, na pia sikatazi mtu kufanya mwenyewe ikiwa ataona anweza ufuatiliaji na anajua abc za usajili, hata ukiniomba ushauri ukasajili mwenyewe nitakupa ushauri bure
 
Mkuu uko sahii kunaupotevu wa mda na uaumbufu wa hapa na pale.
 
Jukwaa la Wajasiriamali linataka watu waaminifu wa aina hii, maana huyu jamaa anapotray real life, na si virtual world kama wengine wengi tunavyofanya.

Mahusiano ya nyuma ya screens yanatakiwa hatimaye yawe productive kama hivi alivyofanya mwanajamvi.
Kwa wenye shaka bado, huyo member Chasha ni jamaa yetu tuko nae Arusha na mjasiriamali aliyepiga hatua.
Binafsi nakupongeza sana mkuu Singo kwa kufaidisha wanajamii kwa kwenda hatua ya ziada nje ya computers.
 
Last edited by a moderator:
Nikupe Elfu 40 za nini na wakati kusajili kampuni ni Elfu 18 tu ?

ghalama ya business names elfu 40? Wapi na wapi bhanaaaa?business name ni sh 6,000/ labda utuambie ghalama za kusajili limited company mkuu
 
ghalama ya business names elfu 40? Wapi na wapi bhanaaaa?business name ni sh 6,000/ labda utuambie ghalama za kusajili limited company mkuu

nitaweka gharama za usajili wa Company Limited ,kuanzia mtaji mdogo kabisa mpaka maximum , kwa mujibu wa Brela. Hiyo elfu 18 sijui kaipata wapi, nasikitika sana kuona watu wanakurupuka kujibu vitu wasivyovijua, ni bora kukaa kimya ama kuuliza ili ujue
 
Ukinipa 40,000 Tshs Certificate of Registration unapata ndani ya week mbili.

Mkuu nashukuru sana.tofauti na pesa kuna kitu kingine ninachohitajika kikupatia.Mimi niko mwanza.
 
Mkuu nashukuru sana.tofauti na pesa kuna kitu kingine ninachohitajika kikupatia.Mimi niko mwanza.

.nitahitaji jina ama majina unayopendekeza Kutumia kama jina la biashara
.anuani yako
.aina ya biashara unayosajili,ijieleze kwa ufupi
.sehemu ya ofisi ya hiyo biashara yako
.nifahamu kwamba ni patnership au mtu mmoja sababu itaamua aina ya form itayotumika
.n.k
 
Asante sana mkuu..Shukrani sana nitakutafuta.
 
Hiki ndo kinacho hitajila hapa watu wenye uaminifu, maana sisi wabongo tunapenda vitu vya bule
Mie kwetu mwanza nigependa kujua garama za register company limited kwa mtaji wa 1million ni sh.gapi, maana nimeshajua garama zakeregister business name
Mungu akuzidishie mara 70*70*70
 
Barikiwa sana sana, hebu nipatie details za kuweka pamoja wakati wa kukupatia
 
Mkuu kama unijulishe na gharama za kufungua company pia.
 
.nitahitaji jina ama majina unayopendekeza Kutumia kama jina la biashara
.anuani yako
.aina ya biashara unayosajili,ijieleze kwa ufupi
.sehemu ya ofisi ya hiyo biashara yako
.nifahamu kwamba ni patnership au mtu mmoja sababu itaamua aina ya form nitayotumia
.n.k najaza mwenyewe

Je kuna umuhimu wa kusajili bizness name?
 
Wana JF elfu 40 ni kiasi kidogo mno! ebu fikiria mie wa Arusha ningeenda Dar piga hesabu za nauli, malazi, chakula na mengineyo ni kiasi gani! Singo fanya kazi na wale watakaohitaji ambao wanaona ni ghali wafanye wenyewe kweli umetusaidia sana. Asante sana.
 
Back
Top Bottom