SPECIAL FEEDBACK: JF members niliowasajilia Business Names na Company Limited 2013-2014

ghalama ya business names elfu 40? Wapi na wapi bhanaaaa?business name ni sh 6,000/ labda utuambie ghalama za kusajili limited company mkuu

Suende kusajili mwenyewe kwa Singo kakulazimisha?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Wewe ndiyo unakurupuka, watu wanaelewa kuwa ni elfu6, hiyo elf34 ni gharama za jamaa anayetoa hiyo huduma, mbona kasea wazi, hata hapo akitoa gharama ya mafuta au nauli na aji ya kunywa utakuta anabakiwa na elf20 au less....tatizo nini mkuu?
 
Je kuna umuhimu wa kusajili bizness name?

umuhimu upo, baada ya kusajili jina ,ukapata TIN na Leseni ya Biashara na una sehemu unayofanyia hiyo biashara,

itakunufaisha kwa kupata mkopo Bank ,Na uzuri wa mikopo ya Bank ukiwa na nidhamu nzuri ya kulipa ,unaweza fika mbali

utaweza pata tender za kusupply bidhaa zako hata kwenye office za kiserikali baada ya kujirejista GPSA

Jina hilo la biashara unaweza lifanya Company limited na ukapata kazi kubwa zaidi za hela nyingi.

Pia ni kosa kisheria kutumia jina la biashara ambalo halijasajiliwa

wengine waliosajili watakusaidia faida zake
 

Kwa Mtaji wa Million 1 ni 177200 (bei hii ni kuanzia july 2015)hii ni hela ya brela pekee. kuna gharama ambazo mimi nitacharge zitazojumuisha kazi ya search name ,kuandaa Memorandum ,na hatimaye kullipa na kufuatilia mpaka unapata Certificate ambayo ndani ya week 2 inakuwa tayari.

Gharama zangu pamoja na gharama za usajili kwa mitaji mdogo hadi mkubwa kabisa nitaweka baadaye leo hii
 
mkuu ungechangia hata buku 10 jamiiforums kwa kuwa imekuwezesha ukafanya biashara cc. Invisible
 
mkuu ungechangia hata buku 10 jamiiforums kwa kuwa imekuwezesha ukafanya biashara cc. Invisible
Panapo majaliwa nitachangia
Pia naamini na wewe mdau umeshachangia, ila kama bado ,na kwa upande wako ni muhimu pia kufanya hivyo
 
Gharama za usajili wa Company Limited by Shares

capital 200,000---------not more than 500,000 = Tsh 111,200(registration,filling fee +stamp duty)

'' 500,000---------not more than 1,000,000 = '' 141,200 ''

'' 1000,000------- '' 2000,000 = '' 161,200 ''

'' 2,000,000------ '' 3000,000 = '' 181,200 ''

'' 3000,000------- '' 5000,000 = '' 211,200 ''

'' 5000,000------- '' 10,000,000 = '' 241,200 ''

'' 10,000,000----- '' 30,000,000 = '' 262,200 ''

above 30,000,000 na kuendelea = '' 361,200 ''

NB; Gharama hizi ni kwa mujibu wa Brela, pia ikiwa umewasilisha vitabu vitatu(Memorandum and Articles of Association),ukiwasilisha vitabu zaidi ya viatatu, bei yake itaongezeka sh 5000,kwa kila kitabu ,hizi ni gharama za stamduty

Malipo yangu

nitakuchaji 180,000 ,mpaka unapata Certificate of Incorporation. Kazi niatazokufanyia itajumuisha kuandika barua ya Company Name Search(kwa kawaida majibu hutoka baada ya siku tatu) ,kuandaa vitabu vitatu(Memorandum) ambavyo vinagongwa na wanesheria sehemu 6 ambazo Directors mmesaini kugawana share za company, maelekezo ya ujazaji wa form itayoambatana na vitabu na gharama za ufuatiliaji mpaka document ina kamilika ambayo kwa uzoefu wangu ndani ya week mbili usajili unakuwa umekamilika
.

kama vitabu mtataka viwe vingi gharama zangu zitaongezeka kidogo,sababu gharama za printing na binding zitaongezeka,pia gharama nitazowalipa wanasheria zitaongezeka
 
big up mkuu tutakutafuta unapatikana wapi?
 
big up mkuu tutakutafuta unapatikana wapi?
mimi napitikana mjini kila siku za kazi, ukinihitaji tuna panga appointment tunaonana, so far ofisi yangu ni JF, ila Mungu akijalia naweza pata ofisi city center
 
nashukuru sana kk singo..mm ni mmoja wa mtu ulyenisaidia kupata bussiness name tena kwa gharama nafuu.. sikujua nianzie wapi lakini nashukuru pia hukuwa na tamaa ya pesa kwa kunipa uwazi ya njia zote na jinsi ya kufuatilia mm mwenyewe kama nitaweza.,nilikuamini na kukupatia kiasi icho kidogo cha pesa na kuweza kunfanikishia. big up sna kk... wanajf kama mtu ana tatzo na brela bas jaribun kumtumia huyo jamaa n mwamminifu.
 
Saluti kwake mkuu SINGO kwa uaminifu wake,mimi nimekua ninahamu ya kusajiri kampuni ya ulinzi lakini ninakatishwa tamaa na maelekezo ya watu.Nimewahi kusajiri kampuni kumbe nilikutana na mhuni akanipa certf's fake,wadau mwenye ujuz amwage jukwani
 
Hongera sana kwa ubunifu na hongera zaidi kwa uaminifu. Tukiunganisha nguvu zetu tutashinda tu. A luta continua!
 

Wewe ni bure kabisa aisee.unadhani kusajili ni kuwa na hiyo 6000 tu? Na hao wote waliomtumia Singo ni wajinga hawakuliona hilo? Unajifanya unajua kumbe unaungua na Jua.

Mkuu Singo wewe piga kazi,binafsi nimependa ubunifu wako na najua ugumu wa kufuatilia vitu Brela si kazi nyepesi ambayo utaiweza kama umeajiriwa au una majukumu mengine,achana na hawa vilaza.
 
03/03/2014 Nimekabidhi Cerificate of Incorporation -inahusika na usajili wa Company Limited Kwa JF member ambaye ni Mwalimu pale jitegemee Secondary Dar, ninayo furaha ya kipekee kwa sababu hii ni kazi yangu ya kwanza kwa upande wa Company Limited kufanya kazi na mtu ambaye amepata taarifa zangu jf.

Nilihusika kila hatua kuanzia kuandika barua ya Search, Kuandaa Memorandum na hatimaye kulipa na kufuatilia kazi mpaka amepata Certificate.Na muda wote wa kufanya naye kazi mimi ndio nilikuwa namfuata ofisini mpaka kazi imekamilika .

Alionesha trust kubwa kwangu,kuanzia kunipa jukumu la kuandika Memorandum kwa aina ya objects za Company yake na Kunipa Kiasi cha 241,200 kulipia usajili ,ukiacha mbali gharama zangu.Kazi imechukua week mbili kama nilivyokadiria

Kwa wewe uliopo Dar huna haja ya kunifuata ,kama utakuwa bizi ofisini twaweza onana ofisini kwako na kazi itaenda vizuri,na mlioko mikoani ama nje ya nchi huna haja ya kuja Dar ,nikiandaa Memorandum nakutumia kwenye mail kisha nakuelekeza sehemu za kusaini ,halafu utatuma documents kwa njia ya bus ama posta ama yoyote itayowezekana
 

Jina lako ni nani yaani la cheti cha kuzaliwa na kitambulisho chako? Anuani ya ofisi yako iko wapi? Kampuni yako inaitwaje (jina unalotumia kufanya biashara)? Namba za simu?
 
Jina lako ni nani yaani la cheti cha kuzaliwa na kitambulisho chako? Anuani ya ofisi yako iko wapi? Kampuni yako inaitwaje (jina unalotumia kufanya biashara)? Namba za simu?
Jina langu la cheti cha kuzaliwa sidhani kama ni issue sana ndio maana hata ambao nimefanya nao kazi nimewaorodhesha kwa jf ids zao mbali na kwamba nilifahamu majina yao halisi wakati wa kuwasajilia,utalijua utapofanya mawasiliano nami personally,ofisi sina so far japo kila siku ya kazi ni mjini kufuatilia maendeleo ya kazi zangu mbalimbali,Singo ndio jina ninalotumia kama ulivyonifahamu,JOUNE INVESTMENT COMPANY ni company yangu, nita upgrade kuwa limited Mungu akijalia, namba ya simu ipo juu kwenye post na 1, labda nikuongezee na mail kesh.west@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…