HITIMISHO!
Kwanza kabisa ninaomba kuwashukuru wooote mliochangia hii thread na kushare nami experiences zenu za Special Romantic Moments. Shukrani za pekee zimwendee Mheshimiwa Mbu kwa kufanya jitihada za ziada kutuletea picha ambazo ninaamini kabisa zitatuhamasisha kuwapa wenzi wetu some special romantic moments once in a while. Kwa wote ninawapa BIG UP and a very HUUUUUGE Hug as a way of appreciating.
Kwa kifupi picha niliyoipata hapa ni kuwa wote hapa ambao tumeshawahi kuwa na mahusiano katika maisha yetu tulishapatiwa/patia wenzi wetu hizi SRMs na tukaenjoy vya kutosha na wapo ambao mpaka leo tukijaribu kuzivuta hisia na kumbukumu zetu tutajikuta tunatabasamu kwa furaha wengine hujikuta tunasisimkwa kabisa na vinyweleo kusimama ati. So ni wazi kuwa relationship yoyote hata kama iliisha, iko katika machungu kwa wakati huu bado kuna that bright spot kwenye hilo wingu jeusi. Hata shetani naye huwa kuna siku anajisahau na kuwa malaika wajameni sema tu tunapokumbwa na maumivu, maudhi na kero huwa tunayasahau mema, mazuri yooote tuliyowahikufanyiwa na huyu muhusika.
Ninamshukuru MTM kwa kuchomekea kipengele cha Communication ambacho kwa bahati mbaya hatukupata nafasi kukichambua vizuri lakini kipengele hiki ndicho kiini kikubwa katika kufikisha jumbe zetu kwa wenzi wetu. Wengi tunashindwa ku'zungumza' kuonyesha jinsi tunavyoappreciate pale tunapofanywa watu muhimu (special) kwenye maisha ya wenzi wetu. MWJ1 hapa nimeuliza kiutani jinsi ya kushukuru lakini kiukweli huwa ninapatwa na 'kigugumizi' cha ukubwa sijui kabisa kuappreciate and that is my weakness to tell the truth and kama MTM alivyosema sometimes hadi nabore maana kama ni 'Thanx darling' ntairudia hadi naonaga aibu!
Failure to communicate your feelings kwa mwenzi wako ambaye anapaswa kuwa rafiki yako huchangia mara nyingi kwa mahusiano kuzorota na mwisho kufa na aither kuwafanya wapendanao waachane au waishi maisha ya 'mazoea'. Imagine kama MWJ1 nashindwa kuappreciate kwa kilicho kizuri je nitaweza kweli kuzielezea hisia zangu nikaeleweka kama nimekwazika/boreka au amenihurt?? (Kwa hili ninaomba msaada, kama kuna mtu anayefundisha twisheni ya hili somo tafadhani aniPM aniokoe).
Kitu kingine ambacho nimekinote kwenye trhread hii ni kuwa watoaji wengi wa SRM ni wanaume!! wanawake wengi tu wapokeaji tu (Unless tuhesabu na zile za 'faragha' ambazo nadhani hata wanaume watahusika). Wengi wetu kina dada tumekuwa (kutokana na jinsi tulivyochangia humu) tukisubiri kupewa!. Jamani tuamke, spice up your relationships, siku moja moja mtoe 'Rais wa Dunia yako" mpeleke mafichoni, ambako utamrusha ujisikiavyo. Ndio usawa wenyewe huo (Tatizo walioenda Beijing mwaka ule waliwasahau kina Bi Chau otherwise hii ingewekwa agenda ya kwanza kabisa LOL). Tusidai usawa wetu kwenye elimu, uchumi, kazi, siasa peke yake tukaisahau sekta hii ambayo ndiyo sekta mama kwa maisha yetu - matajiri, wasomi, wachumi, wanasiasa wote wanatokana na sekta hii, wanakuzwa hapa na wanarelease stresses zao hapa kwa hivyo tusiisahau jamani hata kama ni sekta isiyo rasmi!!
Mwisho ninapenda kuwashukuru wale woooote mnaowatakia mema Mbu na MWJ1 lol. I wish wishes zenu zingewezekanika. But msikate tamaa tuombeeni huku tulikoshikwa tuachiwe hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa
Ninawapenda wote. Mbarikiwe sana.
Msisahau kuwashukuru wapenzi wenu pale mnapopewa Special Romantic Moments jamani.
This Thread has been CLOSED at 6:50 PM (Kwa majira ya saa ya Tanzania).