Special Thread: Hivi Mungu hakuwa na njia nyingine ya kutuondoa duniani zaidi ya kifo?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.
 
Hiyo ndiyo njia nyingine ya kwenda sayari nyingine.

Binadamu hawezi kuhamishwa akiwa anajitambua maana ni mbishi sana.

Fikiria leo dude linakuja kuwa upande uende sehemu nyingine utoke duniani uache chura, pombe, mali na vinginevyo utaenda kweli.

Acha tuhame bila usumbufu.
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili, kama kuna mtu mwenye njia mbadala isiyo ya mateso ambayo Mungu angeitumia zaidi ya kifo aiweke hapa.
Mungu angekuwa mtu bila Shaka angewaza ayo na asingeweza kuruhusu yatokee ila kwakuwa mungu ni spirit co rais kuyatenda ayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili, kama kuna mtu mwenye njia mbadala isiyo ya mateso ambayo Mungu angeitumia zaidi ya kifo aiweke hapa.
Nimependa swali lako. Kama Mungu yupo , asingelitumia njia hii. Nasema hivi kwa vile Mungu antupenda sana watoto wake! Mungu alilipenda Kanisa lake mpaka akamtuma Mwana wake kutukomboa! This confirms, to me, kuwa Mungu hayupo. Death is a scientific phenomenon same like senescence in plants!
 
ni wazo zuri kwa kweli,na mimi ninaongezea hapo kwamba sasa hivi angesitisha kifo tuishi milele na hakuna kuzaana hata kama umeoa hakuna kutiana mimba hata ma Dr wote wa duniani wanashindwa kutungisha mimba na hiyo inakuwa ni siri yake bila sisi kujua kama amefanya mabadiliko ila mtakuja kujishitukia tu miaka ya kuishi imeongezeka umefikisha miaka 150 lakini hata mvi hauna na umekaa na mke miaka 120 hakuna cha mtoto wala mimba iliyohalibika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inabidi tuvumilie tu, maana kama kamtoa mwanawe pekee kufa msalabani kwa mateso, sisi ni nani, ila Yesu akiwa ndani yako kifo unakifurahia tu, maana unaenda kwa muumba wako, tatizo lipo kwa sisi wenye kuogelea kwenye maovu mara kuteka, kuua au kupoteza watu, utajiri w kafara, yaani kila siku unamuuzi Mungu na binadamu wenzako unafiri kifo utakionaje, na ndio yule jamaa alikuwa haendi kwenye misiba.

Hata kuishi milele kuna uzuri wake na ubaya wake, kuna wakati fukara shida zikimzidi sana atatamani kufa tajiri yeye atafurahia, wenye magonjwa sugu nao watachukia kuishi milele watatamani wafe wapumzike.
 
Inabidi tuvumilie tu, maana kama kamtoa mwanawe pekee kufa msalabani kwa mateso, sisi ni nani, ila Yesu akiwa ndani yako kifo unakifurahia tu, maana unaenda kwa muumba wako, tatizo lipo kwa sisi wenye kuogelea kwenye maovu mara kuteka, kuua au kupoteza watu, utajiri w kafara, yaani kila siku unamuuzi Mungu na binadamu wenzako unafiri kifo utakionaje, na ndio yule jamaa alikuwa haendi kwenye misiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika gani ukifa unaenda mbinguni, hizo ni amani tu ndugu yangu, maana hakuna hata mmoja aliyewahi kufa akarudi akatuambia ameonana na muumba au akatueleza mbinguni kulivyo.
 
Yesu wa Nazareth alikufa na kufufuka, huyu ndiye ushududa ambao unawapa nguvu Christians, sasa sijui wewe imani yako inasemaje katika hilo.
Una uhakika gani ukifa unaenda mbinguni, hizo ni amani tu ndugu yangu, maana hakuna hata mmoja aliyewahi kufa akarudi akatuambia ameonana na muumba au akateleza mbinguni kulivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu wa Nazareth alikufa na kufufuka, huyu ndiye ushududa ambao unawapa nguvu Christians, sasa sijui wewe imani yako inasemaje katika hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, lkn nani alikuambia Yesu alikufa, usiniambie umesoma kwenye biblia, kuna mchungaji wa SA naye alitaka kufanya igizo kama hilo lkn kwa ajili ya teknolojia kuwa juu siku hizi kaumbuka.
 
huwa hatufi tunalala tu au tunapumzika. Kifo ni siku ya kiyama kwa waliokataa mpango wa Mungu kuwaokoa kupitia Yesu.
Hayo huwa ni maneno ya kujifariji tu, hata biblia yenyewe imeandikwa hivyo farijianeni, ila hakuna mwenye uhakika mtu akifa anakuwa na hali gani.

Kila dini na mpango wake waislam, wabudha hawatumii mipango ya Yesu.
 
Nimependa swali lako. Kama Mungu yupo , asingelitumia njia hii. Nasema hivi kwa vile Mungu antupenda sana watoto wake! Mungu alilipenda Kanisa lake mpaka akamtuma Mwana wake kutukomboa! This confirms, to me, kuwa Mungu hayupo. Death is a scientific phenomenon same like senescence in plants!
Mungu yupo, ni wachache sana wanaopinga hilo, vile vile kifo kakileta yeye, nafikiri kama kweli aliupenda ulimwengu kama biblia inavyosema asingelituumbia kifo, ndiyo maana nasema badala ya kifo angetutafutia njia nyingine mbadala.
 
Hivi Mungu hashauriki au kukosolewa? Kama ni hivyo kuomba kwetu ni kazi bure.
Ni hivi, wewe ni kiumbe wake, kabla haujafikiri au kupata utambuzi tayari yeye anajua kipi kitakachotokea, sasa wewe unabahatisha haujui hatma yako, yeye anajua nini kilichopo mbele kwa uhakika. Sasa katika mazingira hayo unashauri nini? embu jitafakari
 
Back
Top Bottom