Special Thread: Hivi Mungu hakuwa na njia nyingine ya kutuondoa duniani zaidi ya kifo?

Special Thread: Hivi Mungu hakuwa na njia nyingine ya kutuondoa duniani zaidi ya kifo?

Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.
Uzuri ametupa na kusahau pia
 
Mungu hakupenda tufe ila Yesu alilazimisha akasema atumwe yeye kuja kufa kwa ajili yetu baadae akaona haitoshi na sisi tufe ili tupitie maumivu aliyopitia
 
Ukiwa muislam unaambiwa kuoa wake wengi suna kwenye ukristo et ni dhambi huoni kama hapo mnatuchanganya
Hizo Ni imani mbili tofauti. Jaribu kupima kutumia hekima ya hali ya juu sana then angalia moyo wako unakwambia Nini Kati ya hivyo vitu viwili.
Maana kweli ipo moyoni mwako.
 
Yesu mwenyewe alikufa we ninani usife
Adhabu ya kifo ilitolewa kwa sababu ya dhambi. Sasa ukishaifia dhambi unakufaje Tena?
Kuifia dhambi Ni kuishi maisha ya yesu.

Yesu wakati anakufa alikuwa anaifia dhambi na baadae alifufuka hivyo basi hafi Tena.
 
Maarifa/akili nyingi za kibinadamu, kwa Mungu ni upumbavu mtupu.
Tumwache Mungu aitwe Mungu, kwani kila alichokiweka aliona kuwa ni vema!
 
Huwa Ni furaha ya Mungu kuona mwanadamu anakufa kwa sababu kifo Ni adhabu kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Na kwa sababu Ni adhabu, basi huwa akitaraji mabadiliko ndo sababu kamweka yesu kuwanusuru wote ambao wamefyata mkia wao katka suala zima la dhambi.
Lkn Kama bado hujakoma utakufa kweli na kupotea mazima.
 
... Kwa Mungu ni mbali sana, kiasi hata ukisafiri kwa spidi ya mwanga bado utatumia mabillion ya miaka kufika!
... sasa unatokaje Duniani kufika kwa muumba wako!?
Wataalam wa fizikia wamegundua njia pekee ya kuenda mbali kihivyo kwa muda mfupi ni kutumia njia ya mkato iitwayo 'WORM HOLE', japo mpaka sasa hakuna Engineer yeyote aliyeunda 'WORM HOLE SPACE SHIP'!
Mpaka sasa ni Mungu tu ndiye mmiliki wa 'WORM HOLE SPACE TRAVEL TECHNOLOGY', ... NA TEKNOLOJIA HIYO NI 'KIFO'! ... WHETHER YOU LIKE OR NOT!
 
Maarifa/akili nyingi za kibinadamu, kwa Mungu ni upumbavu mtupu.
Tumwache Mungu aitwe Mungu, kwani kila alichokiweka aliona kuwa ni vema!
Ni Mungu mwenyewe aliyetupa akili za kuhoji.
 
Back
Top Bottom