Special Thread: Hivi Mungu hakuwa na njia nyingine ya kutuondoa duniani zaidi ya kifo?

Kwani anaye kufa ni binaadamu tu peke yake !? Kifo Kipo kwaajili ya kuendeleza uzalishaji Tu hapa duniani hkmakuna kingine hayo mambo mengine ya kiimani ni kujazana ujinga
 
Indeed
 
1)kuna ambao Mungu aliwachukua kwa njia ya tofauti na kifo yani walipaa/walinyakuliwa na kuna wengine walikuja kuchukuliwa na gari la farasi wa moto likiendeshwa na malaika.
mfano Eliya,Musa,Mariam(mama wa Yesu,na hata Yesu mwenyewe alipaa mbinguni.
Na muda mchache sana umebaki nyakati hizi tulizopo watakuwa wamelala watu wawili mmoja atanyakuliwa mmoja ataachwa,watakuwa watu wawili shambani mmoja atanyakuliwa mmoja ataachwa(UNYAKUO WA WATAKATIFU WALIOKO DUNIANI KUPAA MBINGUNI)
Yani Yesu atarudi mara ya pili kuchukua watu wake na kuwaacha wadhambi duniani nusu ya miaka 7 wakiteswa na shetani katika DHIKI KUU.
2)Kuhusu huzuni mara baada ya kuondokewa na wapendwa wako,hii ni maumbile yetu tulivyoumbwa tuna hisia tumeumbwa nazo,kuna wakati tuna furahi na kuna wakati tuna huzuni.Ndivyo ilivyompendeza Mungu atuumbe hivyo.Lakini Mungu ni mfariji wetu,na huzuni hutoweka.Ayubu alifiwa na watoto wake saba siku moja lakini hakumkasirikia Mungu wala hakuhuzunika kiasi cha kukufuru,alisema Mungu ndiye alinipa na sasa Mungu ndiye kawachukua jina lake Mungu lizidi kubarikiwa.
Hivyo haileti afya kuhoji kwa nini Mungu alituumba na hisia za huzuni.Ila Mungu ni mfariji wetu ,hutufariji na huzuni huisha na maisha huendelea.
3)Kuhusu kuwasiliana na wafu.Aisee mateso wanayopitia waliokufa katika dhambi ni makali.Kuna tajiri alimtesa masikini lazaro.Yule tajiri alipokufa akaenda kuzimu(ndio hiyo sayari yake mpya )alipata mateso makali sana.Akaomba ruhusa arudi duniani awaambie ndugu zake wasitende dhambi mana wakifa wataletwa kuzimu ya mateso.Akaambiwa haruhusiwi kuwasiliana na waliohai duniani kwa sababu kule duniani kuna wahubiri wanawahubiria kila siku waache dhambi na bado hawasikii hata wewe ukienda pia hawatakusikiliza.(communication katibya wafu na walio hai imezuiwa)
4)kuhamishiwa sayari nyingine kila mtu atahamishiwa kwenye dunia yake mpya sekunde hiyohiyo roho yake inapo acha mwili KUZIMU kuteseka au mbinguni.Sekunde hiyo roho yako inapokelewa kuzimu na kuanza mateso instantly kabla hata ya kuzikwa mwili wako huku duniani ikiwa ulikuwa mtenda dhambi toho yako inaanza kuteswa .
Kama ulikuwa mtenda mema utaenda mbinguni kwenye raha.(dunia /sayari yako mpya)
KILA MTU ATAVUNA ALICHOPANDA.instantly baada ya roho yake kutoka hakuna mdabwa kupumzika ,kulala kupumua kusubiri siku ya kiyama sijui siku ya mwisho.Wengine huwa wanajiua kabisa ili huko wanakoenda wakapumzike,hakuna kupumzika.
 
Sayansi na imani ya dini mara nyingi vinapingana.Haya maarifa ya sayansi chimbuko lake ni malaika waasi majini waliomwasi Mungu mbinguni walipotupwa duniani baada ya kufukuzwa mbinguni. Walipotupwa duniani walianzisha mahusiano na wanadamu,wakazaa na baadhibya wanadamu,wakawafundisha maarifa(SAYANSI), ILIMU YA MAARIFA(UCHAWI) ,watoto waliozaa na wanadamu walikuwa wakatili wenye nguvu na wenye maarifa sana,na waovu sana.Asili ya waliomuasi Mungu ni uongo.Ni mara chache au sio rahisi kufundisha ukweli wa uwepo wa Mungu.Japo kuna baadhi ya elimu ya maarifa kwa wachawi wakubwa hufundishwa kwa siri.
SAYANSI inakuambia binadamu ametokana na nyani ,wakati imani inakwambia binadamu ameumbwa na Mungu kwa hiyo unaweza kuchagua kuamini scientology au kumuamini Mungu.
Sayansi inasema ulimwengu ulitokana na ndharia kadhaa ila imani inakwambia ulimwengu uneumbwa na Mungu.
IMANI ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiwayo bila kuhitaji proof ya sayansi tukiongozwa na roho.
Kila mtu ana haki ya kuamini vile anavyotaka bila kuingilia haki na uhuru wa imani za wengine.
 
Ukiwa na yesu huwezi kufa
 
Mimi naamini kwamba mungu yupo ila tatizo Ni kwamba yawezekana habar zake zimepindishwa Kama ilivopindishwa habari ya idd Amin dada na yule jamaa wa zanzibar(okello)
Hakuna habari iliyopindishwa Bali umepinda wewe.
 
Kama wewe umeweza kuwepo Mungu anashindwaje kuwepo?
 
Kila nikiwaza et ipo siku ntakufa stimu huwa inakata kabisa
 
Kaafanye homework yako vizuri.

Kifo hakijawahi kuwa njia ya kukuondowa duniani.
 
Kinafanyeje kama hakikuondoi
Kifo ni neno linalotokana na Kiarabu, "Kif" maana yake ni "full stop". Kinakufa kile kilichokufa tu, ama ni kiwiliwili chqko chote au ni kimojawapo ya viungo wa mwili wako.

Ukiacha kuishi (kuwa hai) unaingia kwenye umauti. Kifo hakimaanishi kuwa umeingia kwenye umauti.

Umauti pia haumaanishi kuwa umeondoka duniani.

Kukuondowa duniani na kukupeleka kwengine ni maamuzi ya Muumba wako siyo ya mwengine yeyote.

Usichanganye, kifo, umauti na kuondoka duniani. Ni vitu vitatu tofauti.

Ukuiondolewa duniani unataka uishi wapi na vipi?
 
Kama Samia Angekua msumbufu sana kuhama.
 
Nikaishi peponi biblia yasema hivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…