"Mpanda ngazi hushuka" ni msemo wa kale ambao waswahili wengi tunaujua. Inaonekana msemo huu 'umepotezwa' maana na mzee mmoja wa Kiraracha ambaye alifanya kazi kwa bidii, akafanikiwa sana akawa na mali nyingi sana. Aliwalea watoto wake aliobahatika kuzaa WAkike na WAkiume wakarithi vizuri juhudi zake. Walifanya kazi za utafutaji mali na wakawa matajiri kuliko baba yao. Siku moja huyo mzee wa Kiraracha akiwa katika gumzo la kawaida na wazee wenzake ambao nao wanazo mali za kutosha, aliamua kuuharibu/kuukosoa huo msemo wa wahenga. Alisema:- "Nimepanda ngazi halafu watoto wangu wamekuja na kuiondoa, sasa nitashukaje?" Maana yake yeye katajirika halafu watoto wake wote wakawa matajiri zaidi ni namna gani ataurudia umasikini?
Labda tushee hii, huo msemo haujapondwa na huyo mzee wa Kiraracha?