Karl Peters aliwafunga kamba babu zetu kwa shanga na vitambaa vya kujifunga viunoni, wakati ule wafalme walikuwa wakitembea nusu uchi au wakijifunga ngozi namagome ya miti. Kuvaa kitambaa na mkewe kuulamba shanga lilikuwa jambo la kuukata kwelikweli. Leo hii viongozi wetu wenyewe wanawafuata akina Karl Peters na kutaja bei yetu hata kabla Peters mwenyewe hajawauliza. Wakiambiwa ni majemadari wa vita ya Rushwa na maendeleo ya wananchi kwa mtindo wa kuvishwa kilemba cha makuti wanavimba vichwa na kuwaona hata mama zao kule udongini ni wajinga.
Tutafika kweli?
kusema ukweli ni kuzuri pale tu ukweli utakaposemwa utaleta faida kwa sehemu husika, lakini kama kusema ukweli kutaletea matatizo na machafuko, basi kusema ukweli si kuzuri, na kama kusema uongo kutaleta furaha au amani sehemu husika basi kusema uongo ni bora kuliko kusema ukweli.Mwandishi : Anon
FANYA YALIYO MEMA KWA TANZANIA NA TANZANIA ITAKUTUKUZA KAMA ANIAVYOWATUKUZA KINA SETH BENJAMIN, NYIRENDA,Mwl. LWAKAREHE, NYERERE,SARAKIKYA,PC SOLOMON,BRAISON....NK