Snipper
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,336
- 2,171
Mkuu Upepo wa Pesa mbona umetuacha njia panda?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haujatulia bado mpaka leo Mkuu??Mkuu kabla ya yote lazima ujue spacing ya zao lako!! Ukishajua...then ujue eneo lako ni eka ngapi!!! ...na kuhusu kudumu kwa drip ina tegemea ..je utazukia au utaweka juu...na je mazingira yakoje??? Jua kali..zinakanyagwa mara kwa mara!! ?? Ngoja nikitulia ntakuja na data kamili!!!
Mkuu usihofu...bado nipo...!! Wiki hii ntaanza na basics (somo la kwanza) kabisa on what to consider kuanzia gharama...mazingira na kila kitu kama unataka kuanza kilimo cha umwagiliaji!!! Nadhani itakua mada nzuri kwetu!! Ntaku tag mkuuMkuu Upepo wa Pesa mbona umetuacha njia panda?
Itakuwa vyema sana mkuu Upepo wa Pesa. Mi mwenyewe niko na shamba langu la ekari 10 linapakana na mto wenye maji mengi muda wote huko Kilosa. Ningependa nijue ABCs za kilimo cha umwagiliaji kabla sijaanza uwekezaji.Mkuu usihofu...bado nipo...!! Wiki hii ntaanza na basics (somo la kwanza) kabisa on what to consider kuanzia gharama...mazingira na kila kitu kama unataka kuanza kilimo cha umwagiliaji!!! Nadhani itakua mada nzuri kwetu!! Ntaku tag mkuu
Asanteni sana kwa somo na ufafanuzi wa masuala haya ya umwagiliaji. Ni vipi naweza kupata na kwa bei gani kaw heka?Safi sana thread nzuri hii.... And if anyone interested na drip irrigation anione kwa maelezo zaidi... Ntamuuzia bei nzuriView attachment 425629View attachment 425630View attachment 425631View attachment 425633View attachment 425634View attachment 425635
Inbox tutaibiana,Njoo tulime kilimo chetu.
Drip zipo za level mbalimbali kulingana na level ya mkulima kuanzia Mil 1.8/Acre ambazo hazina dripper ambazo huwa zinasaidia flow ya maji japo zinahitaji shamba ambalo halina miinuko....mpka Mil 10.0/Acre.
Kwa utaalamu zaidi nicheki inbox.
Swali lako la kwanza ...dripper ni kile kitundu au kifaa kinachotoa maji kwa matone kwa jina lingine kinaitwa emitter!!Inbox tutaibiana,
We fafanua hapa, dripper ni nini??
Na tuseme heka oja ya nyanya inahitaji drip tapes za urefu gani jumla??
Ni kweli mkuu hili ni tumaini la mtanzania kwa sasa hasa ukizingatia TMA wametabiri kuna ukame unakuja!!!Nimehamasika sana na hiki kilimo
Wala usihofu mkuu nikiweka ntaku tag!! KaribuItakuwa vyema sana mkuu Upepo wa Pesa. Mi mwenyewe niko na shamba langu la ekari 10 linapakana na mto wenye maji mengi muda wote huko Kilosa. Ningependa nijue ABCs za kilimo cha umwagiliaji kabla sijaanza uwekezaji.
Tusamehe kwa hili mkuu.Mbona maswali ya msingi hayajibiwi kikamilifu?
Roll moja ya drip line/pipe ina tegemea na wewe ulivyoagiza kiwandani ila nyingi za madukani ni kuanzia mita 1000. hizi roller ziko za urefu tofauti tofauti inategemea zilivyoagizwa.Roller 1 ya drip pipe ina urefu gani
kwa 1000 mita inaanzia laki tatu mpaka nne kulingana na sehemu ulipo mkuu!na bei yake ikoje?
Nashukuru sana mkuu Upepo wa Pesa esa kwa kuendelea kutupatia elimu hii ya kutukomboa kiuchumi kupitia kilimo cha umwagiliaji. Kwa kweli kupitia mada hii mimi binafsi najifunza mengi sana. Mungu akubariki sana. Tunategemea kupata mengi zaidi.SEHEMU YA KWANZA.
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUANZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI!
Habari wana jamvi…
Awali ya yote naomba mnisamehe kwa kuto fulfill my promise kushindwa kuweka somo kila wiki kama nilivyo ahidi, okey leo nlitaka kushare nanyi kitu cha kwanza ambacho mtu anatakiwa kumbuka kama anataka anzisha kilimo cha umwagiliaji. Tumeshaona maana ya kilimo cha umwagiliaji katika pati ya utangulizi, sasa leo nlitaka tujadili mambo machache ambayo ni vyema yazingatiwe pale mtu anapotaka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji!
1. Maji na upatikanaji wa maji (availability of water)
Maji katika kilimo cha umwagiliaji ni kama mafuta kwenye gari, kwa lugha ingine kilimo cha umwagiliaji hakiwezi fanikiwa kama hakuna maji tena maji bora nay a kutosha (quality and quantity)! Kuna madhara makubwa sana ambayo yanaweza tokea kama ubora wa maji (quality) ukiwa mbovu, kwa mtazamo wangu haya ndiyo mabaya Zaidi ya yote katika kilimo cha umwagiliaji…embu angalia mashamba kama lower moshi na tpc ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiriwa na magadi/chumvi chumvi (salinity)!! Japo tunahitaji maji kwa umwagiliaji ila maji haya yasipo angaliwa yanaweza kuwa bomu baya sana kwa kilimo!! Katika part hii pia ni vyema kujua allocation ya chanzo cha maji, je kipo karibu au mbali na shamba husika!!! Je kipo mlimani au mremkoni??
2. Aina ya zao (crop type).
Tukishajua upatikanaji wa maji,sasa ni vyema tukajifunza kwanini ni vyema kujua aina ya zao kabla yaku set sistimu wa umwagiliji. Mfano kuna mazao ambayo ni lazima utumie umwagiliaji wa mifereji au boda, na kuna aina ya mazao ambayo sio lazima mfano mahindi na mboga mboga! Mfano katika drip irrigation aina ya zao itakuwezesha kupata ni mipira (drip lines) ngapi utahitaji katika eneo fulani! Hapa nitapawekea somo lake maana kuna mengi yaku cover.
3. Aina ya udongo (Soil type).
Wote tunajua tunapo mwagilia maji katika mashamba yetu maji yanaenda ardhini, basi kwanini hasa niweke sababu hii kama kigezo cha kucheki unapotaka kumwagilia shamba?? Kuna aina nyingi za udongo ila common ni mfinyanzi, kichanga na tifutifu au loam. Kila udongo una sifa yake katika kutunza maji kwa ajili ya mmea. Utunzaji wa maji wa mfinyanzi/clay ni tofauti na mchanga! Mfano clay inavyonza maji haraka na kutunza maji tofauti na mchanga!
4. Mwonekano wa ardhi na hali ya hewa (topography and climate).
Kuna baadhi ya maeneo kuna milima, miinuko na mabonde. Sehemu kama hizi mara nyingi njia inayofaa kutumia ni njia yeyote ya umwagiliaji inayohitaji presha na hasa kama kuna milima na maji niya kupandisha mlimani. Kama eneo liko tambarare umwagiliaji wa mifereji unaweza tumika tofauti na kwenye miinuko! Umwagiliaji wa mifereji kwenye milima unaweza faa kama mifereji itawekwa across the slope na pia angalizo lichukuliwe kuangalia spidi ya maji ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi!
5. Mazingira (environment)
Maji yanahitajika katika kila sekta inayomuhusu mwanadamu, japo maji ni uhai ila maji yanaweza hatari zaidi ya bomu kama hayatatumiwa kwa uangalifu yakinifu. Maji ya umwagiliaji yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa hasa kichocho (water borne desease), malaria (water related deseases) na hata kuwa maficho ya wanyama hatari. Magonjwa na mmonyoko wa ardhi unachangiwa sana umwagiliaji wa mifereji na kutumia boda system kama za kwenye kilimo cha mpunga. Maji pia yanaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa udongo hasa katika miinuko. Ni vyema kabla hujafikiria kutumia umwagiliaji ujue pia ni vyema ukaangalia mazingira yako na jamii pia.
6. Cost/gharama
Kukiweka cha mwisho haimaanishi kwamba hakina umuhimu, na nnaeza sema nimeweka mwisho ili iwe rahisi kukumbuka! Kuna njia nyingi za umwagiliaji, kuna ambazo ni za gharama ndogo mfano umwagiliaji wa mifereji na kuna ambazo ni za gharama kubwa mfano drip irrigation systems, centre pivot na sprinkler irrigation systems. Mifumo hii kwa namna moja au ingine inahitaji gharama kubwa katika kuianzisha na pia muda mwingine katika kuiendesha. Pia inakua logical kama utatumia mifumo ya gharama kubwa katika kilimo chenye faida kubwa mfano kilimo cha high valuable crops nyanya, kabeji na mengine yenye uhitaji mkubwa sokoni!!
Hizo ni baadhi tu, ziko nyingi! nakaribisha mawazo na challenge hasa washika dau katika sekta hii
Link Things to consider before you start to irrigate
Snipper Red Giant sun Shark moniccca iyengamuliro
Nashukuru sana mkuu Snipper ! Irrigation ni pana sana, ki uhalisia bado tunahitaji mapinduzi makubwa kwenye kilimo hasa cha umwagiliaji! mamlaka ya hali ya hewa walitangaza kutakua na upungufu wa mvua hasa miezi hii!!Nashukuru sana mkuu Upepo wa Pesa esa kwa kuendelea kutupatia elimu hii ya kutukomboa kiuchumi kupitia kilimo cha umwagiliaji. Kwa kweli kupitia mada hii mimi binafsi najifunza mengi sana. Mungu akubariki sana. Tunategemea kupata mengi zaidi.
Mkuu cha kushangaza kuna baadhi ya watu inaonekana wanaufahamu mzuri lakini hawakawii kusema njoo pm. Ninapenda kilimo na ufugaji lakini sio mtaalamu wa kilimoTatzo la watanzania tunaumizana sana...mtu anataka 1.8-2m kwa drip pipes za heka moja while for io hela ukiagiza kutoka china unapata pipes za heka 5...