SEHEMU YA KWANZA.
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUANZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI!
Habari wana jamvi…
Awali ya yote naomba mnisamehe kwa kuto fulfill my promise kushindwa kuweka somo kila wiki kama nilivyo ahidi, okey leo nlitaka kushare nanyi kitu cha kwanza ambacho mtu anatakiwa kumbuka kama anataka anzisha kilimo cha umwagiliaji. Tumeshaona maana ya kilimo cha umwagiliaji katika pati ya utangulizi, sasa leo nlitaka tujadili mambo machache ambayo ni vyema yazingatiwe pale mtu anapotaka kuanzisha kilimo cha umwagiliaji!
1. Maji na upatikanaji wa maji (availability of water)
Maji katika kilimo cha umwagiliaji ni kama mafuta kwenye gari, kwa lugha ingine kilimo cha umwagiliaji hakiwezi fanikiwa kama hakuna maji tena maji bora nay a kutosha (quality and quantity)! Kuna madhara makubwa sana ambayo yanaweza tokea kama ubora wa maji (quality) ukiwa mbovu, kwa mtazamo wangu haya ndiyo mabaya Zaidi ya yote katika kilimo cha umwagiliaji…embu angalia mashamba kama lower moshi na tpc ambayo kwa kiasi kikubwa yameathiriwa na magadi/chumvi chumvi (salinity)!! Japo tunahitaji maji kwa umwagiliaji ila maji haya yasipo angaliwa yanaweza kuwa bomu baya sana kwa kilimo!! Katika part hii pia ni vyema kujua allocation ya chanzo cha maji, je kipo karibu au mbali na shamba husika!!! Je kipo mlimani au mremkoni??
2. Aina ya zao (crop type).
Tukishajua upatikanaji wa maji,sasa ni vyema tukajifunza kwanini ni vyema kujua aina ya zao kabla yaku set sistimu wa umwagiliji. Mfano kuna mazao ambayo ni lazima utumie umwagiliaji wa mifereji au boda, na kuna aina ya mazao ambayo sio lazima mfano mahindi na mboga mboga! Mfano katika drip irrigation aina ya zao itakuwezesha kupata ni mipira (drip lines) ngapi utahitaji katika eneo fulani! Hapa nitapawekea somo lake maana kuna mengi yaku cover.
3. Aina ya udongo (Soil type).
Wote tunajua tunapo mwagilia maji katika mashamba yetu maji yanaenda ardhini, basi kwanini hasa niweke sababu hii kama kigezo cha kucheki unapotaka kumwagilia shamba?? Kuna aina nyingi za udongo ila common ni mfinyanzi, kichanga na tifutifu au loam. Kila udongo una sifa yake katika kutunza maji kwa ajili ya mmea. Utunzaji wa maji wa mfinyanzi/clay ni tofauti na mchanga! Mfano clay inavyonza maji haraka na kutunza maji tofauti na mchanga!
4. Mwonekano wa ardhi na hali ya hewa (topography and climate).
Kuna baadhi ya maeneo kuna milima, miinuko na mabonde. Sehemu kama hizi mara nyingi njia inayofaa kutumia ni njia yeyote ya umwagiliaji inayohitaji presha na hasa kama kuna milima na maji niya kupandisha mlimani. Kama eneo liko tambarare umwagiliaji wa mifereji unaweza tumika tofauti na kwenye miinuko! Umwagiliaji wa mifereji kwenye milima unaweza faa kama mifereji itawekwa across the slope na pia angalizo lichukuliwe kuangalia spidi ya maji ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi!
5. Mazingira (environment)
Maji yanahitajika katika kila sekta inayomuhusu mwanadamu, japo maji ni uhai ila maji yanaweza hatari zaidi ya bomu kama hayatatumiwa kwa uangalifu yakinifu. Maji ya umwagiliaji yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa hasa kichocho (water borne desease), malaria (water related deseases) na hata kuwa maficho ya wanyama hatari. Magonjwa na mmonyoko wa ardhi unachangiwa sana umwagiliaji wa mifereji na kutumia boda system kama za kwenye kilimo cha mpunga. Maji pia yanaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa udongo hasa katika miinuko. Ni vyema kabla hujafikiria kutumia umwagiliaji ujue pia ni vyema ukaangalia mazingira yako na jamii pia.
6. Cost/gharama
Kukiweka cha mwisho haimaanishi kwamba hakina umuhimu, na nnaeza sema nimeweka mwisho ili iwe rahisi kukumbuka! Kuna njia nyingi za umwagiliaji, kuna ambazo ni za gharama ndogo mfano umwagiliaji wa mifereji na kuna ambazo ni za gharama kubwa mfano drip irrigation systems, centre pivot na sprinkler irrigation systems. Mifumo hii kwa namna moja au ingine inahitaji gharama kubwa katika kuianzisha na pia muda mwingine katika kuiendesha. Pia inakua logical kama utatumia mifumo ya gharama kubwa katika kilimo chenye faida kubwa mfano kilimo cha high valuable crops nyanya, kabeji na mengine yenye uhitaji mkubwa sokoni!!
Hizo ni baadhi tu, ziko nyingi! nakaribisha mawazo na challenge hasa washika dau katika sekta hii
Link
Things to consider before you start to irrigate
Snipper Red Giant sun
Shark moniccca iyengamuliro