Jumamosi ya Januari 27 beki wa Yanga Gadiel Michael alifunga goli zuri sana ambalo bado linaendelea kujadiliwa kwenye mitao ya kijamii Yanga iliposhinda 2-1. Mwalimu Kashasha alilielezea goli hilo kwa misamiati ya kiingereza.
“Hiyo tunaita triple ‘dropped baster’ kama ni mwendo wa gari basi ni kilometa 100 kwa saa kwa sababu ule mpira baada ya kupata ‘rebound’, Gadiel Michael akiwa kwenye ‘motion’ kutoka kwenye eneo lake la ulinzi wa kushoto, basi ule mpira ulikuja umenyooka nyuzi 180.”
“Hakuwa na mawazo yoyote ya kumpa mtu wala kuanzisha ‘move’ nyingine amekutana nao ule mpira akapiga ‘standard semi short’ ambayo ilikuwa hakuna namna na ilipokwenda kwa Abarola alitaka kuicheza ule mpira kwa sababu ya uzito wake ikaenda kugonga mtambaa panya au ‘crossbar’ ikarudi chini ikawa na ‘drop kick’ ikiwa inakwenda nyuzi 45, 46, imelala mshazari ikaingia goli na hakukuwa na defender yoyote wa kufanya ‘clearance’ Abarola wakati huo akiwa amelala.”
“Ni goli moja zuri.”