Hashim Rungwe ni genius, ila kuna baadhi ya Watanzania wanampuuza. Hoja zake zote zina mashiko. Bila chakula bora hakuna uhai, hakuna maendeleo.
Ukija kwenye hiyo hoja ya kupeleka Bahari Dodoma, napo kuna point! Wenzetu Waingereza na nchi nyingine zilizoendelea, kitambo walichimba mifereji (Canals) ya kutosha tu kutoka Baharini na kuelekea nchi kavu kwa ajili ya kusafirishia abiria, mizigo, bidhaa mbalimbali, nk. kutoka eneo moja kwenda lingine.
Hivyo badala ya kutegemea njia ya barabara, anga na reli, hii ya kuchimba mifereji (Canals) nayo ingefaa sana. Ingeimarisha hata utalii ndani ya nchi yetu.