Watanzania wenzangu,
Baada ya kusikia sera pofu za viongozi wa vyama babaishaji, nimekata shauri kuunga mkono sera ya ubwabwa kwanza ya legendary Hashim Rungwe kwa sababu zifuatazo:
1. Adui aombewi kitu kingine chochote, bali njaa. Unapowapa watanzania ubwabwa maana yake ni kuwafanya marafiki na kuwapa nguvu za kupambania nafsi zao;
2. Msingi mkuu au sababu ya msingi ya mahangaiko yote ya mwanadamu ni kwaajili ya tumbo lake, yaani ubwabwa hivyo ahadi nyingine zote ni sawa sawa na to put a cart before the horse;
3. Ubwabwa ni chakula pendwa zaidi Tanzania (hawsa ubwabwa na maharage) hivyo siyo vibaya tukashughulika na furaha za watu wetu kwa miaka mitano tukasahau stress za barabara, reli na madaraja; na
4. Nashauri legendary aiboreshe sera yake na kuongeza ubwabwa na maharage kwanza na fanta orange ikiwezekana
Huu ni mtazamo wangu, kama unabisha toa wa kwako au andamana.