Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Mkuu nasikia sugu na x plastaz walikua wakipiga Sana show ulaya
 
Solid Ground Family wazee bush party.

wengine ni University corner wazee wa T-shirt na jeans.

Wengine ni Daz nundazi wazee wa barua.

wengine ni Wanaume TMK(kabla haijagawanyika)

Wengine ni Nako 2 Nako soldiers hawa waliofanya madogo flani kitaa watoto wa mapolisi wakaanza kujiita Cota 2 cota soldiers wakapata hadi wadhamini.

Enzi hizo haya makundi yakiwa hai hapakuwepo na maswala ya timu,

Enzi hizo watu walinunua albamu na kuingia kwenye shoo kwa sana.

Enzi hizo tulifurahia sana muziki wa bongo bila kugawanywa kwenye makundi na bifu bifu za kishamba.

Enzi hizo mh.Jay alikuwa akitoa ngoma ni mwendo wa meseji siku hizi anaimba hadi singeli.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hivi boban hakupigwa..maana nasikia bou alipigwa mpaka akalazwa aga khan...ebu tuelezee vizur
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kalapina mnyanyua vyuma
 
Basi ile 2005' marehemu Ngwear na J. nature wakatunga ule wimbo wa mtoto wa Jakaya. Namkumbuka nature akiimba "si ndo CCM" kwenye kampeni za Kikwete.
 
Nilikuwa simpendi na kikosi chao cha mizinga. Alikuwa anatisha sana. Misuli alikuwa akiiacha nje halafu anafunika jicho moja kama chongo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu ulikua unakaa nae mtaa mmoja nin!!!! Hebu tueleze kwa kirefu
 
Nakumbuka 2003-04 Niko Sec kaole,

Basi kutoka Mwenge kwenda bagamyo kipind cha kurud Shule baada ya likzo kulikua na hiace mwenge zilikua na Mzik mzito Saaana kipind hicho asee(zilijulikana kama Paka Mweusi na Paka Mweupe) BA's maisha yalikua matam sana back then,

Na hiz ndio nyimbo zilizokua zinatamba enzi hizo


Ferooz-starehe album
Daz nundaz-nipe 5
Matonya-vailet
Mike tee-mnyalu,kama na nk
DJ yusuph-mbele kwa mbele( Jamaa namkubal sana huyu alitoa hii ngoma moja tu kaimba na hardmad alikua anaish U.K

Nikizipata aaaah mbona itakua noma, nikizipata mbona wanga watakomaa,Nikizipataa wengi watajiita jina langu, hata madem walionitosa watataka wawe wangu. HII NGOMA KALI SAANA ENZI HIZO NAIONA TVT ANAEJUA ALIIMBA NANI ANIJUZE PLZ


Black skull- watu balaa huzuaa balaa kero,

Mshikaj dem wako,-Eazy E ft suma g

Suma g vituko uswahilin

Na zingine nying ...

Aaah Enzi za Walkman
 
Hilo shindano lilifanyikaga diamond jubilee kiingilio ilikuwa buku mbili ila mwisho wa shindano ngoma walitoka droo ila yote Tisa kumi shindano LA kumtafuta mfalme wa rymes sijui ni wangapi wanaokumbuka


 
Gangwe mobb wasanii wakwanza kuvuka mipaka walimpa colabo lady mc nazizi 2000 io
 
Wateule ao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…