Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Bado yupo vizuri huwa naona anatupia picha kwenye page zake
4a83376fa5b674fb720c0bf1c615d4a3.jpg
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
D Rob Zomba (M.A.P)... KU-CREW wameachia wimbo mpya unaitwa REAL HIP HOP chini ya utunzi wa Brother Kibacha (KBC) na Brother Eazy B.. Anko Zavara Mponjika (Chief Rhymson) yupo Mbele.

Enzi hizo nakumbuka kulikuaga na ushindani kati ya KU-CREW na DIPLOMATZ ya kina SAIGON (OIIII OIIIII OIIIII)

HBC, kulikua na kichwa ki1 kinaitwa FANANI, Namkubali miaka mia hiki kichwa, mtu mmoja simple sana lakn UHAKIKA.

Sugu alipeperusha Bendera vema sana Marehemu Faza Nelly wa XPZ,

DJ BONNY LUV.. The best DJ, kautoa muziki mbali sana huyu brother, beach party 97/98 alikua anakiwasha kimeno meno.

Bring Back Our 90's
Mkuu nasikia sugu na x plastaz walikua wakipiga Sana show ulaya
 
Solid Ground Family wazee bush party.

wengine ni University corner wazee wa T-shirt na jeans.

Wengine ni Daz nundazi wazee wa barua.

wengine ni Wanaume TMK(kabla haijagawanyika)

Wengine ni Nako 2 Nako soldiers hawa waliofanya madogo flani kitaa watoto wa mapolisi wakaanza kujiita Cota 2 cota soldiers wakapata hadi wadhamini.

Enzi hizo haya makundi yakiwa hai hapakuwepo na maswala ya timu,

Enzi hizo watu walinunua albamu na kuingia kwenye shoo kwa sana.

Enzi hizo tulifurahia sana muziki wa bongo bila kugawanywa kwenye makundi na bifu bifu za kishamba.

Enzi hizo mh.Jay alikuwa akitoa ngoma ni mwendo wa meseji siku hizi anaimba hadi singeli.
 
kala pina alikuwaga anazingua sana kawazingua sana king'oko, alikuwaga anawaletea sana N2N wakija Dar kupiga show.. kuna siku pale Club billcana Lord eyez akamtolea uvivu aisee hapakutosha Lord naye kumbe ni mtemi bhana daaah alimrushia sana , kalapina akarudi sijui block 41 huko kwenda kuwachukua wenzake. Hii bifu iliendelea sana kwa muda kunakipindi bou ako akataitishwa na washkaji wa kikosi wakiwa na boban.

Wakawekeana mipaka hahahaha kipindi hicho kalapana akawa hafiki arusha ila N2N Wanapiga tu dar fresh.. Umri ushaenda walisha acha mizinguo ila pina alikuwaga ana zingua sana alikuwa anajikuta yeye pekee na kikosi ndo wanafanaya real hip hop
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hivi boban hakupigwa..maana nasikia bou alipigwa mpaka akalazwa aga khan...ebu tuelezee vizur
 
Kalapina ilikuwa too much alikuwa anajikuta msela nyaaa sana kuna halafu nilikuwa nasikia baba yake alikuwa mejaa jeshinii,

Hicho ndo kilikuwa kinamtia jeuri kuna time niliwahi kupita mitaa ya block 41 kinondoni watu walikuwa wanamzungmzia vibaya sana tabia yake ya ukorofi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kalapina mnyanyua vyuma
 
King Crazy GK kuna kikofia cha matobomatobo alikuwa anapendelea kukivaa basi nakumbuka wakati huo nipo sekondari ikageuka kuwa fasheni kwa vijana, 'kikofia cha GK'. Na pia kundi la ECT liliwashika sana vijana miaka kama ya 2002-2004, ikatokea vijana sehemu mbalimbali hasa mashuleni wakiunda vikundi na kujiita East Coast, huku wakitumia majina ya members maarufu kama GK, AY na Mwanafalsafa. Mfano ni shule yetu, kulikuwa na kikundi cha namna hiyo, East Coast baadae walikuja kufunikwa na TMK Wanaume baada ya ujio wao wa ngoma kama NYUMBANI NI NYUMBANI wakitumia style ya kucheza iliyobamba sana miaka ya 2004-2005 (Mapanga Shaaa), huku ikiwa na members maarufu kama Juma Nature, Temba, Chege, KR Mullar, Dollo, Luteni Kalama, YP & Y'DASH, Mabaga Fresh, etc. Hiyo style ya mapanga ilishika ile mbaya kwenye clubs/madisco, ikipigwa ngoma ya NYUMBANI ni NYUMBANI mademu wanakaa pembeni, tunabaki washkaji tumejipanga line tunapiga mapanga huku tukichombezwa na slogan ya (WANAUMEE.....EEEHHH).
Na kutokana na kukubalika sana kwa kundi hili ilipelekea kutumika sana kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 huku wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi na mgombea wa wakati huo wa CCM Jakaya Kikwete.
Basi ile 2005' marehemu Ngwear na J. nature wakatunga ule wimbo wa mtoto wa Jakaya. Namkumbuka nature akiimba "si ndo CCM" kwenye kampeni za Kikwete.
 
Nilikuwa simpendi na kikosi chao cha mizinga. Alikuwa anatisha sana. Misuli alikuwa akiiacha nje halafu anafunika jicho moja kama chongo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu ulikua unakaa nae mtaa mmoja nin!!!! Hebu tueleze kwa kirefu
 
Nakumbuka 2003-04 Niko Sec kaole,

Basi kutoka Mwenge kwenda bagamyo kipind cha kurud Shule baada ya likzo kulikua na hiace mwenge zilikua na Mzik mzito Saaana kipind hicho asee(zilijulikana kama Paka Mweusi na Paka Mweupe) BA's maisha yalikua matam sana back then,

Na hiz ndio nyimbo zilizokua zinatamba enzi hizo


Ferooz-starehe album
Daz nundaz-nipe 5
Matonya-vailet
Mike tee-mnyalu,kama na nk
DJ yusuph-mbele kwa mbele( Jamaa namkubal sana huyu alitoa hii ngoma moja tu kaimba na hardmad alikua anaish U.K

Nikizipata aaaah mbona itakua noma, nikizipata mbona wanga watakomaa,Nikizipataa wengi watajiita jina langu, hata madem walionitosa watataka wawe wangu. HII NGOMA KALI SAANA ENZI HIZO NAIONA TVT ANAEJUA ALIIMBA NANI ANIJUZE PLZ


Black skull- watu balaa huzuaa balaa kero,

Mshikaj dem wako,-Eazy E ft suma g

Suma g vituko uswahilin

Na zingine nying ...

Aaah Enzi za Walkman
 
Hilo shindano lilifanyikaga diamond jubilee kiingilio ilikuwa buku mbili ila mwisho wa shindano ngoma walitoka droo ila yote Tisa kumi shindano LA kumtafuta mfalme wa rymes sijui ni wangapi wanaokumbuka


Nakumbuka 2003-04 Niko Sec kaole,

Basi kutoka Mwenge kwenda bagamyo kipind cha kurud Shule baada ya likzo kulikua na hiace mwenge zilikua na Mzik mzito Saaana kipind hicho asee (zilijukana kama Paka mweusi na paka mweupe) BA's maisha yalikua matam sana back then,

Na hiz ndio nyimbo zilizokua zinatamba enzi hizo


Ferooz-starehe album
Daz nundaz-nipe 5
Matonya-vailet
Mike tee-mnyalu,kama na nk
DJ yusuph-mbele kwa mbele( Jamaa namkubal sana huyu alitoa hii ngoma moja tu kaimba na hardmad alikua anaish U.K

Nikizipata aaaah mbona itakua noma, nikizipata mbona wanga watakomaa,Nikizipataa wengi watajiita jina langu, hata madem walionitosa watataka wawe wangu. HII NGOMA KALI SAANA ENZI HIZO NAIONA TVT ANAEJUA ALIIMBA NANI ANIJUZE PLZ


Black skull- watu balaa huzuaa balaa kero,

Mshikaj dem wako,-Eazy E ft suma g

Suma g vituko uswahilin

Na zingine nying ...

Aaah Enzi za Walkman
 
Gangwe mobb wasanii wakwanza kuvuka mipaka walimpa colabo lady mc nazizi 2000 io
 
Ebana Mkuu kuna SONG FLANI LILIKUWA LINAITWAA OYA MSELA OYAA OYAA MSELAA

HIVI UNAKUMBUKA WASHIKAJI WALIOTOA LILE GOMA LILIHIT SANA MIAKA HIYO.

BILA KUSAHAU ULE WIMBO MIMI NI MSELA SIWEZI KWENDA JELA NIKIENDA JELA NINARUDI NA MAHERA DAH HATA MSANII AMENITOKA
Wateule ao
 
Back
Top Bottom