Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Bifu ya Afande Sele na O Ten
Ilaa daa AFANDE SELE sijui alikuwa ana nini mshikaji maana kuna time alianza kuwa na bifuu

1.nasikia alikuwa na bifuu na PROFESA j hadi kupelekea PROFESA asisusiee ile shooting ya wimbo wa mtazamo.

2.bifuu badae akawa yeye na yule dogo ditoo hadi dogo ditoo akajitoa kundi LA watu pori .

3.bifuu LA yeye na o ten

4.bifuu LA yeye na madee

5.bifuu LA yeye na ney wa mitego

Badae akaingia katika siasa akiwa chadema badae akajiunga ACT.

ILA MZEE afande nae katoka mbali sanaa kuna story pia niliwahi kusikia kabla ya kuwa mwanamuzki alikuwa msaidizi wa sugu kimuziki yaani sugu alikuwa anamtuma Fanya hivi Fanya vilee
 
Jamaa na Sugu wana historia, Sugu alimtoaga jamaa jeshini ndo kisa cha kuitwa Afande Sele
 
FB_IMG_1492619504898.jpeg
 
Naomba kutajiwa alieimba wimbo ule ulikuwa unapigwa sana radio free africa kipindi cha usiku wa mahaba na dr. Maganga....wimbo wa sheilaaaaa.....mshikaji analaumu sana kuachiwa demu wake sheila.
Cha ajab alieimba simjui na huo wimbo haupatikan kama zingine japo ni bonge la wimbo..sheilaaaa, niachie huyu sheilaaa.....
 
Aisee namkumbuka sana yule mdada jina limenitoka kidogo ngoja nitalitafuta ,

Namkumbuka Sean Paul alivyokuja bongo huyu mdada nilianzaga kumjua wakati aki perfom
 
Mkuu fukunyua ukipata itakuwa msaada mkubwa sana kwangu.....naupenda sana huo wimbo
 
Salama Jabir kutekwa na Kikosi cha Mizinga na kunyolewa nywele zote.

Crazy GK alipanda na gwanda za jeshi kuzindua albamu yake, aliposhuka jukwaani tu akadakwa na Wajeda wakampeleka Ngome.

Kalapina kupeleka posa ya kutaka kumuoa Mr Blue na Voice Wonder.

Rais Ben Mkapa kumpa gari msanii Feruz kwa wimbo wake wa Starehe kutokana na ujumbe mzito ndani ya wimbo huo.

Bifu la Master Jay na P funk Majani hadi wakakutana kwenue msiba wa Steve 2k wakachuniana.

Kwaleo niishie hapo...nitarudi
 
Unique sistaz walikuwa wanazindua albam yao pale Pool Side, Kilimanjaro Hotel. Mshereheshaji alikuwa Solo Thang, wasanii waalikwa kibao hadi Jay Dee ndani, kipindi hiyo ana single mbili tu. Inspekta Haroun ndio alikuwa anafunika na Mtoto wa geti kali, wahuni wakamshangilia wakambeba juu juu alivyoshushwa watu wamelamba kila kitu akaanza kupiga kelele, simu yanguuu! Ukiuliza simu yenyewe ni Ericsson. Show ya mwisho akapanda Juma Nature, jamaa kaanza kunywa gongo zamani... Juma Nature akapanda stage na P Funk, kipindi hiyo watu hawamjui ndio nani. Wakati Nature anaimba P Funk akaanza kurusha hela hewani ikawa story mpaka tunaenda Bills tunasema yule jamaa, hata jina lake hatumjui. Pale Billicanas P Funk alikuwa anapanga foleni kama watu wa kawaida tu. Dah, miaka ile mi nilikuwa nakesha kama popo, events zote nipo.
 
Naomba kutajiwa alieimba wimbo ule ulikuwa unapigwa sana radio free africa kipindi cha usiku wa mahaba na dr. Maganga....wimbo wa sheilaaaaa.....mshikaji analaumu sana kuachiwa demu wake sheila.
Cha ajab alieimba simjui na huo wimbo haupatikan kama zingine japo ni bonge la wimbo..sheilaaaa, niachie huyu sheilaaa.....

..OI BRO. FANYA HIVI..,INGIA YOUTUBE AFUU UANDIKE SHEIRA..ITAKUJA lakini ni audi version
 
Wengi e bado walikuwa hawajazaliwa ..hahahahahaha dah aseeeeeeeeeee mr.blue...""tumetoka mbaliii......pesa pesa pesaa""
 
Back
Top Bottom