Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Nikupatie tu taarifa Castro Alishatoka jela nadhani huu mwaka wa4 or wa5 sasa iLikuwa kama 2012 or 2013 na alikuja Hadi EATV na clouds
 
Anaitwa K Basil
 
Anaitwa Ester wassira
 
Aisee namkumbuka sana yule mdada jina limenitoka kidogo ngoja nitalitafuta ,

Namkumbuka Sean Paul alivyokuja bongo huyu mdada nilianzaga kumjua wakati aki perfom
Huyo ni Esther Wasira
 
King Crazy GK kuna kikofia cha matobomatobo alikuwa anapendelea kukivaa basi nakumbuka wakati huo nipo sekondari ikageuka kuwa fasheni kwa vijana, 'kikofia cha GK'. Na pia kundi la ECT liliwashika sana vijana miaka kama ya 2002-2004, ikatokea vijana sehemu mbalimbali hasa mashuleni wakiunda vikundi na kujiita East Coast, huku wakitumia majina ya members maarufu kama GK, AY na Mwanafalsafa. Mfano ni shule yetu, kulikuwa na kikundi cha namna hiyo, East Coast baadae walikuja kufunikwa na TMK Wanaume baada ya ujio wao wa ngoma kama NYUMBANI NI NYUMBANI wakitumia style ya kucheza iliyobamba sana miaka ya 2004-2005 (Mapanga Shaaa), huku ikiwa na members maarufu kama Juma Nature, Temba, Chege, KR Mullar, Dollo, Luteni Kalama, YP & Y'DASH, Mabaga Fresh, etc. Hiyo style ya mapanga ilishika ile mbaya kwenye clubs/madisco, ikipigwa ngoma ya NYUMBANI ni NYUMBANI mademu wanakaa pembeni, tunabaki washkaji tumejipanga line tunapiga mapanga huku tukichombezwa na slogan ya (WANAUMEE.....EEEHHH).
Na kutokana na kukubalika sana kwa kundi hili ilipelekea kutumika sana kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 huku wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi na mgombea wa wakati huo wa CCM Jakaya Kikwete.
 
NASIKIA ILE SAUTI NASIKIA NIKILALA NASIKIA KILA NINAPO KWENDA NASIKIIIIIIIAAAAAA ..........SAUTI YA MANKA....DAH HUYU MSELA ALIKUWA ANATOA MASHAIRI MAZURI SANA ASEEEEE SASA SIKUIZI KAKONDEANA MKAKA WA WATU MHHHH....king crazy GK ......,,,,,,,
 
Kuna moja Kalapina na wagumu wenzie walianzisha tamasha la hip hop yule teja wanamwita Chid benzi akajifanya anavamia jukwaa bila kupewa ruhusa alichezea kipondo toka kwa kalapina[emoji116]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] asiyehusika na hip hop ashuke..halafu hii ni juzijuzi tu
 
kipindi tupo kijijini likizo ukipata nafsi ya kuja dar ata wiki tu unaongea kiswahili cha dar
hiyo tu kuna jamaa yetu alipeleka msiba dar tena kwa usafiri wa mwanza dar waenzi hizo walifika usiku baada ya mazishi wakgeuza siunajua misba yetu ya dini ya kiisilamu jamaa uskiu mmoja tu dar kurudi mwanza kaja kijiweni anatuletea swaga"duuhh dar kijoto"
 
Kuna mshikaji shulen alikua na T-shirt ya East Coast basi alikua haivui kma ngozi na madem full kumshobokea kweli zamani raha
Hahaaa nakumbuka madem walikuwa wanasema wapi watampata mr. Blue awe mpenzi wao basi wavulana tunachukiaaa, haha enzi za mapozi nami by blue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…