King Crazy GK kuna kikofia cha matobomatobo alikuwa anapendelea kukivaa basi nakumbuka wakati huo nipo sekondari ikageuka kuwa fasheni kwa vijana, 'kikofia cha GK'. Na pia kundi la ECT liliwashika sana vijana miaka kama ya 2002-2004, ikatokea vijana sehemu mbalimbali hasa mashuleni wakiunda vikundi na kujiita East Coast, huku wakitumia majina ya members maarufu kama GK, AY na Mwanafalsafa. Mfano ni shule yetu, kulikuwa na kikundi cha namna hiyo, East Coast baadae walikuja kufunikwa na TMK Wanaume baada ya ujio wao wa ngoma kama NYUMBANI NI NYUMBANI wakitumia style ya kucheza iliyobamba sana miaka ya 2004-2005 (Mapanga Shaaa), huku ikiwa na members maarufu kama Juma Nature, Temba, Chege, KR Mullar, Dollo, Luteni Kalama, YP & Y'DASH, Mabaga Fresh, etc. Hiyo style ya mapanga ilishika ile mbaya kwenye clubs/madisco, ikipigwa ngoma ya NYUMBANI ni NYUMBANI mademu wanakaa pembeni, tunabaki washkaji tumejipanga line tunapiga mapanga huku tukichombezwa na slogan ya (WANAUMEE.....EEEHHH).
Na kutokana na kukubalika sana kwa kundi hili ilipelekea kutumika sana kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 huku wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi na mgombea wa wakati huo wa CCM Jakaya Kikwete.