Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Kweli nimezeeka. Kuna vijana wawili walikuwa wakisoma mlimani huku wakifanya muziki. Mmoja alikuwa Engineering akadico alikuwa akitamba na wimbo unaitwa Acquilina. Mwingine aliimba wimbo uliovuma sana "...bure mtakunywa sumu..." aliimba na Stara Thomas. Huyu aliokoka akaacha muziki.
Aliyeimba akwelina alijiita OCG
 
Enzi hizo AY alikua na kundi linaitwa CBM crew, kabla ya kujitoa na kushirikiana na King Gk kutoa single ya Miiko kumi ya Rap, enzi hizo nilikua naona kama GK anaimba kama DXM

Enzi hizo za Mabaga fresh na songi lao la Tunataabika, Enzi za akina Big Dog Pose aka BDP,
Enzi za kabla ya kufa GWM na kuunda Wachuja Nafaka,

Kipindi hicho albam pekee niliyokua nanunua ni za HBC tena kwa kujichanga nipate sh. 700/- nyimbo nyingine zote nilikua navizia kurekod kwenye kipindi cha DJ Show cha abubakar Sadik

Enzi zile Bongo fleva inapigwa kwenye Dj Show tena sio kila siku inabidi usubiri hadi jumanne kuanzia saa nane hadi saa kumi jiono na labda kwenye weekend show.
 
Uswahilini Matola na Mabaga Fresh walikua walewale ama
Uswahilini matora na mabaga flesh yalikuwa ni makundi mawili tofauti kimuziki. .......

Uswahilini matola walikuwaga watoto wa manzese ila ngoma iliyowatoaga kimuziki ilikuwa kosa LA marehemu, tumbo deni LA dunia, kosa LA marehemu rmx.
Baada ya hapo hawakusikika tena

Mabaga flesh walikuwaga watoto wa temeke na ndio kundi lilitoa Juma nature katika ule wimbo wa mtulize kabla hajakutuliza Huu wimbo ndo wimbo wa kwanza nature kusikikaaa.

Ila linapokuja swala LA kimuziki HADI Leo hii Bado wanasikikaa
 
Kuna wimbo aliuimba Duly Sykes ulikuwa unapigwa kwenye kipindi cha Sebastian Ndege, Radio One kama sikosei. Sijui nitaupata wapi?
 
Hivi nyie sna lee,blue,banana zorro,dully mbona hamuongelei ishu zao...dogo hamidu,kuna yule aliyeiimba ndoto tata
 
kwenye mkali wa rymes nakumbuka inspector harun aliingia kavaa yeboyebo na ajisifia ile mbaya eti mkali wa pamba, kipindi hicho yebo ndo yebo kweli bila 15000 huchukui!
 
Ila mtoto bana Badoo analipaa aiseee sio siri dah Mimi nilijua kazeeka kumbe Bado yupo vizuli tuu
Kwa mfano ingekuwa papuchi inasoma mitaa siingeshamaliza no zote maanaa nimkongwee mpakaa nature akamtungia kasong
 
Huyu jamaa alikuwa mkorofi sana na nashangaa sana jinsi alivyobadilika, si nasikia kipindi fulani waliwahi kumnyoa nywele kisa kawaponda kwenye video yao kipindi cha planet bongo
Toka bifu la kikosi na n2n na kalapina kumpasua bou nako kalapina hajawahii kanyaga Arusha hiii mpakaa sahivii
 
kala pina alikuwaga anazingua sana kawazingua sana king'oko, alikuwaga anawaletea sana N2N wakija Dar kupiga show.. kuna siku pale Club billcana Lord eyez akamtolea uvivu aisee hapakutosha Lord naye kumbe ni mtemi bhana daaah alimrushia sana , kalapina akarudi sijui block 41 huko kwenda kuwachukua wenzake. Hii bifu iliendelea sana kwa muda kunakipindi bou ako akataitishwa na washkaji wa kikosi wakiwa na boban.

Wakawekeana mipaka hahahaha kipindi hicho kalapana akawa hafiki arusha ila N2N Wanapiga tu dar fresh.. Umri ushaenda walisha acha mizinguo ila pina alikuwaga ana zingua sana alikuwa anajikuta yeye pekee na kikosi ndo wanafanaya real hip hop
Pina hajawahii kanyaga kipandee hiii kwakweliii maana chalii za Bronx walisemaa atachezeshewa vidaga mpaka aflot
 
Bado yupo vizuri huwa naona anatupia picha kwenye page zake
4a83376fa5b674fb720c0bf1c615d4a3.jpg
VP kale kachura kamepingua au kapo vile vile? Maana alikuwa na chura sio mchezooo
 
Mahsein Awadh kuhusishwa na kashfa ya Ugomora, Picha zake zikazagaa kwenye mitandao na kwenye magazeti ya Eric... Akajitetea alikuwa kwenye mradi wa filamu yake mpya, ... kujisafisha akaona atoe movie kweli ya "Nimekubali Kuolewa". sasa hatujui ile ilikuwa ni mradi kweli au jamaa ni MGOMORA. God Knows!
Mahsen awadh ndo nani
 
Wapi Nataka demu ya Jay usha madem wa bongo wakali wa enz zile faudhia Euginia kajala..... na likaja Goma la kufa mtu booonge la Hip hop ingekua Vipi Mwanafalsafa feat Jay mo ilkua balaa sana miaka ya 2002+.enz zile shigongo gazeti zake anaweka na Lyrics za nyimbo za bongo au America bila kusahau Billboard chart au Bamiza..
Kuna MTU anaitwa mnyalu jamani sintobadilikaaa aisee.....
 
Yeah aisee lile kundi lao alikuwepo Steve k alikuwepo john mjema na spider man ,

Lakini mwisho wa Sikh Steve 2k aliuwawa alichomwaga kisuu alikuwa ugomvi yeye na meneja wakee badae john mjema nae alijiuwaa kwa kujichoma kisu kichwanii hili lilikuwa tukio LA kusisimuaaa bila kusahahauu.

Father g yule wa arusha yeye pia alichomwaga kisu akafaa kama unamfahamu alitoaga wimbo hii ni dhambi kwa mwenyezii ukienda YouTube utaukutaa.

Halafu ivi wimbo wa Mimi sio mwizi wa alikuwepo john mjema ivi naweza kuupata wapi
Mjema kwa nini alijiua
 
DAR YA KIPINDI KILE MKUU ILIKUWA NI DAR KWELI KWELI
MIMI NILIANZA KUPANGA CHUMBA KODI NALIPA ELFU 2,

ASUBUHI CHAI ILIKUWA INAUZWA SH.50 NA VITUMBUA SH.10.

2.MCHANA UBWABWA MAHARAGE BEI 500 UKITAKA CHIPS YAI 700 NA SODA 200._

3.USIKU HIVO HIVO KAA MCHANA

4.SIKU ZA WEEKEND CLUB ILIKUWA BILICANAS , MAMBO CLUB, FM CLUB HII ILIKUWA KINONDONI KIINGILIO ILIKUWA 500 NA UKIINGIA BIA ILIKUWA 500 TENA ILIKUWA NI SAFALI LAKINI KULIKUWA NA BIA KAMA BIGWA, THE KICK BEI MPAKA 300.

HAYA NDO MAISHA DAR MIAKA YA TISINI KUJA ELFU MBILI
We kweli mkongwe
 
Back
Top Bottom