Special Thread: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Karibu tukusikilize

Special Thread: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Karibu tukusikilize

Joined
Sep 17, 2024
Posts
21
Reaction score
16
Habari wana JamiiForums,

Hii ni Akaunti rasmi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kupitia thread hii, tunakukaribisha tuzungumze na tutambue haki zetu sote

Utangulizi

Ni Idara huru ya Serikali ambayo inashughulikia masuala ya haki za binadamu na utawala bora na ni chombo cha Muungano. Ni Idara huru ya Serikali ambayo inashughulikia masuala ya haki za binadamu na utawala bora na ni chombo cha Muungano kinachofanyakazi Tanzania Bara na Zanzibar. Imeundwa kwa mujibu wa Ibara ya 129 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa lengo la kukuza, kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za binadamu na misingi ya utawala bora hapa Tanzania.

Tume ilianzishwa kufuatia mabadiliko ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, mabadiliko haya yalibadilisha Sura ya Sita (6) Sehemu ya Kwanza (1) ya Katiba iliyokuwa imeanzisha na kuelezea kazi za Tume ya Kudumu ya Uchunguzi iliyoanzishwa mwaka 1966 na kuunda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambayo ilirithi pia majukumu na kazi za iliyokuwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi.

Ilianzishwa mnamo tarehe 01 Julai 2001 baada ya kupitishwa na kuanza kazi kwa Sheria ya Tume Sura 391 ya Sheria za Tanzania na kutolewa kwa taarifa ya kawaida Na. 311 kwenye Gazeti la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na. 23 la tarehe 08 Juni 2001. Ilianza kazi rasmi Tanzania Bara tarehe 15 Machi, 2002 baada ya kuteuliwa na kuapishwa kwa Makamishna wake.

Hadi sasa THBUB inatoa huduma zake katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na mitano (5) ya Zanzibar kupitia ofisi yake kuu iliyoko Dodoma na Unguja; vile vile kupitia ofisi zake za kanda zilizoko Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara na Pemba.


MAJUKUMU YA TUME

Majukumu ya Tume yameanishwa kwenye Ibara ya 130 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Tume Na. 7 ya mwaka 2001. Baadhi ya majukumu hayo ni:
  1. Kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu, misingi ya utawala bora na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

  2. Kupokea na kuchunguza malalamiko yanayohusu uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukaji wa misingi ya utawala bora.

  3. Kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

  4. Kufanya utafiti kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora.

  5. Kutoa ushauri kwa serikali na vyombo vingine vya umma na taasisi za sekta binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora

  6. Kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani ili kuzuia vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu.

  7. Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au Taasisi yoyote inayohusika na masharti ya ibara hii katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo.

  8. Kufanyia uchunguzi masuala yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora yanayofanywa na watumishi wa Taasisi au Mashirika ya Umma na watu binafsi.

  9. Kutembelea magereza na sehemu wanamozuiliwa watu ili kutathimini na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha hali ya sehemu hizo kwa mujibu wa sharia.

  10. Kuchukua hatua za kufikia muafaka kwa njia ya mashauriano na makubaliano, aidha kwa kutoa nafuu ya kisheria au ikibidi kuchukua hatua za kisheria.

  11. Kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na vya sekta binafsi kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora
  12. Kutoa mapendekezo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za kiutawala ili kuhakikisha kuwa zinawiana na vigezo vya haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

  13. Kushirikiana na mashirika ya ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya za Madola, Taasisi za nchi za nje na za humu ndani zenye uzoefu na umahiri katika masuala ya ukuzaji na utekelezaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

  14. Kukuza na kuendeleza usuluhishi wa migogoro miongoni mwa watu na taasisi mbalimbali zinazofikishwa mbele ya Tume

Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (THBUB) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie ujumbe kupitia Private Message (PM).

Pia tunapatikana kupitia:
Instagram: chraggtanzania
Twitter: chraggtanzania
Facebook: chragg.tanzania
Website: www.chragg.go.tz
YouTube: @tumeyahakizabinadamunautaw4210

Anuani
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 339 Mtaa wa Nyerere/Kilimani
1049 Dodoma - Tanzania
Simu: +255 734 047 775
Email: info@chragg.go.tz
 
Toka tume hii ianze kuwepo hapa nchini ni mafanikio gani imeiletea nchi...?

Ni eneo lipi mnafikiri lina changamoto zaidi ktk kukiuka haki za binadamu..?

Je, katika kusimamia haki za binadamu ni kwa kiasi ama kiwango gani mnapata changamoto ktk kuingiliana na vyombo vyengine vinavyosimamia haki mfano mahakama...???
 
Tume Haki Binadamu(THBUB)
Karibuni sana jamvini, Je huwa mnakuwa na Service charges mnapomsaidia Muhanga kwenye shida yake ?

Je kunapokuwa kuna taarifa ambazo sio kamili (tetesi) huwa mnamsaidia Muhanga katika kupata taarifa kamili yenye ushahidi ?
 
Karibuni sana JF 🤝🤝

. TUHABIBO = Lingefaa zaidi
. THBUB = Naona jina ni gumu kidogo.
 
Mkuu Tume Haki Binadamu(THBUB), Msaada wenu unaopimika wenye shahidi kwa mwananchi wa kawaida ambao mumekuwa mkiutoa ni upi?.

Pia kuna kasumba ya taasisi za serikali kutokujibu michango ya wadau, vipi na nyie mmejipambanua vipi jinsi ya kukabiliana na kero hiyo kwa vitendo?.
 
Mkisaidia hapo nitawaona wa maana
 
Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au Taasisi yoyote inayohusika na masharti ya ibara hii katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo.

Tafadharini chunguzeni mwenendo wa afande Mafwele,ametajwa mno na waliotekwa na kubahatika kuokoka .Kama kweli mko huru katika utendaji wenu,isaidieni jamii kuelewa mwenendo wa huyu askari.Au mmekuja huki jf kutafuta wakosoaji wa serikari?

Au mtueleze ninyi mmefanya nini katika kupunguza tahatuki inayosababishwa na watekaji?
 
Ili kutoa kero yangu kubwa nataka majibu ya hapo juu
 
Tume Haki Binadamu(THBUB) ninaomba ufafanuzi katika mambo yafuatayo.
1. Mnaitwa tume huru, je vigezo vipi vinatumika katika kuwapata watendaji wa tume?( kama ni teuzi, je tume itakuwa huru kumuwajibisha aliyewateua ikitokea anavyunja haki?)
2. Tume huru, mnazo tafiti kuhusu mwenendo wa haki za binadamu hapa nchini? Kama zipo ingependeza mkaziweka hapa katika mfumo wa PDF ili tuzisome.
 
Back
Top Bottom