kinachonisikitisha, ni watu au wamagaribi kuwaaminisha ukrain kuwa wanaipita na kuipa tabu russia, wakati miji kadhaa ya ukraine imekuwa magofu na russia maisha yanaendelea. westerners huwa wanachukua watu ubongo halafu wanabaki makopo, kwa zana ndogo tu, media.
Kwani unajua nini kitawapata hao Russia baada ya kutolewa Ukraine? Kupigwa na kuwa magofu siyo ushindi, ukivamiwa tegemea kupigwa kwa aina hiyo maana mabomu yanakuwa yanarushwa kwenye ardhi yako huwezi kuyazuia yote yasitue.
Madhara ya vifo na uharibifu wa mali na majengo hayakwepeki lakini mpaka mwisho ndio utaona ushindi. Vita hubadilika kama upepo. Kumbuka na yeye anafanyiwa hujuma kwenye nchi yake na vita ikiisha atamlipa huyo aliyempiga.
Vita siku 3 kwamba angeshamaliza na kwenda takribani miezi 3 huoni kwamba Russia anapata matokeo ambayo hakuyatarajia?
Kama hapati taabu haw wapinzani wake unadhani wanazuia nini, kwamba wamejificha tu hawapigwi, kwanini anarudi nyuma, anarudi kwa matakwa yake?
Tangia vita imeanza hajapata hasara? Ukraine anaweza kuwa amepata hasara ya majengo na mali lakini Russia kwa silaha alizopoteza, gharama ya kuwahudumia askari wake,wafanyakazi kama madaktar na wafanyakazi wengine, majeruhi wake kuwatibu, vifo vya wanajeshi unaweza kukuta ana hasara kubwa kuliko mwenzake.
Kumbuka Ukraine hayuko mwenyewe wakati Russia yuko peke yake anayeharibu uchumi ni nani kama siyo yeye Russia. Hivyo basi tungoje mpaka Ukraine anyanyue mikono juu au atangaze ushindi, au Russia weseme wameshinda vita.
Huwezi kuwalaumu Westerners wana propaganda za media kwamba wanawapiga Warusi wakati huo huo Russia naye anasema amepata ushindi mkuu juu ya Ukraine wakati pia tunaona hujuma zikifanyika nchini mwake na Ukraine hajatangaza kusalimu amri.
Mfano mzuri angalia vita ya Vietname na US,Vietname walipata hasara kubwa watu kufa, askari na miundombinu lakini je walishinda ile vita? Muda bado upo tungoje hadi mwisho.