Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Putin katangaza Martial Law
Akifanya hivo ndo inamsaidia kushinda vita.? Hiyo inazuiaje mashambulizi na kipigo wanachopewa? Itazuiaje wana jeshi wake kutouawa kwa kiwango kile?

Huenda Putin alishapata ukichaa. Hayuko sawa.

Safari hii kanasa, alishalikoroga lazima alinywe tu. Anga la Ukraine likilindwa vyema na kuthibiti makombora na Drone zake atakuwa hana ujanja tena.
 
Hilo litakuja tu, ni muda ndo utakaohamua. Wahenga walisema" Siku ya kufa nyani, hata ile miti aloizoea kupanda huteleza" Majigambo,Vitisho vyake na Ubabe hakuna kinachomsaidia askari wake wasiuawe kwa wingi kwa kiwango kile. Huku akiendelea kutapatapa, askari wake na silaha nyingi vinaendelea kutwangwa na kuteketezwa. Inaonekana upo mpasuko mkubwa ndani ya jeshi lake na hata kwenye Utawala wake.
 
Mhhh! Hapo ndio patamu. Ikishaingia hoja ya Udini basi ujue kila kitu na mikakati ya kivita vitasambaratika. Ogopa sana mambo ya Ki-Imani e.g. hapo 👆 👆 tu inaonekana mizoga 9 ya wanajeshi wa Warusi waliotwangana risasi wenyewe kwa wenyewe kisa ni mabishano ya kiDini.
 
Baada ya kuona anashindwa zuia offensive ya Ukraine kaamua haribu miundombinu ya umeme
 
Baada ya kuona anashindwa zuia offensive ya Ukraine kaamua haribu miundombinu ya umeme
Ndo maana wanaitwa Magaidi. Mfano wanataka Kubomoa Bwawa la Umeme la Dnipro. Wakati Umeme unaenda hadi Crimea. Ni dalili za kushindwa. Eti wanataka mji wa Kherson ukumbwe na Mafuriko. Raia wengi watakufa kama kingo za Bwawa zitabomolewa. Na haizuii Ukriane kusonga mbele.
 
Labda ndiyo maana wanajaribu sana kuhamisha raia ili baadae wabonoe hilo bwawa kukwamisha jitihada za kijeshi.
 

Ni akili matope. Ndiyo maana tunasema wamechanyikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…