Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Hawawezi kupeleka hivo vifaru bila Germany kuruhusu. Ukifanya hivo spare utatoa wapi. Support ni muhimu sana. Labda wanajaribu kuweka pressure zaidi, lakini Germany kakataa kabisa. Huenda ana sababu za msingi.
Wanaweza. Vifaru ni vyao japo walivinunua Ugerumani. Ni sawa na mtu akunyime kinu halafu nikuambia chukua changu.
 
Wanaweza. Vifaru ni vyao japo walivinunua Ugerumani. Ni sawa na mtu akunyime kinu halafu nikuambia chukua changu.
Na kwa kutokana na wewe kunipa kinu chako, utakuwa umeniwezesha na hiyo kazi iliyokusudiwa itafanyika.
 
Sio rahisi kwa kweli..
 
Siwaelewi mnachobishania. Je ni neno "Tank", "Howitzer", au "self-propelled"

Naombeni mjisomee muyaelewe hayo maneno ili msiendelee kubishana na kuonyesha watu nani haelewi na nani yuko sahihi.

Kwa uelewa wangu mnazungumzia kitu kile kile ina mnashindwa kuelewa maana ya howitzer na self-propelled.

Anayesema PzH 2000 ni self-propelled Howitzer yuko sahihi.
Anayesema PzH 2000 ni kifaru (tank) naye yuko sahihi.

Aina ya mtutu na trajectory angle uliofungwa juu ya truck ndo ina determine kama ni Gun, mortor, Howitzer au artillery.

Tuendelee kujifunza, na kubishana ni njia nzuri ya kujifunza ili mradi hatukwazani.
 
Wanaweza. Vifaru ni vyao japo walivinunua Ugerumani. Ni sawa na mtu akunyime kinu halafu nikuambia chukua changu.
Nchi za EU zina vifaru vingi sana vya Leopard 2, zikiamua kupeleka hata kila nchi vifaru 30 tu idadi ya vifaru anavyotaka Ukraine 300 zinatosheleza kabisa.

Issue kubwa itakuwa ni support na kupata vizuri vyake. Akikubali Germany itapenseza sana.
 
Yeah! Huwezi kujua au kufahamu kila kitu (A jack of all trades) lakini zaidi inapendeza sana pale tunaposhirikishana yale tunayoyafahamu au kupeana uzoefu. Sisi tulioishia JKT au Mgambo tunafurahi sana kusoma jinsi wabobezi wanavyotufunulia mambo ya kijeshi/vita yanavyokuwa ikiwa ni pamoja na support ya video clips. Tunashukuru kwa kweli. Slava Ukraine.
 
Umechanganya na kopi ya kichina ya nne toka juu.
Ni kweli, hili gari linaitwa Dongfeng Mengshi, ni Generation ya hizi HMMWV. Sema zinatengenezwa kwa kibali cha USA sababu ni technology yao. Hayo Magari msituni ni balaa. Hata ukifuatilia utakuta chassis zake zinatumia za Hummer

Usifikiri kila kinachotengenezwa china ni fake. China kwenye Magari ya kivita wapo Vizuri mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…