Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Bila hatua madhubuti kuchukuliwa Bakhmut na miji mingine itachukuliwa na Wagner muda si mrefu.

1. Kukosekana kwa tanks, Artillerys, vehicles na risasi za kutosha direction ya Bakhmut kutafanya muda si mrefu Bakhmut na miji mingine kuchukuliwa na Wagner/Russia. Ni ukweli kwamba Wagner wameharibu tanks na Artillery za kutosha eneo la Bakhmut, Soledar na salt mine. Hali siyo nzuri kwa Ukraine kuhusu vifaa.

2. Kucheleweshwa kwa tanks, Artillery, Vehicles na risasi kumeshusha morali ya wanajeshi wa Ukraine direction ya Bakhmut. Moral ya wapiganaji ikishuka usitegemee kupata ushindi. Askari wanataka tanks za kisasa wampige adui.

3. Frontline ya Ukraine direction ya Bakhmut imezidiwa sababu ya uchache wa tanks, artillery, MLRS na risasi.

4. Russia wamepata moral ya ajabu direction ya Bakhmut na Vuhledar. Hawajali wanauliwa kwa kiasi gani, wanapambana kufa na kupona. Hii siyo dalili njema kwa Ukraine na washirika wake.

5. Kama waliyosema USA na Germany ni kweli kuwa Abrams, Leopard 2 na F-16 zinaweza kufika June, sababu ni complex tanks na fight jet, kwamba kufundisha wanajeshi wa ukraine kunahitaji muda. Kwa hali hiyo huenda miji ya Slovyansk, Kramantorsk, Pavlohrad, Dnipro, Nikopol na Zaporizhzhia zitakuwa mkononi mwa Russia mpaka huo mzigo unafika.

6. Ukraine inahitaji powerful air defense system ili kuzuia Hypersonic missile ambazo Russia ameanza kurusha. Patriot na SAMP/T zinahitajika haraka Ukraine. Kichaa cha Putin kimeshapanda maana anayateketeza majengo na miundo mbinu yote iliyoko mbele yake. Ni jini linalotaka damu ya wa Ukraine.

7. Kama NATO hawatapeleka hizo tanks na wataalam wa ku operate F-16, Abrams na Leopard 2 mapema na kusubiri mpaka wanajeshi wa Ukraine watoke mafunzo hiyo June basi hali inaweza ikawa mbaya kwa Ukraine. Indirect Intervention ya NATO inahitajika kummaliza nguvu Russia.
 
Mkuu huwa nakubali uchambuzi wako sana pamoja na Missile of the Nation .
Tumezidiwa sana kwa sasa hadi inatia uvivu kufuatilia mwenendo mzima kuja kuwarudisha tena hawa jamaa nyuma itakuja kuwa ngumu sana.
 
Mkuu huwa nakubali uchambuzi wako sana pamoja na Missile of the Nation .
Tumezidiwa sana kwa sasa hadi inatia uvivu kufuatilia mwenendo mzima kuja kuwarudisha tena hawa jamaa nyuma itakuja kuwa ngumu sana.
Jamaa wanapiga offensive kuizunguka Bakhmut sisi tumebaki kukanusha kuwa mji fulani hawajaukamata wakati jamaa wameshauteka. Niliposema kuwa Soledar na miji mingine iko under control ya Russia kuna watu Walikataa katakata. Baada ya Ukraine ku retreat ndo wameamini.

Tutalazimika ku retreat Bakhmut sababu njia kuu kwa upande wa kaskazini na kusini mwa Bakhmut ziko under fire control of Russia troops. Supply logistic imeanza kuharibiwa na adui. Russia wame copy na ku paste strategy ya Ukraine troops za ku paralyze supply route ya adui.

Kuna urgent needs ya modern tanks Bakhmut ili tuweze kuwafurusha hawa Katsaps.
 
Yaani mara mia Mji Uchukuliwe kuliko vifaa vya jeshi kutekwa au kuteketezwa. Pia hali ya hewa imechangia.. Njia za Pori hazipitiki.

Mimi bado nawapongeza Ukraine sababu ukilinganisha nguvu ya Ukriane na Urusi, ni kama mara nne yake. But wanaweza wakazui mji usichukuliwe hata miezi 5.

Lazima kuwepo na mipango mikakati. Ungekuwa ni mji wa kuzui usichukuliwe ilikuwa ni Mariupol. Lakini Ukraine iliachia.. Tangu 2014 ni mara ya nne Ukraine inapoteza Mji wa Mariupol lakini baada ya muda unarudi. Hivyo kuna miji hata ikichukuliwa itarudi tu hata baada ya miaka 10. Mfano Odessa, Mariupol Bakhmut na hata Dnipro. Bado wafuasi wa Ukraine inabidi watambue sisi tunategemea nguvu za washirika kwani peke yetu hatuwezi. Pia jeshi la Ukriane limeiva.

Pia tuliamini jeshi la Ukraine. Kumbuka pia asilimia kubwa ya Vifaa vinavyo tumika sasa vingi ni vya Urusi wanatumia. Kuna sehemu Ukriane wanamudu then wanawaachia Urusi waingize vifaa vya Jeshi ili Wavizingire wapate Silaha na Risasi. Tumeiona ikifanyika Kherson na kharkiv. Silaha zilizotekwa zimetumika kuikomboa Izyum na Bakhmut hadi soledar na Sloviansk. Tuwapongeze wanajeshi wa Ukraine kwani bila wao hakuna wa kutupigania na hawana makosa.

Kila siku hatuwezi kushinda sisi tu.
 
Kuwatoa Russia kwenye territories za Ukraine hilo halina ubishi inyeshe mvua au jua. Wanajeshi wetu wakitoka mafunzo na mzigo ukafika wote, itakuwa hamna namna lazima afurushwe. Ni swala la.muda tu.

Nachokiona Russia atakuja kujikita kwenye kurusha Hypersonic ballistic missile zake kwa ajili ya kufanya uharibifu wa miundo mbinu.
 
Mwanangu sijakuelewa kwani hii si vita mzes kushinda battle moja au mbili sio kushinda vita mzee mnona unaongea kama vile huna experince na vita kaka

Sikia kwa sasa Ukrain inakabiliwa na uhaba wa vifaa na silaha za vita kwa maana bile walivyokuwa wamepewa ndo walivitumia kurudisha ile mini na mioa yote waliyorudisha kwaiyo kwa sasa silaha ziko njiani

Ngoja ziwafikie alafu utaona icho unachokisema kama warusi hawataitema iyo miji yote na kurudi Ukraine

Ni lazima tufike hatua tukubali kwamba kwa idadi ya siraha Russia amemzidi mbali sana Ukraine kwaiyo nguvu ya Ukraine inatoka kwa washirika wake namaanisha siraha na vifaa vya kijeshi anavyosaidiwa ndo vinamfanya akomboe miji na vijiji,

Mfano rushia anaweza kurusha shellls mpaka 200 kwa siku lakin ata kama watakosea target basi watarudia kufanya vile vile mpaka waipate target,

Sasa Ukraine hawezi kufanya ivyo ata siku moja ukraine ana shell ndogo na pia analazimika kuzitumia kwa hesabu kali sana naamini umenielewa acha mambo ya kuilaum sana Ukraine na wakati unaijua hali yake halisi kivifaa mzee

Kinachopigana vita sio maneno wala wagu kinachopigana vita ni siraha bora na watu jasiri niamini mimi

Ukraini ana watu jasiri mara tano ya warusi ila siraha ndo ana upungufu ngoja aongezewe mzigo alafu tutarudi apa kujadili mpaka wiki ha pili ya mwezi ujao mamilion ya silaha yatakuwa hamefika ukraine na utarudi apa kuniambia
 
Mtakuja kuniambia jinsi Russia wameingia kwenye ambush. Halafu nimegundua pia West na Ukraine kuna vitu wanavisema hadharani ili kumwaminisha adui kuwa wamezidiwa. Hata hizi tanks zinazoombwa usishangae tayari zipo Ukraine.
 
Mkuu huwa nakubali uchambuzi wako sana pamoja na Missile of the Nation .
Tumezidiwa sana kwa sasa hadi inatia uvivu kufuatilia mwenendo mzima kuja kuwarudisha tena hawa jamaa nyuma itakuja kuwa ngumu sana.
Mkuu samahani, hii ya kuona uvivu kufuatilia ni wewe. Sisi wenzio tunafuatilia kuanzia Frontline hadi mipango ya Urusi na ile ya NATO.

Kuna majukumu lazima yaendelee. Sio kila siku utakuwa online kitegemea na Mazingira. Sio kila sehemu kuna intaneti pia kuna Uchovu. Mimi nipo na Ukraine hadi dakika ya mwisho wa piumzi yangu na nitaitetea Ukraine hadi tone la mwisho la damu yangu. Nimekushangaa unachoka kufuatilia. Vipi ungepewa mtutu? Ungeuza kambi na kusaliti. Timu inafanya vizuri unailaumu, vipi ikifanya vibaya? Soledar na Bakhmut ni sehemu ndogo sanaaaa....! Ingekuwa imechukuliwa mikoa mitano tungewaza lakini kuchukuliwa kata ituvunje moyo? Hapana. 💪
 
Hahaa mkuu hapana niko na Ukraine mpaka mwisho wa safari hata wakishindwa ila bad news zina ni discourage kuchimba sana habari sababu najua nitakutana na habari mbaya upande wetu tu.
 
Nimesoma uchambuzi mmoja mahali fulani wanasema hivi, Strategy ya Urusi kwa sasa ni

1.Strategically hawajali tena idadi ya askari wao wanaopoteza. Putin anaamini kuwa Kama Taifa la Urusi litaweza kuvumilia na kufumbia macho idadi ya askari wake watakaokufa vitani basi kuna uwezekano wa kufanya vizuri

2. Pili, Kamandi ya Urusi imeamua miji ya Soledar na Bakhmut kuwa eneo la kutrap vikosi mahiri vya Ukraine ili viende pale viwe kept busy na mapigano ili kuviondolea Luxury ya kupumzika na kupanga Counter offensive nyingine kama waliyoifanya kule Kharkiv na Kherson. Kwa hiyo Urusi inatuma wave after wave ya askari wake katika positions za Ukraine ktk maeneo hayo bila kujali inapoteza askari wangapi.

Kinachonipa matumaini.
1. Vita ni uchumi, na uchumi wa Urusi kutokana na vikwazo kiukweli hauwezi kusustain vita ya muda mrefu.

2. Washirika wa Ukraine wameshaingia ktk hili gemu kwa miguu yote. Wanajua vizuri kuwa iwapo Urusi atashinda, Watapoteza power na ushawishi wao duniani kwa hiyo wataendelea kumsaidia iwe mvua iwe jua. Ukraine akipigwa ni aibu kwao na itamcost Biden uraisi 2024

3. Ukraine anachotakiwa kufanya ni kuendelea kupiga logistics na Command centres, ili hawa askari wa urusi walio msitari wa mbele wakose support ya vifaa, madawa na chakula
 
Hahaa mkuu hapana niko na Ukraine mpaka mwisho wa safari hata wakishindwa ila bad news zina ni discourage kuchimba sana habari sababu najua nitakutana na habari mbaya upande wetu tu.
Zingine ni propaganda. Mfano habari gani? Shukuru kwa kile ulichonacho. Wapi jeshi limepoteza ambapo ni Muhimu? Izyum ipo Ukraine vipi ingetekwa? Si ungelia kabisa? 🤣🤣🤣
 
Hii Wasahau. Hii miji kuna Askari wachache wa Ukriane. Wakati Urusi wanaenda physical, Ukraine wanatuma Teknolojia ikiwemo drones.

Nawashukuru jamaa wa HIMARS wanasaidia kuintong'onyesha Urusi. Mfano usiku wa leo Urusi ilikuwa inapakuwa mzigo wa silaha na Risasi kule Donetsk ila wote umeteketezwa na HIMARS
 
Good analysis with factual.
 
1. Naunga mkono hoja. Kwa plan hiyo watakufa sana bila ku-achieve chochote. Ukraine inatumia technology kujua adui amekaaje na yuko wapi' siyo ŕahisi kuwa-trap.

2. HIMARS au M270 ni machine hatari sana, laiti Russia wangekuwa na uwezo wa kuteka hata HIMARS au M270 moja tu, wangepiga propaganda sana.
 
Shikamoo wazee wa HIMARS. Urussi wakalete tena mzigo mwingine na wembe ndo huo-huo.
Slava Ukraine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…